Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,604
Wanabodi,
Sina uhakika sana humu JF, lakini kati ya JF members wanaozungumzia sana, Katiba, Sheria na Haki, mimi ni mmoja wao.
Nimeandika sana kuhusu katiba, sheria na haki toka enzi za JPM. Rais Samia alipoingia, nimeandika sana kuhusu katiba, sheria na haki.
Rais Samia alipounda Kikosi Kazi tulimpongeza.
Alipopokea Ripoti ya Kikosi Kazi, na kuahidi kufanya mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa tulimpongeza.
Mkutano wa Kutoa Mapendekezo kuhusu sheria hizi, mimi ni miongoni mwa tulioalikwa kutoa mawazo yetu, na mimi ni miongoni mwa tulibahatika kuchangia.
Mchango wangu ni huu
View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=GjujW1--LkjxAKOf
Na kwa faida ya wale ambao bundle ni issue naomba niwa paraphrasie
Utangulizi
Naomba nijitambulishe rasmi, mimi ni mwandishi wa habari mkongwe, nimeripoti toka mwaka 1994, ule uchaguzi wa Jimbo la Kwahani, Zanzibar ambao ndio ulikuwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, na uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 nimeendesha kipindi cha kwanza cha talk show kwenye TV za Tanzania, kipindi cha Mada Moto ile 1995 na baadae kipindi cha Kiti Moto.
Ni mimi ndiye niliyetangaza yale matokeo halali ya uchaguzi wa Zanzibar mwaka 1995, naomba tusirudie kilichotokea. Kwa sasa licha ya kuwa ni mwandishi wa habari, pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea.
1. Kwanza, kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri, naomba kutoa shukrani za dhati kwa Msajili wa vyama, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi, kwa kutushirikisha media na kutu engage the media kupitia Jukwaa la Wahariri na kutufanya ni wadau muhimu kwenye huu mchakato.
Vyombo vya habari ni mhimili, ni mhimili wa nne usio rasmi ambao unaunganisha ile mihimili rasmi mitatu na wananchi.
Ukiwa na jambo, haliwezi kufika kule chini kwa wananchi, bila kupitia kwetu sisi waandishi wa habari na kama kuna jambo huku chini, ni kupitia kwetu sisi waandishi wa habari, linawafikia huko juu.
Ombi: Naomba Media zetu zote za public na private, zime engaged na kuwezeshwa kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu.
2. Naomba kumpongeza Rais Samia kuunda kikosi kazi na kumpongeza kutaka wananchi wafundishwe kuhusu katiba yao, naomba kuongezea sio wananchi tuu wafundishwe kuhusu katiba, bali vyama vya siasa vifundishwe kuhusu katiba, serikali ifundishwe kuhusu katiba, Bunge lifundishwe kuhusu katiba, Mahakama ifundishwe kuhusu Katiba, katiba ndio kila kitu.
Tatu, mwisho Ibara ya 5 ya katiba ya JMT, imetoa haki kwa kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18, kupiga kura kuchagua viongozi anaowataka, na ibara ya 21, inatoa haki kwa kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 21, kuwa huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu bila masherti yoyote kandamizi. Hivyo ndivyo katiba ya JMT ya mwaka 1977 inavyosema, na hiyo ndio dhima ya mtunga katiba.
Kukatokea mambo fulani hapa katikati, ikatungwa sheria ya uchaguzi yenye kipengele batili, kikaweka shurti batili, ili Mtanzania aweze kugombea, shurti ajiunge na chama cha siasa, na adhaminiwe na chama cha siasa!. Hili ni shurti batili linalokwenda kinyume cha katiba ya JMT, na shurti hili batili, limechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, Mahakama Kuu ya Tanzania iliishatangaza, ilikuwa Bunge liuondoe ubatili huu, sijui ni kwa nini huu ubatili uko ndani ya katiba yetu mpaka sasa?
Naomba ndugu Mwenyekiti, pendekezo hili liingizwe, lile shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa kumlazimisha Mtanzania ili kugombea, liondolewe, ni shurti batili kinyume cha katiba, ili kila Mtanzania awe huru kugombea.
Kwa hiyo, naomba sasa, Ili Uchaguzi wa 2025 uwe wa haki, na Mama Samia ameisha onyesha kwa dhamira ya dhati, kwa kauli na matendo, anataka Watanzania watendewe haki, ili kila Mtanzania mwenye nia ya kugombea, awe huru kugombea, kuna viongozi wazuri wanataka kuwatumikia Watanzania, lakini wanawekewa kauzibe ndani ya vyama vyao, kwasababu wanaonekana "sio wenzetu".
Paskali