Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Nauliza hili swali sababu kama wananchi tunataka kufahamu ukweli juu ya hili janga. Tunataka waziri wa afya, au msemaji mkuu wa serikali kila siku awe anatoa taarifa zilizo rasmi.

Mbona nchi za wenzetu ambazo zimekumbwa na hili janga kila siku lazima watoe taarifa rasmi kuhusu maambukizi,waliopona na waliofariki.

Au hapa Tanzania ndio kusema mambo yanaenda kimya kimya? Maana watu kila kukicha ni kutishwa tu na habari ambazo sio rasmi.

Mara tunasikia watu wanazikwa usiku, mara tunasikia rubani wa Tanapa alikufa kwa Covid-19,mara kuna maiti imekaa siku mbili mtaa wa Lumumba. Lakini hatusikii serikali ikikanusha wala kuwaambia ukweli wananchi.

Kwa jinsi hili janga lilivyo serious ilipaswa waziri wa afya au msemaji wa serikali angekuwa kila siku anakaa na wanahabari na kutoa takwimu na taarifa rasmi.

Lakini mtu mmoja ambae anamiliki jarida la mtandaoni (Pambazuka) anapoachiwa awe anaandika habari za uongo kuwa watu wanazikwa usiku kimya kimya ni jambo baya maana watu hofu inazidi kwa wananchi.

Inatoka habari kuwa madereva wanne watanzania wamepimwa huko Uganda na kukutwa na ugonjwa wa Covid-19. Hofu inazidi kuwa kubwa kwa wananchi.
Hivyo ili kuondoa hofu lazima mtupatie taarifa rasmi,kama nchi tupo wapi?

Maambukizi ni mengi? Yamepungua? Na wanaopona ni kiasi gani? Hii iwe kila siku na mruhusu kupigwa maswali na waandishi wa habari kama Andrew Cuomo gavana wa New York anavyofanya kila siku. Maana hatulali ni hofu tu.
 
Nchi iliyozoea kupika data utaijua tu. Sasa data za korona hazipikiki kirahisi ni lazima watafute wapishi wazuri ndio wazipike na wakisha pika ndio unasomewa.

Ukiona umesomewa watu 50 basi wewe ongeza wengine 40 ili upate data kamili ambayo haija pikwa.

BTW mzee yuko chattle bado?
 
Ndiyo bado yuko chattle, ila makamu wake ndo hatujui yuko wapi
Nchi iliyo zoea kupika data utaijua tu. Sasa data za korona hazipikiki kirahisi ni lazima watafute wapishi wazuri ndio wazipike na wakisha pika ndio unasomewa.

Ukiona umesomewa watu 50 basi wewe ongeza wengine 40 ili upate data kamili ambayo haija pikwa.

BTW mzee yuko chattle bado?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi iliyozoea kupika data utaijua tu. Sasa data za korona hazipikiki kirahisi ni lazima watafute wapishi wazuri ndio wazipike na wakisha pika ndio unasomewa.

Ukiona umesomewa watu 50 basi wewe ongeza wengine 40 ili upate data kamili ambayo haija pikwa.

BTW mzee yuko chattle bado?
Hilo la kama bado yupo Chato mpigie simu umuulize. Hoja kuu hapa ni kupata official information kwa manufaa ya taifa.
 
Toka Mkuu wa Kaya atoe ile hotuba yake kule kijijini, naona upepo wa kutoa taarifa umebadilika kabisa! Watoa taarifa sijui wameingiwa na hofu ya kutumbuliwa!!

Mola atuepushe na hili janga kwa kweli huku na sisi tukiendelea kuchukua tahadhari kila wakati.
 
Nauliza hili swali sababu kama wananchi tunataka kufahamu ukweli juu ya hili janga. Tunataka waziri wa afya, au msemaji mkuu wa serikali kila siku awe anatoa taarifa zilizo rasmi.

Mbona nchi za wenzetu ambazo zimekumbwa na hili janga kila siku lazima watoe taarifa rasmi kuhusu maambukizi,waliopona na waliofariki.

Au hapa Tanzania ndio kusema mambo yanaenda kimya kimya? Maana watu kila kukicha ni kutishwa tu na habari ambazo sio rasmi.

Mara tunasikia watu wanazikwa usiku, mara tunasikia rubani wa Tanapa alikufa kwa Covid-19,mara kuna maiti imekaa siku mbili mtaa wa Lumumba. Lakini hatusikii serikali ikikanusha wala kuwaambia ukweli wananchi.

Kwa jinsi hili janga lilivyo serious ilipaswa waziri wa afya au msemaji wa serikali angekuwa kila siku anakaa na wanahabari na kutoa takwimu na taarifa rasmi.

Lakini mtu mmoja ambae anamiliki jarida la mtandaoni (Pambazuka) anapoachiwa awe anaandika habari za uongo kuwa watu wanazikwa usiku kimya kimya ni jambo baya maana watu hofu inazidi kwa wananchi.

Inatoka habari kuwa madereva wanne watanzania wamepimwa huko Uganda na kukutwa na ugonjwa wa Covid-19. Hofu inazidi kuwa kubwa kwa wananchi.
Hivyo ili kuondoa hofu lazima mtupatie taarifa rasmi,kama nchi tupo wapi?

Maambukizi ni mengi? Yamepungua? Na wanaopona ni kiasi gani? Hii iwe kila siku na mruhusu kupigwa maswali na waandishi wa habari kama Andrew Cuomo gavana wa New York anavyofanya kila siku. Maana hatulali ni hofu tu.
Jibu kwa title ni SIO kila mtu alifanya basi iwe STANDARD.
 
Back
Top Bottom