Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Mwanakijiji hizo zimefanyiwa photoshop. Ni muendelezo wa kuchafuana watia nia. Hata km mtu humkubali lakini simama katika ukweli siku zote utaonekana muungwana !

Akili nyingine sijui zinatumia betri??!!!
Wqdau wameomba original version . . . . .. .Weka hizo uzi ufe. . . .
 
Ni sawa mkuu na umenena vyema.
Suala linabaki pale pale nani atamfunga paka kengere. Genge la wanasiasa ndo wanatengeneza vigezo vya wagombea wao kutoka kila chama. So far, kama Pasco anavyosema kila wakati chama pendwa ndiyo kinaongoza dola. Kinapaswa, au kwa matazamo wa haraka kuwa role model; hicho ndicho kimeweka pemneni kigezo cha afya; kwa hiyo logically nakubaliana hatuwezi mpa mtu uongozi wa nchi akiwa na afya tete. Kisheria huwezi mbana yeyote maana haijawekwa popote, kwamaba afya bora ni moja ya kigezo!!!

Kwa hiyo hapa tunaongelea, technically hakuna wa kumbana mgombea yeyote atakayethibishwa kuwa na afya mbovu, maana si kigezo na hakikuandikwa kokote! Kama wao watalazimisha kumleta mgombea yeyote... ambaye sisi wananchi tunaamini ni mgonjwa, kwa umoja wetu tumkatae. Kumkataa, ndo shida inapokuwa, what if kati ya watakaomleta akakubali kwa wengi!! Atapita tu, na taongoza kwa style yeyote iwayo.

So relax...
Pasco let's be objective. FaizaFoxy kasema and I quote "ana kila dalili za Parkinson Disease wala haihitaji kuwa daktari kulielewa hilo" Kwa kiswahili, nadhani na yeye pia ameonyesha mashaka na siku ameonyesha full diagnostic results kuwa ni Parkinson Disease.

Au miye ndo nakosea hapa, inawezekana kiswahili kimenipiga chenga. Na dada yetu hapo ni mswahili haswaaa...

Tukirudi kwenye mada, ni kweli, afya si moja ya vigezo hili halina shaka. Lakini kwa hali ya kawaida, waTZ tusitawaliwe na mapenzi na hisia kali juu ya mgombea pendwa tukasahau tutaliingiza taifa katika gharama!!! Kazi kubwa kama uraisi naamini inaambatana na level za stress kwa hali ya ju, sasa kwa hali tunayoiona si itakuwa shaka na tete...
respect wa boda hakuna anayemshambulia Pasco, tunasema ukweli. Ukweli ambao hata Pasco amesema kuwa ukiangalia video ya kukaa kwenye kiti, ni "bonafide genuine" Je mkuu hayo maneno ya Pasco unayaelewa maana yake? Hakuna anayemshambulia Pasco tunajadili. Na Pasco hajasema anashambuliwa tunajadili, maana sisi ni sehemu ya Jukwaa la Wafikiriao kwa kichwa na si kwa feeling.
FaizaFoxy ametaja "kila dalili za ugonjwa" hajatuhumu Lowasa kuugua huo ugonjwa, bali kasema kila dalili... wakuthibitisha hayo ni daktari wake na familia yake. Hili liko ndani ya uwezo wa hao tulowataja, na ndo maana mimi msimamo unabaki Lowasa anaumwa, kwa kuwa sina uhakika na ugonjwa anaoumwa sijautaja; tunaelezea dalili za machoni, ambazo zaweza kuwa kweli au si kweli.

Lowasa alisema chama kiandae utaratibu wa kuwapima wagombea wote ikiwamo na yeye, hii ni kauli ya kisisasa maana hata yeye anajua hilo haliwezekani, hata ukiwapima uamuzi wa kutangaza matokeo hautakuwa wa chama bali mgombea binafsi. Na ninadhani hii inaweza kuwa sababu kubwa ya kutoweka afya kama kigezo, chama hakina uwezo kutangaza matokeo ya kiafya ya mgombea yeyote yule. Kwa kwa technicality hii Lowasa na yeye alisema vile out of jazba maana anajua haiwezekani. Sasa sisi ambao haya hatuyajui, tunatokwa mapovu pasi kuruhusu akili zetu kufikiri mara mbili.

Yeye anajijua, anaumwa. Nyinyi ambao mnaamini vimaneno vya niko fit kwa mapambano, haya subirieni, only time will tell na tutakaa pamoja kama waTZ kukubali kumbe alikuwa anaumwa!!!!

Mfungo memo ndugu, kama wafunga weye...
Mkuu , nimependa objectivity yako na logical thinking kwenye hili la ugonjwa, much respect kwa hili!.

Kuna kitu cha msingi sana umekizungumza, ambacho nakubaliana na wewe 100%, kuwa maadam urais ni ajira, na haijawahi kutokea Tanzania kwa a sitting president kuachia kiti hicho kwa ugonjwa, then kama yalivyo masharti ya ajira zozote, kupimwa afya ni muhimu, na hata joining instructions za shule na vyuo zinahitaji medical examination, hivyo na sisi kama hatua za tahadhari, NEC iliweke hitaji la medical examination report kama kigezo, ili vyama wakati vikitafuta wagombea wake, watia nia wao wote wawajibike kupimwa afya ili disqualification katika hatua za awali, lakini huu mtindo wa sasa ambapo kipenga kimeishapulizwa, halafu kila zikionekana dalili za mchezaji super star kutaka kufunga goli, watu wanahamisha milingoti ya goli!, mtahamisha magoli hadi lini?!.

Wanayemtaka Lowassa sio CCM ni watu!, Lowassa ni mwana CCM, ana sifa zote za kuomba kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea, ikitokea CCM wakaamua hawamtaki, it is fine, hakuna yoyote humu anayelazimisha lazima Lowassa apitishwe, ila wenye uamuzi wa mwisho wa nani ni rais wa nchi hii sio CCM, bali ni watu!, kama CCM hawamtaki, na sisi wananchi tunamtaka, then it is ok, CCM wamkate, na asimame chama chochote, wananchi wanaomtaka, watamuingiza ikulu, na hapo ndipo litatimei lile neno la Mwalimu kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM!.

Niliwahi kuzizungumza streghths za Lowassa hapa Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa
ila pia niliwahi kuliweka wazi hili kuwa Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu 2015!.

Pasco
 
Lowasa cyo mgonjwa shida yake ni pombe kali anazokunywa

ameanguka zaidi ya mara 3,na juzi kati mlinzi wake "Tendewa"Alimuwahi asianguke ingekuwa mara ya 4
Kitu cha Hennessy
 
Mkuu lancanshire, kiukweli kabisa, mtu kuitwa mjinga wengi wankutafsiri kuwa ni kutukanwa, lakini mimi natafsiri kuwa mjinga ni kutokujua tuu, ukiishajulishwa, ukajua, then ujinga unakutoka!. Kama dhambi kuu ya Lowassa ni ufisadi wa Richmond, then endelea na ujinga wako, utakapoelimishwa kuwa Lowassa ni mbebaji tuu, huo ujinga utakutoka!.


Na hii sasa naomba nisiirudie tena, ila kwa msiojua, Richmond ndio ile ile Dowans, na ndio hii hii Simbioni, Mkataba ni ule ule, mitambo ni ile ile, na ile capacity charge ya shilingi 152 kwa siku bado ni ile ile!. Ile tozo ilikwisha lipwa siku nyingi!.

Sisi Watanzania ni wajinga!, tungekuwa na akili tungejiuliza kama tuliuvunja mkataba wa Richmond/Dowans kwa sababu ya ufisadi wa capacity charge ya shilingi milioni 152, tukashitakiwa, tukashindwa kesi, tukatozwa faini, tukailipa kisirisiri, sasa tumepandishiwa bili za umeme kufidia deni, na tunalipa, kisha ile ile Dowans tulioikataa kwa mbwembwe zote kule bungeni, ndio hii hii Simbion, mkataba ni ule ule, capacity charge ile ile!, tumeshuhudia watu waliojiapiza kwa maneno "over my dead body", siku hiyo walicheza ngoma za kwao na Obama kwenye Simbion, na sasa hakuna tena wa kujiuliza!, huu kama sio ujinga ni nini?!.

Niliwahi kusema hivi mahali, Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!, na leo bado nasema, tena na tena, we are either ignorants au tumelogwa!.

Pasco
Uchafu wa lowasa si kwenye richmond tu. Hata kwenye huu mchakato wa kutaka kuteuliwa anacheza rafu.au huoni?
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji Umegongelea msumari wa moto wa nch 6 kwenye Jeneza la safari ya matumaini!

Hapa naona akina Pasco wanatapata tu, JUA LIMESHAZAMA KWENYE HII SAFARI!

Ni dakika ya 90 sasa "safari ya matumaini" 0 Vs 5 MMM!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzee Mwanakijiji Umegongelea msumari wa moto wa nch 6 kwenye Jeneza la safari ya matumaini!

Hapa naona akina Pasco wanatapata tu, JUA LIMESHAZAMA KWENYE HII SAFARI!

Ni dakika ya 90 sasa "safari ya matumaini" 0 Vs 5 MMM!
 
Last edited by a moderator:
1. Pasco NEC iweke kigezo cha afya??!!!. . . . .. . seriously human conscioisness haiwezi ona hilo mpaka liandikwe??!!! Amini watu wanaona na wana akili timamu labda tu huwa hawapewi taarifa sahihi na za kutosha katika wakati muafaka. . . . .

Wananchi hawahitaji muongozo wa maandiko juu ya mambo kama haya, wanahitaji taarifa sahihi tu ili wafamye maamuzi sahihi. . . . . .,. Ngonjera, vifijo, vigelegele na shamrashamra zote zitakuwa na maana kama wananchi watafanya "informed decision making". . . . . huwa unajutanabaisha hapa hujaajiriwa na mambo kama hayo unasahau tu "the power to decide took you this far", . . . . .empower others too. . . . .
 
Last edited by a moderator:
Ukikamua maziwa asubuhi halafu ukaja kuyachemsha jioni usishange yakiganda.......mgombea wenu hatoshi!!!!
 
1. Pasco

Wananchi hawahitaji muongozo wa maandiko juu ya mambo kama haya, wanahitaji taarifa sahihi tu ili wafamye maamuzi sahihi. . . . . .,. Ngonjera, vifijo, vigelegele na shamrashamra zote zitakuwa na maana kama wananchi watafanya "informed decision making". . . . . huwa unajutanabaisha hapa hujaajiriwa na mambo kama hayo unasahau tu "the power to decide took you this far", . . . . .empower others too. . . . .
Mkuu OLESA, kila kitu kwenye nchi, huendeshwa kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni!, hakuna sheria kuhusu watangaza nia kupimwa afya zao, hakuna kanuni juu ya hili na hakuna utaratibu rasmi!, hivyo bado niko very right kuitaka NEC ilete uraratibu huo, utungiwe sheria, zitungiwe kanuni!.

Hili la wananchi kufanya "informed decision making" ni very important, ili hao wananchi waweze kufanya informed decisions, inabidi kwanza 'wawezeshwe' ili waweze. Swali langu ni dogo tuu, tangu lini Watanzania tunachagua rais kwa kufanya informed decisions?!. Kama unaweza kukumbuka tatu bora ya 2005 ambayo waliingia Jakaya, Dr. Salim na Prif Mwandosya, alafu aliyechaguliwa ni Jakaya Kikwete, ukiangalia alichaguliwa kwa vigezo gani, then utakubaliana na mimi kuwa mgombea wa CCM, 2015 ni Edward Lowassa, provided kama CCM ni ile ile, watu ni wale wale na vigezo ni vile vile!, unless kama CCM imebadilika!.

Pasco
 
kwa bahati nzuri na kwa mda maalumu nimekuwa karibu na huyo anayetajwa humu....mengi nimeyashuhudia na ni zadi ya haya yanayosemwa humu...ni ukweli usiopingika kwamba lowassa anauwa tena anaumwa sana...hali yake si nzuri kabisa. siku za mwanzo kabla hajabadili utaratibu wa maisha hasa nyakati za usiku alikuwa anapata shida sana anapolala, kugeuka hawezi. ikitokea daktari amechelewa kumdunga sindano na kumpa vidonge basi atavimba vidole,miguu, kutembea hataweza na akitembea basi atajikokota sana, hataweza hata kupiga mswaki, achilia mbali kushika kikombe cha chai....
kuna siku alikuwa arusha kuonana na baba askofu wa katoriki wakati wa mazungumzo alimba udhuru zaidi ya mara sita kwenda kujisaidia haja ndogo hata baada ya kuonyeshwa mahali pa haja hiyo bado aliomba mtu wake ampeleke (siku natangazia nia arusha alikwenda haja ndogo mara mbili akitkea pale jukwaa kuu)...alitembea kwa shida sana, vidole vilikuwa vikitetemeka sana,na baada ya mazungumzo mzee alishindwa kupanda kwenye gari..kunyanyua mguu ilikuwa ni shida sana mpaka akasaidiwa....
lowasa hapo alipo hawezi kugeuza shingo..anageuka mwili mzima ..ngozi ya mwili wake imebadilika kwa kiasi kikubwa ..weupe alio nao wa sasa si kawaida, hawezi hata kukunja nne...hatua ilipofika kwa sasa analala chumba kimoja na daktari wake na mkewe chumba kingine ili daktari aweze kumwangalia kwa ukaribu...

wakati flani kwenye mazungumzo alisikika akisema anatamani awe rais wa nchi hata kwa wiki mbili tu...hata hivyo tahadhari zote zimezingatiwa katika kumpata rais wa nchi anayefaa ...

yeah! sasa nimeelewa kwa nini anawambia ukawa "mnaweza kuongoza hamuwezi" wanajibu "tunawezaaa" , anauliza can you? wanajibu "yes we can !!!" kama hizo habari za ugonjwa ni kweli basi inaonekana kabisa lengo lake ni kusaidia kuchukua madaraka ya nchi kutoka kwenye mikono ya ccm na akizidiwa awaachie ukawa waendelee. Yote mema tu...
 
Back
Top Bottom