Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Kwa hali hii akiingia Ikulu uhuru wa media utabaki kua historia.
 
Mi naona hawa wapambe wake wanamtumia km sehemu ya ajira, otherwise wangemshauri apumzike, yaani wanamuangamiza huku anajiona....duh! Hataree
 
Mitanzania ni mijitu mijinga ajabu!. Watu wote wanaompinga mgombea mmoja tuu kwa hoja za ufisadi nao pia ni wajinga tuu kama wajinga wengine, kwa sababu mzazi wa rushwa na usisadi ni CCM!, huwezi kuupinga ufisadi kwa kumnyooshea kidole fisadi mmoja tuu ndani ya chama cha kifisadi kilichojaa mafisadi!.

Huu ufisadi wa CCM haukuanza leo, ufisadi mkubwa wa mwanzo ni EPA, ndipo ikaja Richmond bado uchaguzi uliofuatia sisi waTanzania, kwa ridhaa zetu wenyewe tukaichagua tena CCM!, na hata hii October inayokuja, tutaichagua tena CCM!, huu sio ujinga ni nini?!.

Mijitu ignorants, kila siku kazi kutupigia mikelele humu kuhusu ufisadi, halafu siku ya siku, ikifika, tunakichagua chama kile cha kifisadi, watu wale wale na kurudi kupiga kelele zile zile!.

Kama hoja ni ufisadi, hakuna msafi ndani ya CCM!.

2015 hatutafuti malaika!, Tanzania inahitaji mkombozi, ikitokea mkombozi mwenyewe ndio fisadi, then be it.

Pasco
N

Njaa hizi wa Tanzana zina tumaliza. Inasikitisha sana kwa watu ambao kidoogo unadhani wanauelewa wanapo zama zaidi kwenye ushabiki na si kuimamia maslahi ya nchi.Kizazi kijacho kikiamka kitatudharau sana .lol!
 
Huyo aliyetoa hilo tangazo ni punguani, slow motion kwenye picha iwe kwa Lowassa tu wengine hawajawekewa hiyo slow motion?

Lowassa ni mgonjwa kweli na nilisema humu toka zamani ana kila dalili za Parkinson Disease wala haihitaji kuwa daktari kulielewa hilo, kama ni mpenzi wa michezo na umewahi kufatilia maisha ya Muhammad Ali kwenye video utaliona hilo pasi na shaka.

Coordination ya brain na viungo vya mwili wa Lowassa vina synch differently, vina wrong timing.

Lowassa ni mgonjwa. Full stop.

Halafu angepumzika, wala tusingejua yote haya!
 
Kama mtakumbuka wakati Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma alimtaja Karamagi Nazir kama mbunge. Alishasahau kama
Nazir Karamagi siyo mbunge! Pia alipokuwa Kigoma alisahau kabisa kama yupo jimbo la rafiki yake kipenzi Peter Serukamba hadi mwishoni kabisa ndipo akakumbuka!

Pia Lowassa hana uwezo wa kushika kitu maana anatetemeka sana! Ikumbukwe kuwa bungeni hajawahi kusoma taarifa ya kamati yake akiwa kama mwenyekiti kwa miaka yote mitano! Pia aliongea mara moja tu katika mjadala bungeni hata hivyo hakumaliza dakika tatu! Sidhani kama hata gwaride tu anaweza kukagua achilia mbali kusimama wima kuimba wimbo wa taifa!

Wakati wa mkutano Arusha Lowassa alipopanda jukwaani alijaribu kukimbia ila alipofika katikati alishindwa ikabidi ashikiliwe kwa muda na yule cemera man akafanya kuchukua picha kwa mbali ili watu wasione!

Pia alipokuwa akisoma alikuwa anatetemeka sana mikono hali iliyomfanya camera man asionyeshe kabisa eneo la mikono na picha alikuwa anaikatia juu!
 
Kuumwa si kufa.

Kama anaumwa anaumwa tu, kama ulivyokiri anaonekana anaumwa siri ya nini?

Anaogopa akisema anaumwa atakosa Urais?

Kwanini ang'ang'anie Urais?

Km kiingozi mkubwa mtarajiwa anayeshikilia maisha ya mamilioni ya watu ni muhimu watu wake wakajua juu ya afya yake
 
Hivi kwanini tunapenda sana longolongo. Wewe unayesema zimeeditiwa POST ORIGINAL ILI SISI tujue kama kweli hizi ni fake au ni orginal. Maneno matupu hayajibu. Post original hapa watu waone. Wenzenu wamepost na nyie postini sio kuleta longolongo. Kwanini tukuamini wewe wa maneno matupu badala ya yule aliyeleta ushahidi wa macho?
 
Kudharauliwa, kama kaka yangu Mzee Mwanakijiji alivosema, tusha dharauliwa. Mana kwa mgombea anayetuhumiwa kuwa mgonjwa, na ninavyoona kwa matazamo wangu kuwa Lowasa ni mgonjwa; lakini bado umati mkuuubwaaa unatoka kushangilia na kumtia nguvu agombee; kwa hiyo wao, wa TeamLowasa tayari walikwisha tudharau, maana ndai ya mioyo yao wanajua mzee wao ni mgonjwa. Wanajipa moyo, kuwa akishaingia tu mengine yatajiseti.

Wewe kama ni mtumiaji mkubwa wa social media utakubali, Lowasa anadhaminiwa na watu lukuki. Kwa mazingira ya kawaida, ni dalili ya kupendwa na watu. Kama amenunua hao au la haijalishi ukweli unabaki pale pale watu wanampenda, au ndivyo inavyotengenezwa tujue "anapendwa" Tumekwisha dharauliwa na hao.

ImageUploadedByJamiiForums1434969601.924282.jpg
 
Last edited by a moderator:
Labda wengine mmeshaliona hili:

My Take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana Lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.

Kwanza kabisa ili udharaulike lazima uheshimike. Wewe Mzee Mwanakijiji unatumika kisiasa utapata wapi heshima? Nenda mkale hela za Escrow anozogawa mzee wa Mtama ila mwisho wake ni mwezi wa saba
 
Mitanzania ni mijitu mijinga ajabu!. Watu wote wanaompinga mgombea mmoja tuu kwa hoja za ufisadi nao pia ni wajinga tuu kama wajinga wengine, kwa sababu mzazi wa rushwa na usisadi ni CCM!, huwezi kuupinga ufisadi kwa kumnyooshea kidole fisadi mmoja tuu ndani ya chama cha kifisadi kilichojaa mafisadi!.

Huu ufisadi wa CCM haukuanza leo, ufisadi mkubwa wa mwanzo ni EPA, ndipo ikaja Richmond bado uchaguzi uliofuatia sisi waTanzania, kwa ridhaa zetu wenyewe tukaichagua tena CCM!, na hata hii October inayokuja, tutaichagua tena CCM!, huu sio ujinga ni nini?!.

Mijitu ignorants, kila siku kazi kutupigia mikelele humu kuhusu ufisadi, halafu siku ya siku, ikifika, tunakichagua chama kile cha kifisadi, watu wale wale na kurudi kupiga kelele zile zile!.

Kama hoja ni ufisadi, hakuna msafi ndani ya CCM!.

2015 hatutafuti malaika!, Tanzania inahitaji mkombozi, ikitokea mkombozi mwenyewe ndio fisadi, then be it.

Pasco

Watu waliendelea kuichagua ccm kwa kuwa wale mliopokea vijihela vya mafisadi na mmetumika kama vibara wa ufisadi.Na hata sasa unakanusha ufisadi sio issue...mara tena unatamka ugonjwa sio issue...

Wazee wa vibahasha huu ni mwisho wenu kutupandikizia rais.Ukanjanja wa media hauna nafasi tena.
 
hivi la ufisadi wameshindwa hadi wakomae na afya yake!!!!!!!

Hata huko nako watagonga mwamba. Kwa jinsi wanavyoacha single moja na kudandia nyingine, inaonyesha wazi kwamba "Mzee" kawashika pabaya.
 
Labda wengine mmeshaliona hili:
My Take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana Lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.

Nirejee nukuu yao ili tuwadharau:
  • "Mtu mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu wakati anajua una akili, ukikubaliana nae anakudharau"- Mwl. Nyerere

Huyu haumwi na ndiyo raisi anayefuata. Hata hao walioko huko sidhani kama wote wazima. Na kama angekuwa na tatizo asingepewa fomu

Teh teh!…fomu mmewapa mpaka wa darasa la saba(Bihole wa kigoma)!…na yule underage(wa mzumbe )!…ndiyo mtashindwa kuwapa fomu hata "WAGONJWA??"
 
Hata huko nako watagonga mwamba. Kwa jinsi wanavyoacha single moja na kudandia nyingine, inaonyesha wazi kwamba "Mzee" kawashika pabaya.

huyu jamaa yenu hawezi chomoa hilo jiti...wanamla kichwa ati
 
Halafu angepumzika, wala tusingejua yote haya!

Munamsema Lowassa gani?huyu anayepita huku mikoani kutafuta wadhamini na kujichanganya mbele za watu???naanza kukubali maneno ya Gwajima huyu jamaa ni Yoshua wa leo!!!ile nyimbo ya ufisadi imechujaje???Si amekubali kupima afya kwa wagombea wote????siamini kama tumehishiwa hoja kiasi hiki!!!!
 
Ndio utajua ibnadamu tulivyokuwa wanyama kasoro mkia. Sasa hivi Money and Fame unaweza kumuuza hata baba yako mzazi..Na hakuna watu waongo na walaghai kama Wabongo, nadhani duniani tunaweza kuongoza sema hayajawahi tokea mashindano yake tu!.

Mkuu Mkandara nashangaa, na ndiyo maana nimesema hapo mwanzo, wanatudharau. Maana TeamLowasa wanajua jamaa yao ni mgonjwa, halafu kuna watu tunanunuliwa kuja kumpokea kwa bashasha kama mgombea pendwa wa chama.
respect wa boda sina dhamira ya kuendelea kubishana na wewe, maana hujaelewa, ama hutaki au umezingwa na hisia za mapenzi kwa mgombea wako, kuwa, kupima inawezekana kwa wagombea/watia nia wote, lakini kutangaza ni ngumu kwani "ethics" za kitabibu haziruhusu siri ya daktari na mgonjwa wake kutangazwa na daktari bali mgonjwa mwenye au mwakilishi wa mgonjwa kwa ridhaa ya mgonjwa.

nyinyi mlokubali kununuliwa na kuaminishwa upuuzi endeleeni kuamini Lowasa yuko fit; wenye kuona mbali twasema yu hoi bin taaban. Hata video aliyoweka FaizaFoxy hapo juu inaoneka hujaangalia kwa upofu wa hisia juu ya jamaa yenu.

Hongereni...
 
Last edited by a moderator:
Teh teh!…fomu mmewapa mpaka wa darasa la saba(Bihole wa kigoma)!…na yule underage(wa mzumbe )!…ndiyo mtashindwa kuwapa fomu hata "WAGONJWA??"

Hilo nalo neno lakini
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, japo mimi siko Team Lowassa, wala team yoyote, ila namsupport huyu 'jamaa yangu', kiukweli tangazo hilo is a mistake!, kwanza namfahamu huyo jamaa aliyesaini hapo anajiita Mshauri wa Siasa wa Team Lowassa Makao Mkuu, the way alivyoiweka ni misleading, watu wanaweza kudhani ni kweli huyu ndie mshauri wa Team Lowassa, kiukweli huyu ni kiongozi wa fb group na whatsup group linalojiita team lowassa na huyu ndio mshauri wa group hilo.

Mimi nimeiangalia video moja hiyo ya kukaa, ni bonafide genuine, kuhusu hali ya afya ya 'jamaa yangu' hata mtu mwenye macho tuu ya kawaida, hahitaji kutumia darubini au hadubini kuona au kuelezwa kuwa mzee ni mgonjwa, ila, hali ya afya ya mgombea sio miongoni mwa sifa, vigezo au sababu ya kukubalika au kukataliwa, kwa sababu inachohitaji CCM sio kiongozi bora, kama CCM inataka kiongozi bora itampitisha Jaji Agustino Ramadhani. CCM haihitaji kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kuihamisha Tanzania hapa ilipo kuifikisha kule ilikopaswa kuwepo. Ingehitaji kiongozi wa aina hii ingempitisha Prof. Mhongo, Dr. Magufuli au Prof. Mwandosya. Rushwa na ufisadi sio tatizo kwa CCM, kwa sababu CCM ndie mzazi, mlezi na msimamizi mkuu wa rushwa zote na ufisadi wote unaolitafuna taifa hili.

CCM inachohitaji ni ushindi tuu!. CCM inataka kushinda tuu uchaguzi kwa landslide victory, kwa njia yoyote ile, na kwa mbinu zozote, yaani by hooks and crooks!. Kiongozi wa kuwapatia CCM hiyo landslide victory ni huyu 'jamaa yangu', hiyo afya ataimarishwa na yule yule anayesimamia kuhakikisha 2015 'jamaa yangu anatinga Ikulu ya Magogoni au kupitia CCM au kupitia njia nyingine yoyote!.

Ikitokea ni yeye akapitishwa na CCM, then huyu ndie rais wetu 2015!. Ikitokea asipitishwe na CCM, chama chochote atakachojiunga nacho ndicho chama kitakachoishika ikulu yetu!. Hii hali ya afya tunamuachia YEYE ambayo huyu 'jamaa yangu' ameishasema wazi kuwa "nayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!.

Kwa sasa zimebaki siku 10 tuu muhimu!.

Pasco

Kwa kiasi kikubwa Pasco umemaliza
 
Mitanzania ni mijitu mijinga ajabu!. Watu wote wanaompinga mgombea mmoja tuu kwa hoja za ufisadi nao pia ni wajinga tuu kama wajinga wengine, kwa sababu mzazi wa rushwa na usisadi ni CCM!, huwezi kuupinga ufisadi kwa kumnyooshea kidole fisadi mmoja tuu ndani ya chama cha kifisadi kilichojaa mafisadi!.

Huu ufisadi wa CCM haukuanza leo, ufisadi mkubwa wa mwanzo ni EPA, ndipo ikaja Richmond bado uchaguzi uliofuatia sisi waTanzania, kwa ridhaa zetu wenyewe tukaichagua tena CCM!, na hata hii October inayokuja, tutaichagua tena CCM!, huu sio ujinga ni nini?!.

Mijitu ignorants, kila siku kazi kutupigia mikelele humu kuhusu ufisadi, halafu siku ya siku, ikifika, tunakichagua chama kile cha kifisadi, watu wale wale na kurudi kupiga kelele zile zile!.

Kama hoja ni ufisadi, hakuna msafi ndani ya CCM!.

2015 hatutafuti malaika!, Tanzania inahitaji mkombozi, ikitokea mkombozi mwenyewe ndio fisadi, then be it.

Pasco
Umenena kweli. Lakini haizuii watu kuchukua taadhari. Ofisi hiyo inahitaji myu aliye na afya kamili ili kukifhi matakwa ya majukumu yake. Na hii ni kwa kila aina ya kazi ina matakwa yake...
 
Back
Top Bottom