Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Hili Tangazo la Timu Lowassa linatudharau!

Kama zimefanyiwa Slow motion watupe zile original tuzione.

Na aliyefanya hiyo slow motion ni kiboko hasa, manake watu wote alionao pamoja wakiwemo walinzi wake wote wako noma vizuri tu, hawajaathiriwa na hiyo slow motion isipokuwa yeye tu, teh teh teh
 
Kudharauliwa, kama kaka yangu Mzee Mwanakijiji alivosema, tusha dharauliwa. Mana kwa mgombea anayetuhumiwa kuwa mgonjwa, na ninavyoona kwa matazamo wangu kuwa Lowasa ni mgonjwa; lakini bado umati mkuuubwaaa unatoka kushangilia na kumtia nguvu agombee; kwa hiyo wao, wa TeamLowasa tayari walikwisha tudharau, maana ndai ya mioyo yao wanajua mzee wao ni mgonjwa. Wanajipa moyo, kuwa akishaingia tu mengine yatajiseti.

Wewe kama ni mtumiaji mkubwa wa social media utakubali, Lowasa anadhaminiwa na watu lukuki. Kwa mazingira ya kawaida, ni dalili ya kupendwa na watu. Kama amenunua hao au la haijalishi ukweli unabaki pale pale watu wanampenda, au ndivyo inavyotengenezwa tujue "anapendwa" Tumekwisha dharauliwa na hao.
Pia ninachojiuliza hivi il slow motion katengenezewa yeye tu, bodyguard hakuwekwa slow motion???
Afu ukiangalia vizuri ile video unaona kabisa network ya mzee ilikata kabisa
 
respect wa boda hoja yangu ni moja tu. . . . .Wadhamini ni wananchi, watakaongozwa ni wananchi na wqpiga kura ni wananchi. . . . . .waachwe wazungumze kwa mapana na marefu juu ya mgombea yeyote yule. . . .Bila kuvunja utu wala sheria hilo tu baas. . . !!!

Hapo tuko pamoja mkuu, hakijaharibika kitu,

Tatizo kunawatu wanataka kuvisha akili zao vichwani mwa wananchi kwa maslahi yao kisiasa. Hao ndio ninaowakataa mimi. Wanachi wanawajua watu wagonjwa na watu wazima, iwe kiafya au kisiasa ,wagonjwa wanajulikana.!! Wasitumie ugonjwa wa mtu kama mtaji wao kisiasa. Washindane kwa hoja, iwapo Afya ni jambo la lazima kwenye nafasi hiyo then wote wakapime.

Kwa mtizamo. huo mkuu nadhani tuko pamoja.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Mbona hiyo slow motion ina aply kwake tu? Je hao wanaomsaidia mara kumpandisha ngazi, mara kumvutia kiti, mara kumletea kiti aangalie ngoma? Hayo yote ni slowmo?

Tuambie ukweli.

Kwanini maongrzi yanayomzunguka hayaathitiwi na hiyo slow motion hata watu waliomzunguka?
 
teh teh hii ndo nguvu ya hoja na umma LOWASSA NI MGONJWA OVER
 
Kwa katiba ya Tanzania hakuna uchaguzi wa marudio.

Kama ikatokea Rais amefariki basi Makamu wa Rais ndiye anakuwa Rais kwa kipindi kilichobaki.

Kama ni hivi basi Makongoro awe mgombea mwenza wa edo, manake automatically Makongoro atabaki kuwa rais mzalendo tunayempenda (kidding though)
 
Bahati mbaya, ndugu yangu malihoja nakufahamu vizuri sana. huu ni mwendelezo wako wa kujifanya unafikiri juu ya vichwa vya watu wengine. hivi una mamlaka gani ya kutupa maelekezo kana kwamba tuna fikra zinazofanana kwa huyo mtu wako mgonjwa kweli? hivi unaweza kutoka na akili timamu na kupinga kuumwa kwa huyo mzee hata kama si kwa kiwango hicho unachofikiri wewe? mbona hamtuamibii kwamba mpaka sasa ameshaanguka mara ngapi badala yake unakuja na suala la slow motion? unadhani atakusadia katika mkakati wako wa kugombea ubunge kule kwenu? kuna jambo moja tu linakuja nalo haliko mbali sana, ambapo mtakaa kama watoto yatima.

Mkuu Samahani,mie Malihoja ni rafiki yangu FB,anategemea kugombea ubunge wapi ili na Mimi nifahamu?
 
Mkuu Nyunyu,



Yaani mimi hii leo nikawe team Lowassa, Team Ufisadi..!!! We jamaa wewe..

Kwenye bandiko langu lililopita nimesema kwamba ccm waweke kipengere cha Kutangaza hadharani Ugonjwa wa Watiania wao kwakushawishiwa na wao wenyewe (Wagombea) Sasa Daktari atakuwa na kizuizi gani ikiwa mgonjwa mwenyewe ameamua ugonjwa wake uwe wazi? Wao si watakuwa wanajiamini wako fiti, sasa wataogopaje tena siri za vipimo vyao kuwa wazi? Mgombea pekee aliyetoa suruhisho hilo ni Lowassa na ndo huyohuyo anayedaiwa kwamba anaumwa (Na hapa mi sipingi) Ninachokisema mimi hapa ni kwamba hao wengine wasiutumie ugonjwa wa Lowassa (kama upo) kujijenga wao na kumuangamiza yeye, Kwani ni yeye binafsi kasema yuko tayari kwenda kwenye vipimo..... Ubishi wangu uko wapi hapo?


Ikiwa unataka kubishana kwa hoja, nipo nimejaa tele. Lakini kama unataka kubishana ilmradi kubishana nipuuze mkuu.

Mchana Mwema.

BACK TANGANYIKA

= kipengele
= suluhisho
 
Mkuu Samahani,mie Malihoja ni rafiki yangu FB,anategemea kugombea ubunge wapi ili na Mimi nifahamu?

Haaa mngoni huyo,umepata picha? Tena cha ajabu anajiita mshauri wa lowasa mambo ya siasa,nimecheka sana.huyo aseme hivi,mshauri wa lowasa mambo ya mitandao maana ana vicertificate vingi vya kompyuta na amevipatia nje ya nchi.
 
wakuu dunia itatuona watanzania wote hewa, kama tutamng'oa mtu uwaziri mkuu kwakuwa ni fisadi halafu sisi tugeuke eti tunamtuma nje ya nchi kutuwakilisha kwa hili ccm wakimpitisha ntaamini wamechoka kama alivyosema mh. mwanasheria kule bungeni
 
kwa bahati nzuri na kwa mda maalumu nimekuwa karibu na huyo anayetajwa humu....mengi nimeyashuhudia na ni zadi ya haya yanayosemwa humu...ni ukweli usiopingika kwamba lowassa anauwa tena anaumwa sana...hali yake si nzuri kabisa. siku za mwanzo kabla hajabadili utaratibu wa maisha hasa nyakati za usiku alikuwa anapata shida sana anapolala, kugeuka hawezi. ikitokea daktari amechelewa kumdunga sindano na kumpa vidonge basi atavimba vidole,miguu, kutembea hataweza na akitembea basi atajikokota sana, hataweza hata kupiga mswaki, achilia mbali kushika kikombe cha chai....
kuna siku alikuwa arusha kuonana na baba askofu wa katoriki wakati wa mazungumzo alimba udhuru zaidi ya mara sita kwenda kujisaidia haja ndogo hata baada ya kuonyeshwa mahali pa haja hiyo bado aliomba mtu wake ampeleke (siku natangazia nia arusha alikwenda haja ndogo mara mbili akitkea pale jukwaa kuu)...alitembea kwa shida sana, vidole vilikuwa vikitetemeka sana,na baada ya mazungumzo mzee alishindwa kupanda kwenye gari..kunyanyua mguu ilikuwa ni shida sana mpaka akasaidiwa....
lowasa hapo alipo hawezi kugeuza shingo..anageuka mwili mzima ..ngozi ya mwili wake imebadilika kwa kiasi kikubwa ..weupe alio nao wa sasa si kawaida, hawezi hata kukunja nne...hatua ilipofika kwa sasa analala chumba kimoja na daktari wake na mkewe chumba kingine ili daktari aweze kumwangalia kwa ukaribu...

wakati flani kwenye mazungumzo alisikika akisema anatamani awe rais wa nchi hata kwa wiki mbili tu...hata hivyo tahadhari zote zimezingatiwa katika kumpata rais wa nchi anayefaa ...

Duh hatarii

cc Heaven on Earth njoo ujionee mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Mjadala umefungwa Lowassa ni mgonjwa

Mkuu kula lyke (sema nimetafuta kidude nmekikosa)

Kiukweli mambo 2 hayaepukiki kwa edo,
1; UFISADI (RICHMOND)
2:UGONJWA

nahic atakuwa anawakati Mugum sana hata kama atapitishwa, maana zile kampan za kuzunguka vijijin kusimama kwa saa 1 itakuwa ngum sana,

Huon mwenzake aliwahi dondoka?? Ila walao yy ni kwa sabab za kiimani (kufunga)

Tunachozungumzia c ugonjwa tu bali afya ya mzee haiko vzr, huhitaji elim ya chuo kujua kuwa ni mgonjwa au yy ni FiSadi...

Juzi nmemsikia anasema anawaambia watu kuwa hahofii kukatwa jina, nadhan alikuwa na maana kuwa ikitokea wakamkata jina anaweza kwenda kwingine maana anawafuasi, sasa acjiamini sana, anaweza kujikuta amedondoka kwa kihoro baada ya matokeo ya kamati ya maadili..

Kwa sasa hyo nafasi inahitaji mtu asiekuwa na tuhuma ya wizi au Mgonjwa, huo ndiyo ukweli japo ni mchungu kwa teamedo...
 
Wanamuonea huyu bure kabisa kweli kuna kiongozi mmoja msafara wake unakuwa na ambulance na aliishaanguka zaidi ya mara moja.
 
1) Mbona wao hawatupi au kusambaza hizo ambazo hazina slow motion? Kama hizo video ziko edited, wasambaze wao basi ambazo ni original.

2) Na video itakuaje edited kwenye vitendo tu halafu sauti isiwe edited? si maneno yatapishana na vitendo?

3) Inawezekanaje wanaonekana watu wawili kisha mmoja akawekewa slow motion mwingine asiwekewe na wote tunawaona pamoja kwa wakati huohuo mmoja? Editing ya wapi hiyo?

Asante! Popote ulipo agiza moja moto moja barid nakuja kulipa
 
Kuumwa si kufa.

Kama anumwa anaumwa tu, kama ulivykiri anaonekana anaumwa siri ya nini?

Anaogopa akisema anaumwa atakosa Urais?

Kwanini ang'ang'anie Urais?
Ugonja ni hali, hakuna anayeamua awe mgonjwa au awe mzima bali ni Mola wetu.

Uamuzi wa kuweka bayana uzima au ugonjwa ni uamuzi binafsi wa mtu, daktari wake na familia yake!, maadam amejieleza wazi kuwa yuko fit!, no matter how sick he looks, nasisitiza yuko fit!.

Maadam hali ya afya sio kigezo cha kuupata au kuukosa urais, this is a non issue!.

Hakuna mtu anayeung'ang'ania uras, maadam urais upo, na umetangazwa kwa yoyote anayeutaka, amejipima amajiona anauwezo, why not asiutake!, kwani hao wengine 37 wao hawautaki?!, au wamechukua fomu za kujaribishia tuu?, si ni wote wanautaka?!.

Rais wa Tanzania 2015, ni yule tuu aliyeandikiwa!, ikitokea ni yeye, no one can change a thing!, kama sio yeye, hatu watu humu mdhikir uchi, hawi!.

Pasco
 
Afya ya mtu ni siri ya mtu na familia yake!, unless yeye mwenyewe aseme wazi kuwa ni mgonjwa na anaumwa kitu fulani kama alivyofanya JK!. Yes 'jamaa yangu' looks sick, mwenyewe amesema yuko ok, as fit as fiddle!. Who are you kumsemea anaumwa parkinson?.

Tena wewe FaizaFoxy, ni mtu mwenye daraja la juu sana humu jf kwa sababu u miongoni mwa wanawake wacheche humu who can think, most women feels only few think, kama ilivyo kwa most men think, few feels!, na kwa avatar yako suggest wewe ni mtu wa dini, swala 5!, afya ya mtu iko mikononi mwa Mola wako!, unaweza kumuona mtu kama anaumwa akadunda hadi miaka 100!, na kuna mwingine anayeonekana fit kabisa, kesho unaweza kusikia tii!.

Nawaombeni sana tusilete unyanyapaa kuhusu hali za afya za watu, kwa maana hakuna ajuaye siku wala saa!, kila siku iendayo kwa Mungu, Israel humpitia kila kiumbe mara sabaini fii sabaa kwa siku, kuhakikisha siku ikifika, saa ikifiki, dakika ikifika, haipiti hata sekunde!.

Pasco

Yes, hata Aerial Sharon wa Israel alidumu miaka zaidi ya mitano akiwa in the coma. Tunataka mtu mzima wa kufanya kazi na si yule wa kuzungukwa na manesi 24/7
 
Back
Top Bottom