Maoni ya Jumla ya Wadau Kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Vyama vya Siasa - Sehemu 1

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
JamiiForums, Jukwaa la Katiba (JUKATA), Tanganyika Law Society (TLS), Twaweza East Africa, Centre for Strategic Litigation (CSL) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa pamoja tunawasilisha maoni kwenye miswada minne: Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani; Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi; na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi.

Serikali iliwasilisha miswada hii Bungeni na ilisomwa kwa mara ya kwanza tarehe 10 November, 2023. Kisha Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba imealika wadau kutoa maoni kwenye miswada hiyo kuanzia Januari 6-10, 2024.

Hii ni fursa muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia nchini kwetu na kulinda haki muhimu za raia. Tunatambua pia awamu hii miswada hii haikuwasilishwa Bungeni kwa hati ya dharura na hivyo imeongeza muda kwa wadau kuweza kuichambua na kuwasilisha maoni. Kamati ya Bunge imefanya vyema pia kupokea maoni kwa siku kadhaa na kwa njia mbalimbali ili kuwezesha wadau wengi zaidi kuwasilisha maoni yao.

Kwa kuitikia wito huu na katika kutekeleza wajibu wetu wa kikatiba, tunafarijika kuwasilisha maoni yetu ili kuchangia katika kuboresha muktadha wa kisheria utakaowezesha kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania. Tunaamini haki na demokrasia ni misingi muhimu sana ya kuwezesha ushiriki wa watanzania wote katika kufikia malengo ya maendeleo.

Katika kila muswada, tunawasilisha maoni ya jumla na maoni mahsusi kifungu kwa kifungu. Maoni ya jumla yanatoa muhtasari wa mambo ya msingi katika kila muswada na maoni mahsusi yanatoa ufafanuzi wa kina wa mapungufu na maboresho katika vifungu vingi.

Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanya jambo zuri la kuunganisha sheria mbili za awali na kutengeneza sheria mama ya maswala ya uchaguzi. Hili ni jambo zuri ili kurahisisha rejea ya kisheria. Maoni yetu yamelenga kuboresha utaratibu mzima wa uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi zetu ni huru, za haki na za uadilifu. Tunapokuwa na chaguzi huru na za haki inaepusha uvunjifu wa amani na hivyo kuimarisha demokrasia yetu.

Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa unapendekeza mabadiliko kadhaa kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019. Pamoja na mambo chanya kadhaa ikiwemo kutoa ufafanuzi wa kuboresha maswala ya ujumuishi wa makundi maalum ndani ya vyama, muswada huu hauna mabadiliko makubwa sana katika sheria iliyopo. Na baadhi ya vifungu pendekezwa vinahitaji maboresho kama ambavyo tumebainisha katika uchambuzi wetu ili kuviwezesha vyama vya siasa kutekeleza majukumu yao ya kisiasa bila kukiuka katiba ya nchi yetu na sheria nyinginezo. .

Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi unalenga kuhamasisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika maswala ya fedha kwa wadau wote wa uchaguzi. Hili ni jambo zuri katika kujenga demokrasia imara yenye uwazi na uwajibikaji wa wadau wote.

Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi unapendekeza kuanzishwa kwa sheria inayojitegemea kuhusu Tume ya Uchaguzi. Sheria hii itatoa ufafanuzi wa kina kuhusu Tume ya Uchaguzi tofauti na ilivyo sasa ambapo Tume imetajwa kikatiba lakinin maelezo yake yamekuwa sehemu tu ya Sheria za Uchaguzi. Maoni yetu yamekusudia kuboresha muundo wa Tume na kuifanya iwe tume huru isiyoingiliwa na mamlaka yoyote katika utekelezaji wa shughuli zake.

Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani
Muswada huu unaunganisha sheria mbili za uachaguzi. Muswada hauna tofauti sana kimaudhui na sheria zilizokuwepo awali isipokuwa baadhi ya mambo mapya yamependekezwa ikiwemo kuiwezesha Tume ya Uchaguzi kukataa jina la mgombea wa chama kwa nafasi tajwa kwa kutumia sababu ambazo zimebainishwa katika muswada huu (Vifungu 36-37).

Uchambuzi wetu umezingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, mapendekezo ya ripoti mbalimbali hasa ripoti za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, maamuzi ya mahakama za ndani na za kikanda pamoja na uzoefu na mifano kutoka nchi nyingine.

Kiujumla, muswada huu unamambo mbalimbali mazuri ikiwemo kuunganisha sheria mbili ambazo ni Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 1979 kuwa sheria moja.

Maoni ya Jumla

Tunapendekeza…

1.
Jina la sheria ijulikane kama Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambayo itasimamia chaguzi zote na mambo yote yanayohusu uchaguzi nchini.[Kifungu cha 1]

2.
Tunapendekeza vifaa vya uchaguzi na miundombinu vizingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu.[Kifungu kipya]

3.
Tume ibanishe siku mahususi ya uchaguzi “election day” mathalani Jumatano ya Mwisho ya mwezi Oktoba kuwa siku ya uchaguzi.[Kifungu cha 41]

4.
Tume iwe na mamlaka ya kuajiri watumishi wake kwenye ngazi zote.[Kifungu kipya]

5.
Watu waruhusiwe kupiga kura kwa vitambulisho mbadala vinavyotambulika kisheria. [Kifungu cha 14]

6.
Matumizi ya teknolojia yatumike kufanya utambuzi wa wapiga kura kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia “fingerprint.” [Kifungu 166]

7.
Fomu ya uteuzi wa mgombea wa ubunge na udiwani umezingatia mahitaji maalum tofauti na fomu ya uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais ambayo haijaweka sharti la fomu hiyo kuzingatia mahitaji maalum. [Kifungu cha 34]

8.
Popote kwenye neno “chini ya sheria hii” pafutwe na pasomeke “kwa mujibu wa sheria hii”.

9. Popote kwenye neno “tarehe iliyochaguliwa” pafutwe na pasomeke “tarehe iliyopangwa”.

10. Endapo mpaka siku ya mwisho ya uteuzi hapatakuwa na mgombea au mgombea kajitoa ndani ya saa 24 baada ya muda wa uteuzi kuisha, chama husika kipewe nafasi ya kuteua mgombea mwingine. [Kifungu cha 70 (3)]

11.
Kuweka kifungu kitakachoweka wajibu kwa vyombo vya habari vya umma kutokuwa na upendeleo kwa kuwapa fursa sawa wagombea kujinadi. Aidha vyombo vya habari binafsi kuweka muda maalum kwa ajili ya wagombea wote wakati wa kampeni. [Kifungu cha 74]

12.
Usikilizwaji wa mashauri ya uchaguzi ukamilike ndani ya siku 90 badala ya miezi 12 kama inavyopendekezwa katika mswada huu. [Kifungu 144 (2)] Na rufaa zikamilike ndani ya siku 60 badala ya miezi 12 kama inavyopendekezwa kwenye muswada huu.

13. Kuwekwa takwa la lazima la uwepo wa midahalo kwa ngazi ya urais mdahalo urushwe mubashara kwenye vyombo vya habari na kwa ngazi ya ubunge na kata midahalo ifanyike katika ngazi husika. [Kifungu kipya]

14.
Uwepo wa kifungu kinachoainisha ukomo wa muda wa kutangaza matokeo ya urais, ubunge na madiwani.[Kifungu cha 45, 105, 106]

15.
Mtiririko wa vifungu vya muswada huu ufuate mzunguko wa kiuchaguzi “Election Cycle” ili kuleta mantiki na kurahisisha usomaji, yaani uandikishaji, elimu ya mpiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeni, upigaji kura, matokeo na mashauri ya uchaguzi.

16. Kuondoa kifungu kanachoweka takwa la kutaifisha dhamana ya mgombea ikiwa hatopata moja ya kumi ya kura zote zilizohesabiwa.[Kifungu cha 51(1)]

17. Mshindi wa nafasi ya urais, ubunge na madiwani wapatikane kwa kura nyingi zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.

18. Kuwe na sura maalum kuhusu “Elimu ya Mpiga Kura na Watazamaji wa Uchaguzi”.

19. Uwasilishwaji wa fomu za uteuzi wa wagombea katika ngazi zote ziwasilishwe kwa njia ya nakala ngumu au tepe. [Kifungu cha 34(2),50(7), 62(7)]

20.
Kuondoa kifungu cha 107 (3) kinachopendekeza kuteketeza nyaraka za uchaguzi ndani ya miezi 6 inakinzana na muda wa mashauri ya uchaguzi na Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Taifa ya Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Namba 3, 3002 (The Records and Archives Management Act No.2 of 2002) ambayo inaweka takwa la nyaraka za Taifa kutunzwa ndani ya miaka 30.

21. Nyaraka za uchaguzi zitunzwe kielektroniki.

22. Kurekebisha Kifungu cha 102(1)(e) kirekebishwe kuondoa maneno “iwapo fomu za taarifa za matokeo zipo za kutosha”.

Pia soma: Maoni ya Wadau Kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Vyama vya Siasa - Sehemu 2
 
Maoni ya Jumla

  • Tunapendekeza…
  • Jina la sheria ijulikane kama Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambayo itasimamia chaguzi zote na mambo yote yanayohusu uchaguzi nchini.[Kifungu cha 1]
  • Tunapendekeza vifaa vya uchaguzi na miundombinu vizingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu.[Kifungu kipya]
  • Tume ibanishe siku mahususi ya uchaguzi “election day” mathalani Jumatano ya Mwisho ya mwezi Oktoba kuwa
Sawa ni maoni mazuri ya marekebisho, BUT......THESE ARE PEETTY AND COSMETIC ISSUES........... Kuna vitu vya msingi kuliko hayo ya IS/WAS.
 
MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS 2020 HAYAPO KATIKA GAZETI LA SERIKALI KWA SABABU UCHAGUZI ULIVURUGWA?

Kutokana na uchaguzi wa 2020 kuporwa, wameshindwa kuoanisha matokeo ya urais ili yatangazwe katika gazeti la serikali (gazetted). Watu wangestuka na kuona tofauti kubwa ya jumla ya kura za wabunge wote na zile za urais.


Maana kama wangekusanya matokeo ya urais kutoka kila jimbo na kuyajumuisha ni aibu tupu, jumla ya kura ya urais ingetofautiana sana kwa umbali mkubwa na jumla ya kura za walizopata wabunge wote.

N.B
More info :

UCHAGUZI MKUU WA 2020
Aidha, siku ya kupiga kura jumla ya wapiga kura 15,091,950 sawa na asilimia 50.72 walijitokeza kupiga kura kati ya wapiga kura 29,754,699 walioandikishwa. Kura halali zilikuwa 14,830,195 sawa na asilimia 98.27 ya kura zote zilizopigwa na kura zilizokataliwa
zilikuwa 261,755 sawa na asilimia 1.73 ya kura zote zilizopigwa.
Mheshimiwa Rais,
Kwa ujumla, Tume iliendesha uchaguzi mkuu katika hali ya amani na utulivu. Mafanikio
hayo yalitokana na maandalizi yaliyofanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Tume pia ilipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali wa uchaguzi.
Mheshimiwa Rais,
Baada ya uchaguzi mkuu kukamilika, Tume imeandaa taarifa inayoelezea namna mchakato wa uchaguzi ulivyofanyika.
Kwa heshima na taadhima, Tume inaomba kuwasilisha kwako Taarifa ya Uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2020.
xv
…………………………………………
Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles S. Kaijage
Mwenyekiti
…………………………..………….
Jaji (Mst.) Mary H. C. S. Longway
Mjumbe
........................................
Asina A. Omari
Mjumbe
…………………………..………….
Jaji (Mst.) Thomas B. Mihayo
Mjumbe
…………………………..………….
Dkt. Wilson Mahera Charles
Mkurugenzi wa Uchaguzi


View: https://m.youtube.com/watch?v=e3Grxxco7hQ

Hivyo ni muhimu uchaguzi wa rais kuhojiwa mahakama kuu, na kuwepo takwa la lazima kuoanisha kura za ujumla za wabunge na urais ili uoanishi huu kuwa njia (tool) mojawapo ya kuibana Tume Huru ya Uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi kufanya kazi yao sawa sawa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi
https://www.nec.go.tz › publications
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu

Matokeo ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa mwaka 2020 Pakua · Wabunge Wanawake Walioteuliwa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu ....

Tume ya Taifa ya Uchaguzi
https://www.nec.go.tz › 1630...PDF
TAARIFA YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI ...

1704794279401.png
Haki zote zimehifadhiwa, hairuhusiwi kuiga, kunakili au kutoa kitabu hiki kwa njia
 
12 April 2024
BBC SWAHILI

Demokrasia Tanzania: Tume huru ya uchaguzi au wajumbe, utendaji huru?​

Maafisa wa Tume ya uchaguzi

Maelezo kuhusu taarifa
  • Author,Na Ezekiel Kamwaga
  • Nafasi,Mchambuzi, Tanzania
  • 12 Aprili 2024
Katika mchezo maarufu wa kuigiza wa Romeo and Juliet ulioandikwa na William Shakespeare mnamo mwaka 1597, kuna sehemu Juliet alitamka maneno maarufu ya “What is in a name?”. Kufupisha hadithi ndefu, Juliet alisema waridi litabaki kunukia tu hata kama lingeitwa kwa jina lingine.

Baada ya Serikali ya Tanzania kutangaza kwamba kuanzia leo, Aprili 12, 2024, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) itaanza kujulikana kwa jina jipya la Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania, maoni ya wanasiasa wa vyama vya upinzani na wadau wengine yalinikumbusha mchezo ule wa kuigiza wa Shakespeare uliotungwa mwishoni mwa karne ya 16.

Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa viongozi wake wa juu wametoa matamshi hadharani ya kusema jambo la msingi kabisa si kubadili jina la tume hiyo bali kufuata matakwa ya sheria mpya ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 2024 iliyobadili jina la tume.


Chama kikuu cha upinzani na maarufu zaidi nchini Tanzania cha CHADEMA, kupitia kwa Katibu Mkuu wake, John Mnyika, kimeendelea na msimamo wake wa kutokubaliana na kuundwa kwa tume hiyo pasipo kwanza kufanya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.


Ni kama vile CHADEMA na ACT Wazalendo wanakubaliana na Shakespeare kwamba jina pekee la tume ya uchaguzi halifanyi tume hiyo kutimiza majukumu yake ipasavyo. Tume inaweza kuitwa huru na isiwe huru na inaweza isiitwe huru lakini ikawa huru.


Ingawa kwenye hilo ACT na CHADEMA wanakubaliana, lakini vyama hivyo na chama tawala cha CCM vinaonekana haviko njia moja kwenye suala zima la sheria tatu mpya za uchaguzi zilizosainiwa na Rais Samia Suluhu Hassan Machi 29.


Sheria hizo ni Sheria ya Uchaguzi wa Wabunge na Madiwani, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Tume ya Uchaguzi – zote za mwaka 2024.

CCM, ACT na CHADEMA katika hali tofauti​

Tangu kuanza kwa mjadala na hatimaye kupitishwa kwa sheria hizo tatu, ni rahisi kuona njia tatu ambazo vyama vikuu vya siasa vya Tanzania vinaona mchakato huo. Kwa chama tawala, ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana pekee ndiye amezungumza hadharani kuunga mkono sheria hizo.


Kimsingi, baadhi ya waandishi wa habari wa Tanzania wamejikuta katika hali ngumu kupata maoni ya baadhi ya wabunge na wanasiasa wa chama tawala kuhusu maoni yao kuhusu sheria hizo. Ni kama vile wapo wanaoamini sheria hizo hazina faida kwao kama chama tawala.


ACT Wazalendo wanaonekana kuunga mkono sheria hizio mpya kwa sababu wao – pengine kuliko chama kingine chochote cha upinzani nchini, wameshiriki kuanzia hatua ya kwanza ya kutaka kufanyiwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kwenye Kikosi Kazi cha Rais Samia.


Mafanikio ya aina yoyote kwenye mabadiliko ya ufanyikaji na uendeshaji wa siasa Tanzania kupitia mchakato uliofanyika – kwa namna zote, yanaonekana kama ni mafanikio kwa ACT Wazalendo.


Kwa upande mwingine, CHADEMA haikuwa sehemu na haikuunga mkono mchakato uliofanikisha kupitishwa kwa sheria hizi. Tangu awali, msimamo wake ni kuwa kinachotakiwa ni mabadiliko ya Katiba ya Tanzania na si sheria zinazosimamia uchaguzi pekee.


Kwa CHADEMA – kuondoa ukweli wa madai yao ya Katiba, inatambua pia kwamba mafanikio ya mchakato uliofanikisha sheria hizi, yanakipa nguvu chama cha ACT Wazalendo na ushawishi wake na kwa sababu hiyo ni muhimu kwake kuendelea kupinga mchakato wenyewe na matokeo yake.

Kuhusu uhuru wa tume za uchaguzi​

H

Kila ninapofanya uchambuzi kuhusu uhuru au uhalali wa Tume za Uchaguzi barani Afrika, kigezo changu kikubwa huwa ni andiko maarufu la kisomi la mwaka 2020 la maprofesa wawili; Nic Cheeseman na Jorgen Elklit – Understanding and Assessing Electoral Commission Independence: A New Framework. (Uelewa na tahmini ya uhuru wa tume ya uchaguzi: Mwelekeo mpya) Wasomi hawa walitoa vigezo vitatu vya kueleza endapo tume ni huru au si huru.


Vigezo hivyo ni; Utaasisi wa tume, namna inavyofanya kazi zake na uwezo wake kibajeti. Kwenye eneo la utaasisi wa tume inazungumzia ilivyoundwa kisheria, aina ya watu wanaoiongoza na weledi wao. Kwa vigezo vya akina Cheeseman, tume haiwezi kuwa huru kwa kubadilishwa jina pekee. Uhuru ni utaasisi wake, weledi wa watumishi na wajumbe wake na kuaminika kwake mbele ya jamii.


Inafikirisha kwamba katika andiko hilo la maprofesa hawa – mmoja wa demokrasia na mwingine wa sayansi ya siasa, kuna mahali wameandika kwamba tume nyingi za uchaguzi zinazoitwa huru, kiukweli hazina uhuru isipokuwa ni jina tu.


Hoja kuu ya Kiongozi wa Chama wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ni kuwa ingawa tume sasa itaitwa huru, wajumbe wake ni walewale wa zamani na hivyo wanatakiwa kuchaguliwa wengine watakaoendana na “roho” ya sheria mpya.


Kwa mujibu wa sheria mpya, wajumbe wapya wanatakiwa kuomba nafasi hiyo na kupitishwa na Tume ya Usaili. Wajumbe wote waliopo sasa walipata nafasi hizo kwa uteuzi wa Rais wa Tanzania kwa mujibu wa matakwa ya sheria iliyokuwepo awali.

Muktadha wa tume za uchaguzi za Afrika​

Kufananisha uhuru na utendaji wa tume za uchaguzi za Afrika ni jambo lenye changamoto. Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya ilikuja baada ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2010. Hata hivyo, utafiti wa akina Cheeseman ulionesha nayo haikuwa “huru” kama neno lenyewe lilivyo.


Tume ya Uchaguzi ya Afrika Kusini ni miongoni mwa zinazosifiwa barani Afrika lakini nayo ujio wake ulifuata mabadiliko ya Katiba. Tume za uchaguzi za Senegal na Malawi haziitwi huru kwenye majina yake lakini zimefanikisha kufanyika kwa uchaguzi ulio huru kwenye nchi zao ambapo wagombea wa upinzani walishinda pasipo mabadiliko ya Katiba.


Tanzania ni nchi tofauti na hizo mbili lakini inaweza kufuata njia zao. Ni nchi inayofanya uchaguzi na kupitisha sheria zake bungeni kama misingi ya kidemokrasia inavyotaka. Lakini bado inaitwa ya demokrasia-nusu kwa sababu inaonekana bado chama tawala kinapata upendeleo maalumu kwenye uchaguzi.


Nchini Senegal, siri ya tume yao ni kuwa na wajumbe wanaofahamika kwa maadili na wasiohusishwa na vyama vya siasa. Siri ya Malawi ni kuwa na mahakama na jeshi la nchi vyenye weledi na uzalendo kwa nchi na katiba yao.


Katika muktadha wa Afrika, suala la nani wanaongoza tume ya uchaguzi na taasisi za haki ni la muhimu kwa taswira ya uhuru wa tume kuliko jina lenyewe.
Kama serikali ya Rais Samia imedhamiria kuleta siasa za tofauti kwa kuanza na tume huru na inayoaminika, ni muhimu kwanza ikamaliza suala hili kwa kuwa na wajumbe wa tume wanaokubalika na wadau wa siasa na wanaoendana na matakwa ya sheria mpya.


Jina la tume ni muhimu, lakini wanaounda tume na utendaji wao katika misingi ya haki pasi na uependeleo ni muhimu zaidi.
Katika mazungumzo yangu na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile, aliniambia changamoto kubwa iliyopo ni kuwa wajumbe na watumishi waliopo sasa wana mikataba halali kisheria na hawawezi kuondolewa tu kwa sababu ya kuundwa sheria mpya na kwamba ni lazima kuwepo na utaratibu wa namna ya kuwabadili.


Lakini Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, anaamini kama serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha uchaguzi unasimamiwa na tume huru, inaweza kuweka utaratibu wa kuondoa wajumbe waliopo sasa na kupata wajumbe wapya haraka. Hili, kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, ni suala la dhamira na nia njema kwa upande wa chama tawala.


Hata hivyo, dhamira na nia njema hiyo ya chama tawala inategemea kwa kiwango kikubwa tathmni ya ndani ya chama hicho kuhusu mustakabali wake katika uchaguzi ulio karibu wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025. Kwamba CCM itatekeleza dhamira yake hata kama inahatarisha kupungua kwa kura na viti vyake vya uwakilishi, achilia mbali kushindwa uchaguzi hilo ni suala la kulingojea kwa hamu kulishuhudia.

Toka maktaba :

TUME HURU YA UCHAGUZI NI KAA LA MOTO TANGU 2020​


1713272523799.png
 
17 April 2024

JUKWAA LA SAUTI YA WATANZANIA, MJADALA MPANA KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI

LIVE : TUNDU LISSU ANAONGEA KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI, TEUZI ZA,WAJUMBE WA TUME HURU YA UCHAGUZI N.K NA JINSI RAIS ALIVYO NA MAMLAKA YA KUTEGUA


Sheria mpya za uchaguzi ya Tume Huru ya Uchaguzi athari zake kwa uchaguzi mkuu 2025 na ule wa serikali za mitaa pia vijiji mheshimiwa Tundu Lissu anaongezea kwa kina mazungumzo yake ya awali aliyofanya wiki iliyopita ktk kituo cha radio cha Clouds FM.

Leo mheshimiwa Tundu Lissu anajikita kwa kina zaidi kuhusu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi jina lake tu lina mushkeli mkubwa na inakinzana na Katiba hivyo ni batili .......

katiba ambayo ni sheria mama haitambui Tume Huru ya Taifa Uchaguzi inapingana na jina la Tume ya Uchaguzi hilo ni la kwanza ... hivyo msidanganywe

Jina la Tume ya Uchaguzi ilianza kutumika 1961 (tanganyika constitution order in Council 1961) kufuatia amri ya Malkia au Mfalme wa Uingereza kupitia Privy Council ....

Katiba ya Jamhuri 1962 ikalirithi jina Tume ya Uchaguzi na mwaka 1965 Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1965 na iliendelea hadi 1977 Tume ya Uchaguzi na hadi leo 2024 jina halijabadilika ......

Tundu Lissu anageukia sasa kuchambua ..... Tume Ya Uchaguzi na kinga ya kushitakiwa ni kuwa ..... haitafuata maelekezo au amri ya mtu yeyote. Tume ya Warioba olisema hiyo siyo kweli kwa Tume ya Uchaguzi ni ya Rais na inateuliwa na kutenguliwa na Rais hivyo Tume ya Uchaguzi hupokea amri na maelekezo kutoka kwa mwenye Tume ya Uchaguzi ambaye ni Rais ... juzuu ya Tume ya Warioba imesisitiza hivyo Tume ya Uchaguzi haina uhuru katika uwajibikaji ...


Uundwaji wa majimbo ya uchaguzi Tanzania ni tofauti na nchi zingine, maana Tanzania majimbo yanaibuliwa huku kukiwa na nia ya kushinda uchaguzi ..... na mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu mipaka na majimbo mapya yapo chini ya rais

Rais ndiye anayeitengeneza Tume ya Uchaguzi na kuondoa wajumbe wa Tume. Rais ndiyo anaye toa na kutwaa haya madaraka ni absolute power hivyo Tume hii ni ya Rais pekee...
 
Back
Top Bottom