Serikali isipuuze tamko la APHFTA kusitisha matumizi ya bima ya NHIF kutibiwa hospitali binafsi. Yanazungumzika

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Tangu Mwenyekiti wa Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya nchini (APHFTA), Dk Egina Makwabe atangaze azimio la vituo vyote vya afya kutaendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wapya wa bima ya NHIF kuanzia Machi 1, 2024, hakuna response yeyote kutoka upande wa serikali kuhusu tamko hilo.

Je, tuamini kwamba serikali itatumia ubabe kuvilazimisha hospitali binafsi kupokea wateja wa NHIF au nini hatima ya wagonjwa wenye bima hiyo?

barua ya Chama cha wamiliki wa hospitali binafsi (APHFTA) imeeleza wazi kutoshirikishwa kwa wamiliki wa hospitali binafsi kwenye mchakato wa maandalizi yote ya Kitita Kipya cha huduma za Bima ya NHIF. Imeeleza wazi kuwa vyama vya manesi na madaktari walihusoshwa na mchakato huo. Na bahati mbaya sana wamiliki ws Hospitali binafsi walipeleka maoni yao ambayo yalitupwa katika majumuisho ama ukamilishaji wa kuandaa kitita hiko.

Serikali inapaswa kufahamu kwamba hatma ya wanachama wa NHIF ipo shakani pale ambapo watakoanza kukosa huduma za afya kwa kigezo cha kuondolewa kwenye mfumo wa kupokea huduma kutoka hospitali binafsi nchini.

kuna malalamiko kutoka kws wamiliki wa hizi hospitali binafsi kwamba malipo ya bima ya afya huchukua muda mrefu sana kulipwa kutoka NHIF hivyo kupelekea kuyumba kwa utoaji huduma.

Wamiliki wa Hospitali Binafsi nchini kupitia APHFTA wametoa angalizo la anguko la hospitali binafsi na kufilisika kabisa endapo sheria hiyo mpya ya NHIF itaanza kutumika. Serikali inawajibu mkubwa kuimarisha sekta binafsi ili iweze kukidhi pengo la uhakika wa hiduma bora za afya hasa baada ya serikali kuzidiwa.

waziri wa Afya anapaswa kusimama kwenye nafasi yake kutatua huu mtanziko unaoenda kuzua taharuki kuanzia tarehe 1 Machi 2024. Tunaiomba serikali isipuuze bali busara itumike kwenye hili.
PIA SOMA
- APHFTA: Tutasitisha huduma za NHIF kuanzia saa sita usiku, wagonjwa mahututi tutawaongezea saa 48


CC: Wizara ya Afya Tanzania
 
Back
Top Bottom