Hivi ina maana wachawi hawapo kabisa JF?

Hivi ina maana wachawi hawapo kabisa JF?

Sasa mkuu utajuaje kama umerogwa au haujarogwa? Kwani unajua kurogwa kunakuwaje? Mi naona una mtazamo usio sahihi kuhusu uchawi.

Unategemea utoke mapembe mkuu ndio ujue umerogwa au ama vp maana kinyume na hapo sidhani kama utakubali kuwa ni uchawi na umerogwa.
Blah blah blah! Uchawi haupo.
 
🤣🤣Walitaka wakupuru mkuu,sema nawe unanguvu za mababu aisee...walishindwa
Niliaga kwa tambiko zito kwenye makaburi ya watu wa kale. Nikisikia hizo purukushani nakula mjani wa manabii kwanza halafu natoka nje kucheki usalama
 
Uchawi ni nini?

Uchawi ni kuwa na nia mbaya, wivu, unafiki, kumnyima mwenzako kwa makusudi, au kumtakia mabaya mwenzako.

Kwa ujumla; wote humu ni wachawi kwa namna moja ama nyingine.​
 
Ndio eleza sasa inakuje? Mfano mie ninataka kumtia uchizi mgombea mwenzangu kwenye uchaguzi ili nibaki mwenyewe bila mpinzani, naenda kwa mganga ili nimroge huyo mpinzani awe chizi je nini mganga hufanya kuniaminisha kuwa kweli huyo mpinzani wangu kawa chizi?
Tunapishana sehemu moja Tu,Mimi siamini katika uchawi,Yale ni maigizo!!
Kipindi nasoma kuna jamaa WA mazingaombwe walikua wanakuja shule,wanachukua makaratasi wanageuza yanakuwa hela🤓🤓🤓 wanafanya live bila chenga unaona kabisa,unataka kuniambia walikua na uwezo huo????
Mambo ya flani kamroga flani mi siamini mtu kama kawa Chizi atafutwe mwana saikolojia amsaidie au aende mirembe!!
 
Haujanijibu swali lakini mkuu, eleza sasa waganga huwa wanafanyaje ili kumuaminisha mteja mwenye kutaka kumroga mtu ili awe chizi au kumuuwa kabisa? Kwa sababu katika mambo ambayo hufanya watu kwenda kwa waganga ni pamoja na kumroga mtu mwengine, sasa mganga akiletewa kesi kama hiyo huwa anatapeli vp na mteja akaamini?
Umeona wapi mganga akimroga mtu kuwa chizi au akamuua? Thibitisha
 
Back
Top Bottom