Hoja binafsi: Vyama vya siasa viwe makini sana kwenye uteuzi wa wagombea wenza katika chaguzi zijazo ama sivyo Katiba imulikwe

Achana na mambo ya mgombea mwenza wewe mataga Katiba mpya itakayoimarisha taasisi ndio kila kitu.
Sawa mkuu ahsante kwa kunipa jina jipya nitafungua ID mpya itaitwa mataga Kama itanipendeza.
 
Nimeandka nimefuta karibu mara 5 kwa hyo mgombea mwenza wa CCM mwaka 2020 alikuwa mzaha au una maana gani?
Ohooo hayo umesema wewe sasa mkuu, ila mimi nimeshauri vyama vipunguze mizaha kwenye kuteua wagombea wenza ili kuepukana na mabalaa yanayoweza kutokea.
 
Mkuu hakuna tunachotaka zaidi ya kupunguza mizaha kwenye kuteua wagombea wenza ukinielewa hapo basi hakuna kesi mkuu
nimeelewa sana ,mlitaka mama samia awe kama magufuli huo ndo ukweli aendeleze uvunjwaji wa sheria nakatiba zanchi ...hapa tupate katiba mpya hata nchi akiwa chizi inaenda sawasawa..tupunguze nguvu ya rais mifumo ifanye kazi ,ukizingua gereza lako
 
Mama Samia ndio Rais wetu wether like it or not,nyie team mwendazake kubalianeni na matokeo, Samia is far better than jiwe Mungu kamleta wakati sahihi kabisa
Kwenye mada yangu sijalinganisha mtu na mtu wala sijataja habari za team hapa na wala sijabisha kuwa mama ndio rais wetu.
Mimi nimezungumzia habari za uteuzi wa wagombea wenza hayo mengine yakwako bidada.
 
nimeelewa sana ,mlitaka mama samia awe kama magufuli huo ndo ukweli aendeleze uvunjwaji wa sheria nakatiba zanchi ...hapa tupate katiba mpya hata nchi akiwa chizi inaenda sawasawa..tupunguze nguvu ya rais mifumo ifanye kazi ,ukizingua gereza lako
Hayo mengine ulio sema mimi sijui mkuu.

Umeongelea mifumo ni kweli kabisa lakini hata tukiwa na mifumo ya aina gani ila Kama bado tuna viongozi wenye tamaa kama fisi bado itakuwa kazi bure tu.
 
Walioko bungeni hawajaliona hili,hadi 2025 wataona madhara yake. Ilitakiwa makamu atawale kipindi cha mpiti madhalani miezi 6, then uchaguzi mkuu ufanyike.
SASHA hakujiandaa kuongoza hii nchi, ameangukiwa na BAHATI YA MTENDE tu. Udhaifu wa Katiba iliyopo utajidhihirisha tu hata kabla ya 2025, ni suala la muda tu.
 
SHASHA hakujiandaa kuongoza hii nchi, ameangukiwa na BAHATI YA MTENDE tu. Udhaifu wa Katiba iliyopo utajidhihirisha tu hata kabla ya 2025, ni suala la muda tu.
Dah jiwe aliyejiandaa tuliona madhara yake
 
Ni kweli; hata mimi nimeshaona tatizo la kikatiba hata. Ile katiba ya zamani ilikuwa inasema rais akifa, basi uchaguzi mwingine unafanyika kujaza nafasi yake kama ambavyo anapokufa mbunge nafasi yake inajazwa kwa uchaguzi mdogo.

Mabadiliko ya kusema makamu wa rais anakuwa automatic na akishachukua madaraka anafanya lolote atakalo ikiwa ni pamoja na kupangua serikali aliyokuta, linaweza kuwa unintended consequences kwa mustkhabali wa nchi.
Uchaguzi mpya ni gharama sana, unachukua muda, na nchi haiwezi kukaa bila rais.

Utaratibu wa makamu wa rais kuchukua urais upo sehemu nyingi, unaondoa gharama za uchaguzi, na unaondoa nchi kusubiri uchaguzi kupata rais mpya.

Huo utaratibu wa kufanya uchaguzi unaweza kuleta mpasuko mkubwa sana na hata vita.

Kwani huyo anayeenda kuchaguliwa tena hawezi kufanywa mgombea mwenza akifa rais yeye akawa rais automatically kama VP?
 
Kwenye mada yangu sijalinganisha mtu na mtu wala sijataja habari za team hapa na wala sijabisha kuwa mama ndio rais wetu.
Mimi nimezungumzia habari za uteuzi wa wagombea wenza hayo mengine yakwako bidada.
Nyie team jiwe mnahangaika Sana kwa huyu mama baada ya mwendazake kuondoka ghafla mumechanganyikiwa na ningekuwa Samia siwahurumii nawafurusha na Kama kawa spare mnakuja huku jf na thread's za hivi ni rahisi kumhujumu ili mpate na kusema
 
nimeelewa sana ,mlitaka mama samia awe kama magufuli huo ndo ukweli aendeleze uvunjwaji wa sheria nakatiba zanchi ...hapa tupate katiba mpya hata nchi akiwa chizi inaenda sawasawa..tupunguze nguvu ya rais mifumo ifanye kazi ,ukizingua gereza lako
Yani wanataka mama awe katili kama mwendazake asiyefata katiba huku akiua uchumi, uwekezaji wao as long as walifaidika naye wako okay kabisa
 
Nyie team jiwe mnahangaika Sana kwa huyu mama baada ya mwendazake kuondoka ghafla mumechanganyikiwa na ningekuwa Samia siwahurumii nawafurusha na Kama kawa spare mnakuja huku jf na thread's za hivi ni rahisi kumhujumu ili mpate na kusema
Aah kumbe ni hivyo haya ahsante kwa kunipa team dada sasa na wewe team ipi sasa hapo?
 
Uchaguzi mpya ni gharama sana, unachukua muda, na nchi haiwezi kukaa bila rais.

Utaratibu wa makamu wa rais kuchukua urais upo sehemu nyingi, unaondoa gharama za uchaguzi, na unaondoa nchi kusubiri uchaguzi kupata rais mpya.

Huo utaratibu wa kufanya uchaguzi unaweza kuleta mpasuko mkubwa sana na hata vita.

Kwani huyo anayeenda kuchaguliwa tena hawezi kufanywa mgombea mwenza akifa rais yeye akawa rais automatically kama VP?
Upo sahihi kabisa mkuu ila hawa wagombea wenza ambao muda wowote wanaweza kuwa wakuu wa nchi inabidi ufanyike mchakato wa nguvu na kwa umakini mkubwa kuwapata na si kujiamulia tu na kuweka mtu yoyote kana kwamba ni nafasi tu ya kishikaji.
Hii inatuletea madhara makubwa Kama taifa pindi zinapotokea dharura jiulize Membe angeshinda urais alafu yengetokea Kama haya yalio tokea (japo hatuombie) inamaana yule mgombea mwenza ndio angukuwa rais wetu leo.

Hili ni kwa vyama vyote, huo ni mfano tu.
 
Sio wagombea wenza tu, kiujumla Watanzania huwa tunaishi kwa mazoea tu.

Hatuangalii sheria na katiba.

Kama huyu rais wa sasa watu waliona hapa tuweke mgombea mwenza mwanamke tuonekane tunajali wanawake.

Hawakuwahi kufikiri kwamba rais atafariki na huyu anaweza kuwa rais muda wowote.
 
Wazeee naona this round mnawashwa washwa sana tatizo liko waapi!!?

Na laazma mnyooke😀😀😀😀😀

Kuchekana ni kwa zamu wazee😀😀
 
Back
Top Bottom