Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Mkuu Mkandara nashangaa, na ndiyo maana nimesema hapo mwanzo, wanatudharau. Maana TeamLowasa wanajua jamaa yao ni mgonjwa, halafu kuna watu tunanunuliwa kuja kumpokea kwa bashasha kama mgombea pendwa wa chama.
respect wa boda sina dhamira ya kuendelea kubishana na wewe, maana hujaelewa, ama hutaki au umezingwa na hisia za mapenzi kwa mgombea wako, kuwa, kupima inawezekana kwa wagombea/watia nia wote, lakini kutangaza ni ngumu kwani "ethics" za kitabibu haziruhusu siri ya daktari na mgonjwa wake kutangazwa na daktari bali mgonjwa mwenye au mwakilishi wa mgonjwa kwa ridhaa ya mgonjwa.

nyinyi mlokubali kununuliwa na kuaminishwa upuuzi endeleeni kuamini Lowasa yuko fit; wenye kuona mbali twasema yu hoi bin taaban. Hata video aliyoweka FaizaFoxy hapo juu inaoneka hujaangalia kwa upofu wa hisia juu ya jamaa yenu.

Hongereni...
Mkuu wala usiwalalamikie hawa ni madalali na Makuhadi kazi yao ni kukushawishi wewe umchague EL sio kwamba wao wanampenda sana bali wameahidiwa pepo kama Boko Haram vile. Kwa hiyo kazi ipo kwetu sisi wapiga kura tumehadaika kiasi gani na nachoogopa ni hii kuishi kwa mazoea - Ombaomba!.

Hawa jamaa wanaulamba mkono hadi mabaki na harufu ya pilau hilo iishe, kesho EL hatakuwa naye maana kazi walotakiwa kuifanya wameifanya. All what matters ni kiasi gani wewe, mimi pamoja na wananchi wapiga kura wamehadaika kiasi gani na hii comedy ya mchaka mchaka Chinja! Arinselema Arijaa!
 
Ndio utajua binadamu tulivyokuwa wanyama kasoro mkia. Sasa hivi Money and Fame unaweza kumuuza hata baba yako mzazi..Na hakuna watu waongo na walaghai kama Wabongo, nadhani duniani tunaweza kuongoza sema hayajawahi tokea mashindano yake tu!.

Soma hii: Tabia ya Watanzania inatosha kuwa kivutio cha Watalii - Pohamba
 
FaizaFoxy mbona umetuoia hewa ya kusoma au ni makengeza yangu!!!
 
Last edited by a moderator:
majungu yao uimara kwa timu yetu,mtaishia kuchonga domo mwisho mh. ndo raisi wa awamu ya 5 JMT
TEAM Lowassa.
 
Last edited by a moderator:
Mtu mmoja akiwa ni mbumbu au mpumbavu basi mara zote hufikiri na wengine ni mambumbu au ni wapumbavu.

Tunawaomba hiyo video ambayo haijafanyiwa slow motion.
 
Afya ya mtu ni siri ya mtu na familia yake!, unless yeye mwenyewe aseme wazi kuwa ni mgonjwa na anaumwa kitu fulani kama alivyofanya JK!. Yes 'jamaa yangu' looks sick, mwenyewe amesema yuko ok, as fit as fiddle!. Who are you kumsemea anaumwa parkinson?.

Tena wewe FaizaFoxy, ni mtu mwenye daraja la juu sana humu jf kwa sababu u miongoni mwa wanawake wacheche humu who can think, most women feels only few think, kama ilivyo kwa most men think, few feels!, na kwa avatar yako suggest wewe ni mtu wa dini, swala 5!, afya ya mtu iko mikononi mwa Mola wako!, unaweza kumuona mtu kama anaumwa akadunda hadi miaka 100!, na kuna mwingine anayeonekana fit kabisa, kesho unaweza kusikia tii!.

Nawaombeni sana tusilete unyanyapaa kuhusu hali za afya za watu, kwa maana hakuna ajuaye siku wala saa!, kila siku iendayo kwa Mungu, Israel humpitia kila kiumbe mara sabaini fii sabaa kwa siku, kuhakikisha siku ikifika, saa ikifiki, dakika ikifika, haipiti hata sekunde!.

Pasco

"Tena wewe FaizaFoxy, ni mtu mwenye daraja la juu sana humu jf". Hayo madaraja aliyapanga nani? This is a misconception. Wengi watakubaliana na mimi kuwa hapa umepotosha. Kwa mfano, ingekuwa ni JK ameshindwa kusimama, huyu dada angemtetea. Is that what you mean by "who can think"?
 
Na timu nzima yenu inaumwa, amepita huku tumemuona anavyotegeshea karibu na gari lake kuongelea hapo mate yanamtoka,hawezi kutembea hatua 20 akinyanyua miguu anaivuta chini kama kinyonga,kaa pembeni huna jipya,
 
Mtu mmoja akiwa ni mbumbu au mpumbavu basi mara zote hufikiri na wengine ni mambumbu au ni wapumbavu.

Tunawaomba hiyo video ambayo haijafanyiwa slow motion.

Video ya nini wakati tumemuona anavyotegeshea kusimama karibu na gari lake ili hasitembe watu wakacheka.
 
Mkuu Nyunyu,

Si dhamira yangu kuendesha marumbano na mabishano, Ni dhamira yangu kueleweshana kwa mwendelezo wa mjadara unaojenga hapa ndani. Nadhani umejiweka kwenye viwango vya kubishana ndiomaana unaniambia mimi sijaelewa na nimeelemewa na mapenzi kwa mgombea wangu!! Hii inathibitisha wazi kwamba umeshindwa kwenye viwango vya kusasambua hoja na badala yake unajificha kwenye kichaka cha kubishana hapa...

Yaani mimi hii leo nikawe team Lowassa, Team Ufisadi..!!! We jamaa wewe..

Kwenye bandiko langu lililopita nimesema kwamba ccm waweke kipengere cha Kutangaza hadharani Ugonjwa wa Watiania wao kwakushawishiwa na wao wenyewe (Wagombea) Sasa Daktari atakuwa na kizuizi gani ikiwa mgonjwa mwenyewe ameamua ugonjwa wake uwe wazi? Wao si watakuwa wanajiamini wako fiti, sasa wataogopaje tena siri za vipimo vyao kuwa wazi? Mgombea pekee aliyetoa suruhisho hilo ni Lowassa na ndo huyohuyo anayedaiwa kwamba anaumwa (Na hapa mi sipingi) Ninachokisema mimi hapa ni kwamba hao wengine wasiutumie ugonjwa wa Lowassa (kama upo) kujijenga wao na kumuangamiza yeye, Kwani ni yeye binafsi kasema yuko tayari kwenda kwenye vipimo..... Ubishi wangu uko wapi hapo?

Katika dharau zoto anazofanyiwa mwanadamu, Dharau ya kufanya maamuzi yake binafsi kwa kuongozwa na pesa ndiyo dharau kuu kuliko zote. Kamwe binafsi siwezi kuiruhusu.!! Tubishane tu kwa hoja, kusema fulani kanunuliwa nasijui anaongozwa na hisia na upofu kwa mgombea fulani hakuna mantiki na hakukujengei wewe na mwingine yeyote moral Authority kumsema mwingine... Tafakari...!! Itoshe tu kusema kwamba tuliopo hapa hatufahamiani, wengi tunatumia Id fake.. Sasa sijui wewe ulimshuhudia nani akinunuliwa na nani mpaka kuja kumsemea hapa Jukwaani..!!!

Ikiwa unataka kubishana kwa hoja, nipo nimejaa tele. Lakini kama unataka kubishana ilmradi kubishana nipuuze mkuu.

Mchana Mwema.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Mental case,

Study : Tanzania :

sub topic: National Elections 2015,

supervised by: Stroke.
 
wewe utakuwa unajua anachoumwa huyu binadamu mwenzako na kwanini useme kuna jambo linakuja?kwani wewe ni Mungu?mimi sio mwanasiasa wala sipo hapa kumtetea wala kumkandamiza Lowassa ila kwa namna ambavyo umeandika hapa kunaonekana kuna kitu unakifahamu kuhusu afya ya huyu binadamu mwenzako aliyeumbwa na Mungu kama wewe na pia huna mamlaka juu ya uhai wake pia.hivi kwa mfano ikitokea leo nimemtokea la kutokea huyu binadamu mwenzio Lowassa ni kwanini wewe usiisaidie Polisi kueleza chanzo na kama ikishindikana kwa polisi wa Tanzania kwa sababu wanazozijua wao na aina ya watu kama wewe basi mengine yote utayakuta kwa Mwenyezi Mungu kuyajibu.Jamani hizi siasa ama madaraka sio kila kitu duniani hadi kufikiria kuweka maisha ya binadamu wengine rehani wakati wote mwisho wa siku tunaishia kufunikwa na udongo huu huu na kuliwa na mchwa hao hao.au kuna watu hawataguswa na mchwa nini??au mchwa wao watakuwa wa dhahabu?????hii ni mbaya sana

Nadhan una matatizo makubwa ya kutotambua nyakati kupitia maandishi.nikusaidie kufumbua ulipoona pamefumbwa.ni hivi sijasema lowasa atakufa bali nachomaanisha ni kupigwa chini kwenye harakati zake ndani ya chama na hapo ndo wapambe wake watabaki wamejikunyata.umeelewa mtoto mzuri?siku zingine usihukumu kabla hujahukumiwa,umesikia heee!
 
Kupunga mkono kwa maandalizi makubwa, kugeuka mzimamzima kama sanamu, mmh.
 
"Tena wewe FaizaFoxy, ni mtu mwenye daraja la juu sana humu jf". Hayo madaraja aliyapanga nani? This is a misconception. Wengi watakubaliana na mimi kuwa hapa umepotosha. Kwa mfano, ingekuwa ni JK ameshindwa kusimama, huyu dada angemtetea. Is that what you mean by "who can think"?

Kama unaweza panda juu nenda ukazibe - Sabah Muchacho
 
Labda wengine mmeshaliona hili:

My Take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana Lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.

Team lowasa wanatufanya kama sisi hatujui lowasa hv duuu
Kizee kinaumwa mpaka kinashindwa kusimama halaf wanalazimisha tuone haumwi duuu
 
Mkuu Nyunyu,

Kwenye bandiko langu lililopita nimesema kwamba ccm waweke kipengere cha Kutangaza hadharani Ugonjwa wa Watiania wao kwakushawishiwa na wao wenyewe (Wagombea) Sasa Daktari atakuwa na kizuizi gani ikiwa mgonjwa mwenyewe ameamua ugonjwa wake uwe wazi? Wao si watakuwa wanajiamini wako fiti, sasa wataogopaje tena siri za vipimo vyao kuwa wazi? Mgombea pekee aliyetoa suruhisho hilo ni Lowassa na ndo huyohuyo anayedaiwa kwamba anaumwa (Na hapa mi sipingi) Ninachokisema mimi hapa ni kwamba hao wengine wasiutumie ugonjwa wa Lowassa (kama upo) kujijenga wao na kumuangamiza yeye, Kwani ni yeye binafsi kasema yuko tayari kwenda kwenye vipimo..... Ubishi wangu uko wapi hapo?

FaizaFoxy na Mzee Mwanakijiji naomba mnisaidie kumuelewesha huyu mkuu hapa suala la ethics na matakwa ya siri kati ya mgonjwa na dakatari. Nimeshindwa kumuelewesha maana hataki uelewa anataka kubishana tu.

Sijasema daktari ana shida, nimesema kitabibu + ethics zake hilo haliwezekani, sasa kama nimekosea nawaombeni wandugu tumfanye huyu mkulu aelewe ugumu wake.
 
Kama hizo video zimefanyiwa Slow motion vp sound yake inasikikaje? maana video iliyofanyiwa slow motion lazima ita affect na sound pia thats why slow motion inawekewa sound effects because original sound imakuwa affected. Mi sijaziona hzo video.
 
Afya ya mtu ni siri ya mtu na familia yake!, unless yeye mwenyewe aseme wazi kuwa ni mgonjwa na anaumwa kitu fulani kama alivyofanya JK!. Yes 'jamaa yangu' looks sick, mwenyewe amesema yuko ok, as fit as fiddle!. Who are you kumsemea anaumwa parkinson?.

Tena wewe FaizaFoxy, ni mtu mwenye daraja la juu sana humu jf kwa sababu u miongoni mwa wanawake wacheche humu who can think, most women feels only few think, kama ilivyo kwa most men think, few feels!, na kwa avatar yako suggest wewe ni mtu wa dini, swala 5!, afya ya mtu iko mikononi mwa Mola wako!, unaweza kumuona mtu kama anaumwa akadunda hadi miaka 100!, na kuna mwingine anayeonekana fit kabisa, kesho unaweza kusikia tii!.

Nawaombeni sana tusilete unyanyapaa kuhusu hali za afya za watu, kwa maana hakuna ajuaye siku wala saa!, kila siku iendayo kwa Mungu, Israel humpitia kila kiumbe mara sabaini fii sabaa kwa siku, kuhakikisha siku ikifika, saa ikifiki, dakika ikifika, haipiti hata sekunde!.

Pasco

Tambua kwamba tunamjadili mtu ambaye atakuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu,mkuu wa nchi na kiongozi wa watu.kama wananchi lazima tujue kiwango cha uimara wa kiongozi wetu.unataka tuchague tu ili wakati wa maadhimisho pale taifa akikagua gwaride atuangukie?unataka tumchague kila siku awe ujerumani kutibu kile anachoita jicho!hiyo mchakamchaka ya maendeleo anayosema ataisimamia lini?kifupi,tunajadili mtu muhimu kwa maslahi ya taifa na si unyanyapaa kama unavyotaka kuhamisha mada.
 
Back
Top Bottom