DOKEZO Hospitali ya Mloganzila inatumia wanafunzi (interns) kuhudumia wagonjwa mahututi, na manesi wana huduma mbaya, mnatumaliza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari,

Nimepoteza mtu wangu wa karibu sana siku ya jana kutoka Hospitali ya Mloganzila 😭😭😭😭😭😭😭.

Hakuna daktari pale, kuna wanafunzi (interns) tu wanaotoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa aliye mahututi, hawana uzoefu, wanabahatisha, kauli zao zinapingana, hawajui walifanyalo.

Mashine zao ni mbovu, manesi na wauguzi wanachukua muda sana kumtembelea mgonjwa, hawajali kabisa, wana majibu mepesi sana kwenye maswali magumu.

Amana ina huduma mbovu sana, Mloganzila ina huduma mbovu sana sana, samahani kwa unandishi mbovu, nimempoteza mama yangu mzazi kwa huduma mbovu za hospitali zote hizo.

Kama unampenda ndugu yako, sikushauri kumpeleka huko.

Mloganzila kutwa kucha kijisifu tunaondoa mara uvimbe kwenye ubongo, na blah blah kibao, hakuna kitu pale!

Surgery ndogo wameshindwa kunmfanyia mama yangu na kunipa jibu fupi kwamba haiwezekani, kesho yake daktari mwengine wa zamu (mwanafunzi intern), ananambia nisubiri Jumatatu anakuja neurosurgeon, sasa huyo surgeon wa nini ilihali dokta (intern) wa zamu wa mwanzo kaniambia surgery haiwezekani?

Interns mmoja anachezea simu, mama yuko chumba cha X-Ray, yeye yupo nje ya chumba busy na simu, mwenziwe anamuita, njoo huku, mpaka kamfuata na kumvuta kwa nguvu arudi kwa X-Ray Room, yeye bado yuko busy na simu!

Serikali inafumbia macho haya malalamiko kwa miaka sasa mingi, wagonjwa wakiendelea kufa kwa uzembe mdogo mdogo.

Hospitali ya Amana, kidude cha IV ilitoka kwenye mkono, damu ilitoka nyingi sana, kitanda kilitapakaa damu mpaka mgongoni, hakuna dokta aliyeona na kujali ila mimi nikiwa mbali niliona na kuwaambia 😭😭😭😭😭 , nilibaki kulia sana, umasikini mbaya sana

Usimpeleke mgonjwa wako huko.
Narudi tena, Usimpeleke mgonjwa wako huko.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom