Mbunge ataka Sheria kuweka bayana uteuzi wa Wagombea ndani ya Vyama vya Siasa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Lugangira ametaka maboresho ya vyama vya siasa na chaguzi ziainishe bayana uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Ameyasema hayo leo Aprili 25,2023 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2023/2024.

“Niombe Serikali itakapoleta maboresho hapa bungeni sheria ya vyama vya siasa pamoja na sheria ya uchaguzi ianishe bayana namna ambayo uteuzi ndani ya vyama vya siasa utafanywa,”amesema.

Amesema ingependeza sana kama sheria hiyo itapelekwa bungeni kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwakani.

Amesema sababu ya kupendekeza hayo ni uwepo wa viongozi wachache wanawake wa Serikali za mitaa nchini.

Lugangira ameainisha kuwa viongozi wanawake ambao ni wenyeviti wa vijiji ni asilimia 2.1, wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni asilimia 12.8 wakati asilimia 6.7 ya wenyeviti wa vitongoji ni wanawake.

Amesema ipo haja ya kuongeza idadi hiyo na hivyo ni lazima sheria hizo zije kabla ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa serikali.

Aidha, Lugangira alitaka asasi za kiraia hasa za pembezoni kushirikishwa ipasavyo katika kutoa elimu na mchango wa namna ya kuboresha Katiba.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom