stabilityman
Senior Member
- Jul 9, 2024
- 199
- 344
Rejeeni hapa kuna link inayowarejesha kwenye fungamano la odinga na ruto achilia mbali wanasiasa wengine hata wale ambao hawajajitqikeza
Ndo maana niliwaambia wananchi wanaweza jiaminisha au kuamini kuwa tatizo ni ruto na litatatulika akitoka
Ila wasomi na wanasiasa na wafukunyuaji wanajua tatizo ni deni kubwa la nchi ya kenya dhidi ya mbinyo wa wanaoidai kenya na nchi za magharibi katika kuhofhi uchumi wa kenya kutokea katika mikataba ya ukopaji na athari ya strings attached ambapo imepelekea kuanza kuonyesha makali yake katika macro economic policies and elements
Kuelewa hili vyema rejea mdororo wa sei lanka na maandamano yaliyotokea mpaka kuitoa serikali ya kifamikia familia ya ukoo wa kina rajapaksa japo kwa suala lao kulikuwa na vita vingine vya kiuchumi na kisiasa vyenye mkono mkubwa wa nje kati ya nguvu za ushawishi za china us &europe na india
Mantiki yangu sio kumtetea ruto japo nae alijichanganya katika mkumbo wa siasa za kidunia anapoingia mkenge wa igogoro ya madola makubwa kama usa na europe dhidi ya china na urusi
Ilhali anajua fika kuwa modola hayo pia na yenyewe yapo katika mkaati maalumu wa kujipenyeza afrika na kuindoa ushawishi wa dola za kimagharibi kama ufaransa na marekani hasa katika maeneo ya ilivyokuwa himaya ya francophone mfano nchi za bukinafaso mali niger jamhuri ya afrika ya kati n.K
Sasa kuivagaa mikenge hiyo inaweza pelekea madola hayo kuingiza misaada kwa wapinzani wake au kuwezesha uandaaji wa mipango ya kumvurugia zaidi uongozi wake kupitia convert mission na hybrid welfare zingine maana kwa afrika ukiweka dola milioni 2 za marekani kwa waumda zengwe ahh mbona jambo lako linaleta impact hata kama halitafanikiwa ila athari yake itaonekana unachokifanya unatia upupu kwenye maji ya chooni kisha unawaacha wanaotafutana uchawi washutumiame na kulumbana mpaka idara za usalama zijue mchawi nani ahh mbona kitambo choo kishavunjwa afu kila mtu akajisaidie mashambani au vichakani kisha kesho na kesho kutwa wahusika wabang'atwa na nyika au kuliwa na wanyama wakali ama kuumwa kipindupindu kuhara na homa ya matumbo kisha wanakuja kwako uwauzie dawa ama uwape misaa ama uwakopeshe hela ya kujenga choo kipya walichokijenga kwa mkopo ambao bado hawajamaliza ulipa na riba zinaongezeka kisha unawakopesha kwa masharti afu wanaanza kukulipaa tena kwa riba hukubwakitunishiana tena misuli safari hii ukiweka tena upupu siishii kuchoma moto choo bali nakuloga na puru lako tuone utajisaidia na nini 😃🤪
Sasa tuachane na fashion ya utani turudi kwenye mada kiuhalisa kwa mwanasiasa yoyote mwenye akili na naamini ruto sio mjinga ama hajui analotaka ama analofanya kama ambavyo wakenya wengi wanavyojidanganya ama kutaka ionekane hivyo lah hasha ruto ni mwanasiasa mfanyabiazhara mbobezi hivyo kwake hii game yote ilikuwa fursa haijalishi kama ilikuwa na risky ya kugharimu heshima yake historia yake ama uongozi wake lah hasha aliijua nini kitatikea na akaendelea na mpango wake makusudi ili atimize lengo najua wakenya wengi mnajiamini kuwa siasa zenu ni za pelee enu na watanzania ni wajinga hawana cha kuwaambia kisa kiingereza 😃😊
Iko hivi nimekuwa nikifatilia sana hotuba za ruto hasa akiwa nje ya kenya tukiamzia ile alipomtembelea waziri mkuu wa india narendra modi na ile aliyofanya katika bunge la ulaya achana na hii aliyotamani kufanya katika bunge la congress marekani alipomtembelea joe biden au ile press no hizo sio hotuba real maana alienda akiwa amekwama na akataka kupata pesa za imf na nafuu zingine za uchumi wa marekani hivyo nilitarajia aongee chochote ili kupata anachokitaka japo hakupata mkwamuo wa maana kiuchumi ila pesa mbuzi na kupewa hadhi ya juu ya ushirika wa umoja wa kujihami wa nchi za magharibu kwa nchi isiyo mwanachama
Ni zawadi chonganishi kwake maana inazidi kuweka kenya katika mahusiano tata na washirika wengine ambao wana uhasimu na nchi za magharibi kama china na urusi achilia mbali nchi za afrika ambazo zinapambana kuondoa ushawishi wa ulaya na marrkani kijeshi barani afrika ikiwemo tanzania uganda somali congo ethiopia south afrika zimbabwe n.K ambapo baadhi zina mahusiano tata na tishio la kuingliwa kiuongozi kupitia mbinu za kichochezi upandikizi na kijeshi
Sasa nije kwenye point ruto na wakenya wanataka nini, changamoto kubwa ya kenya inatokea kwenye mbinyo wa magharibi kupitia athari ya uchumi wa kenya kujifungamanisha sana na mfumo wa magharibi ambapo matokeo yake makali ya ubepari wa kenya yamezidi kuwa na mbinyo mkali kwa wananchi wa kenya wa kawaida ambao awali udhaifu wake haukuonekana sana maana kulikuwa na pengo kubwa la maendeleo ya kiviwanda na uchumi kati ya nchi ya kenya na majirani zake hivyo nakisi ya fedha za kigeni ilimezwa na hela zilizoingia kenya kutokea kwenye biashara ya kimataifa kati ya kenya na majirani zake pamoja na biashara kati yake na mataifa ya ulaya na marekani hasa kutokea kwenye mazao ya malighafi
Kumbuka kipindi cha nyuma kenya ilikuwa mnufaika mkubwa wa biashara za kikanda uwekezaji wa ulaya na marekani biashara ya kuuza makighafi nje ya nchi kama maua parachichi pareto bidhaa za viwandani n.K pamoja na kuvutia uwekezaji kutoka nchi ya marekani uingereza na ulaya kwa sababu kuu zifuatazo
- Athari ya ukoloni kutokana na kuwa nchi ilivyokuwa makao makuu ya ukoloni wa uingereza kwa afrika mashariki ambayo toka mwaka 1885 uingereza iliwekeza pale mpaka ilipoachia uhuru na wala haikutengeza uadui na uingereza wala mfumo wa kibepari baada ya uhuru kama ilivyo tanzania wala kuwa na machafuko ya vita kama ilivyo tanzania uganda somalia msumbiji hivyo paliendelea kuwa rafiki kwa wamagharibi
Athari ya uwekezaji wa uingereza marejani ulaya na wakenya wenyewe katika viwanda miundonbinu elimu sheria sera haki za umiliki wa ardhi akili bunifu biashara n.K
Lazima tuelewe kuwa kitendo cha kenya kuwa imeendelea zaidi na kuziacha mbali nchi zingine kiviwanda kiuchumi kimiundombinu maana yake ilipelekea mitaji msingi ya nje , pesa nyingi za kigeni na watalii wengi wafanyabiashara wengi na mashirika mengi ya kibiashara kuvutiwa na kenya na kuufanya kenya kuwa hub ya kiuchumi na kimaingiliano hivyo kupelekea kenya kupata pesa zaidi na zaidi
Chumi za ulaya japani na marekani kuwa katika hali nzuri za ukuaji hivyo kupelekea kuwa na nahitaji makubwa ya malighafi, pesa nyingi za uwlezaji pesa nyingi za mikopo na uwezo mkubwa wa ku outsource ama kusambaza viwanda ama sehemu za uzalishaji kenya rejea namna makamouni ya kiingereza na marekani yalivyokuwa katika ukuaji jinsi brands za glaxosmith unilever n.K zilivyokuwa katika ubora wake katika masoko ya kenya
Mambo hayo ya juu yalipelekea kenya kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi na kupata pesa nyingi za kigeni huku ikiziacha mbali nchi jirani kutokana na kuwa na advantages nilizozitaja hapo juu
Sasa tujuzane nini kimebadilika kenya kikanda na kidunia
Nchi jirani na kenya zimebadilika na kukuza uwezo wale wa kuvutia wawekezaji mitaji miundombinu na kukuza viwanda na elimu
Nchi jirani na kenya kama Tanzania uganda zambia ethiopia zimepunguza sehemu ya mapato ya kenya kupitia hatua zili,opiga katika nyanja ya elimu miundombinu sera sheria viwanda kilimo n k hivyo zimepunguza nafasi ya bidhaa za kenya katika masoko yao na kupelelea kupungua kwa nguvu ya viwanda vya kenya kusambazia na kunufaika na masoko ya nchi jirani mfano maziwa ya brookside ya kenya kwa sasa hayaana nguvu kubwa katika soko la uganda kutokana na maziwa ya lato ya uganda bidhaa za blueband unilever ya uk zilizokuwa zikizakishwa kenya kenya kwa sasa nchi nyingi za afrika mashariki hazitegemei kenya kuzipata kama ilivyokuwa zamani bidhaa za sausage juice kiwin.K ambazo nchi nyingi zilinunia kutoka kenya kwa sasa nchi nyingi zinazalisha ama kuagiza pengine kutokea hapo kuna mitaji kodi ajira na pesa ambapo serikali ya kenya imepoteza ambapo zamani ilizipata kwa wingi na urahisi kutokana na pengo kubwa la nguvu za kiuchumi
Kukua kwa uchumi wa nchi jirani na kupunguza pengo la maendeleo ya uchumi kupitia.Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu viwanda elimu sera sheria na utulivu kumepelekea kenya kuanza kupunguza unafuu wa gharama za kiuwelezaji na kizalishaji hivyo baadhi ya wawekezaji ambao zamani walikuwa wanaenda kenya wanaanza kuonana nchi kama tanzania ethiopia na zambia ni nchi nafuu kigharama na kimiundombinu tofauti miaka ya nyuma hivyo ushindani unakuwa na manufaa yanapungua mfano tanzania ndo nchi ya kwanza kwa vivutio vingi vya utalii afrika na ya pili duniani baada ya brazil lakinikipindi cha nyuma kenya ilikuwa inaongoza kwa kupokea watalii wengi zaidi kuliko tanzania ambapo sehemu ya watalii hao walikuwa wanapitia kenya na kuletewa tanzania ili kufanya utalii kwa sababu ya ubovu wa miundombinu rafiki kwa utalii matangazo n.K ambaoo kenya ilifikia hatua ya kunadi hata baadhi ya vivutio vya utakii vya tanzania kuwa vikokena mfano mlima kilimanjaro , maana yake kuamka kwa tanzania kiuwelezaji kunapokonya share ya kenya katika mapato ya utalii achilia mali kuboreshwa kwa miundonbinu ya relief barabara viwana vya ndege kinapelekea kupokea watalii wengi ambao awali walisukumwa kwenda kenya
Kumbukeni pia hizi nchi jirani zinapoendelea zinaanzia kuweka mazingira magumu kwa washindani wa kenya kufanya la,I katika nchi zao katika sekta ambazo wazawa wao wamepata ufanisi rejea tanzania kubana ufanyakazi wa wakenya tanzania katika biashara viwanda ualimu nk
Kushukuk kwa ukuaji uchumi wa ulaya marekani na mdororo wa nguvu za uchumi za magharibi dhidi ya kukua kwa uchumi wa china na nchi za mashariki hasa asia
Rejea sehemu kubwa ya uchumi wa kenya ilifungamanishwa na uchumi wa nchi za magharibi hasa marrkani uingereza na ulaya sasa maaa yale ni kwamba chumi zao zikiyumba na wakaanza kufunga mikanda wanapunguza uwekezaji mitaji mikopo usambazaji teknolojia na hata misaada na utalii hivyo mapato yake yana athari
Kukua kwa uchumi wa china na nchi za asia
Hii imepaelekea kushuka kwa masoko ya viwanda vingi vya ndani kutokana na kushindwa kwa ufanisi wa bei kutokana na kuzidiwa kiteknolojia hapa unapoteza ajir
Naomba niweke angalizo hizo sababu sio pekee ila zina athari kubwa zikikutana na factors zingine za ndani japo athari kubwa ililetwa na sababu kuu za kiuchumi zilizotikisa nguzo za ndani ambazo nazo zina nyufa kama zifuatazo
Mgawanyo mbovu wa rasilimali za uzalishaji mfano mkuu ardhi ambapo tabaka kubwa la wananchi hawaodhi ardhi bali makundo ya wafanyabiashara wanasiasa na matajiri ambao wanamiliki sehemu kubwa ya ardhi ya kenya huku masikini wakitaabikabkuipata ama kulipa gharama kubwa kunitumia kiuzalishaji au makazi ama kuwa na ardhi karme
Athari za ukabila na siasa za ukanda na makundi
Kupanda kwa gharama ya maisha na gharama za chakula riba kodi n.K
Athari ya kutetereka kwa shilingi ya kenya kutokana na sababu za kidunia mikopo na sababu zingine xa kiuchumi
Kupungua kwa nguvu ya kenya katika kuhodhi ama kuathiri mienendo ya kiuchumi ya nchi jirani kiuzalishaji masoko ushindani n.K
Kushuka kwa siko la mazao ya biashara na oñgezeko la washindani kimauzo katika soko la dunia huku kukiwa na athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi teknolojia n k
Mabadiliko ya tabia ya nchi kame mkali ukosegu wa maji katika maeneo ya kati na changamoto za kiusalama.
Sasa hayo yote yakikutana na ongezeko kubwa la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji wa kiuchumi ajira mitaji maisha bora huku watu hao wakipata elimu ya kujitambua na kuina maisha manono ama propaganda za maisha manono za nchi zingine lazima wadai katika nchi yao na hasa katika ulimwengu huu wa mitandao ambapo taharifa na propaganda zina nafasi ya kusambaa haraka zaidi na kukusanya nguvu ya umma
Sasa nini nataka kusema ni ukweli usiofichika kuwa athari zilizotokea hapo juu nikadhiorodhesha zilipunguza mapato ya kenya hivyo kuathiri utimizaji wa majukumu ya serikali na changamoto kubwa ni kuwa kutokana na ushindani wa siasa za kenya na hulka ya wanasiasa wa kiafrika kulinda vyeo kwa gharama yoyote viongozi wengi waliwekeza kwenye kukopa ili kuendesha miradi ili kuepuka kuonekana wadhaifu kiutendaji haijalishi athari ya miradi kwa uchumi ilikuwa na faida kiasi gani ama iliwezesha taifa kunufaika kiasi gani achilia mbali sehemu kubwa ya mikopo hiyo iliwelezwa katika miradi ya kutoa huduma badala ya miradi ya uzalishaji mali na biashara ama uwekezaji wa miundombinu faidishi kiuchumi pia kuna wimbi la pesa za mikopo iliyokopwa kwa rib kubwa kuibwa kunyonywa kufujwa ama kutumika kwenye maisha ya anasa za kiserikali badala ya uwekezaji mfano kulipana posho kununua mgali ya kifahari kulipa mishahara kughalamia miradi binafsi rushwa matumizi ya kampeni mbalimbali nakadhalika
Sasa kiuchumi deni la taifa linapaswa kuwa himilivu na mara nyingi wanasiasa hudanganya wanachi kuwa deni ni himilivu mpaka liamze kuwakaba ndo hujifanya wanaurupuka kama hawakuwepo deni la kenya lilishaanza kuwa mwiba kitambo na ndo chanzo kenya kuanza kupata ugumu wa kukopesheka mfano rejea ziara ya rais uhuru kenyata na raila ofinga kwenda china pamoja ili kuinyesha mshikamano kwa ajili ya kupata mkopo wa kuendeleza reli ya sgr inayotumia diesel kutoka kipande cha nairobi mpaka uganda ambapo ilishindikana wakafanikiwa kupata mkataba wa kenya kuruhusiwa kuuza maparachichi china pia rejea sintofahamu za kupata mkopo wa kujenga bandari ya kizazi cha nne ya mombasa
Rejea ziara ya rais wilium ruto marekani na namna mazungumzo yake na taasisi za fedha za magharibi juu ya kupata unafuu wa kulipa madeni ya mikopo ya kenya na riba zake pamoja na kuimba tena mkopo mwengine ambapo ndilo lilikuwa lengo kuu la ziara yake nchini marejani rejeeni taharifa ya faida ilizopata kesha muangalie kiwangi katika pesa na masharti waliyopewa na imf ili kupata mkopo mwengine ndipo mtajifunza kitu
Sasa bhasi lazima mjue kuwa kenya inapopungukiwa rasilimali za asili kama madini ardhi hifadhi kubwa za bahari gas tushukuri wamegundua mafuta ambapo wingi wa hizo rasilimali unazipa nafasi kubwa hizo nchi kupata mikopo zaidi na kikubwa zaidi maana wakopeshaji wana hakikisho kuwa nchi ukikwama kulipa wanaweza zitwaa kimkakati na kusimamia uvunaji wake mpaka warudishe mikopo yao riba zai na cha juu ama wana hakikisho la nchi zao kupewa haki za kuvuna na kurudisha faida
Na hili ndo lengo kuu la wakopeshaji we gi siyo ulipe m ujikwamue kiuchumi bali ukwame kisha wahodhi rasilinali zako kisha wakutawale ili kujihakikishia chumi zao daima zina makoloni yalopata uhuru wa bendera na mikopo ni sehemu ya nyenzo za ukoloni mamboleo
Sasa I ruto odinga wala kenyata wasiojua kilichomkuta ruto sio kosa lake la moja kwa moja bali ji matokeo ya uruthi wa nchi ambayo waliopita wameijenga na kuiharibu kwa nafasi yake hivyo hawawezi kumlaumu moja kwa moja wala kujizubaisha kuwa hawajui nini chanzo na nani kasababisha zaidi maana takwimu zitawaumbua na mara wakianza hilo ruto nae anaweza anza kutoa siri na nyaraka za kuwaumbuabkatika madhaifu yao achilia mbali kuwavua nguo mbele ya wananchi
Pia viongozi hao wanajua fika muswada wa finance bill wa 2024 ni matokeo ya pressure za muda mrefu za deni la taifa la kenya na pressure za wanaoidai kenya kutaka kulipwa pesa zao amabpo hapa unazungumzia waaodai kama nchi jumuia za kimafaufa mashirika ya mikopo na mitaji mabenki wafanyabuashara wakubwa na taasisi mbalimbali za uwelezaji na pesa sasa msumali wa mwisho uliopelekea mpaka serikali kuleta finance bill 2024 inayochochea uongezaji kodi na kubana matumizi ya ustawi ni ziara ya wilium ruto nchini marrkani ambapo majafiliano yake na shirila la fedha la kimataifa imf na matajiri wa kimagharibi yaliwela mashariti na mbinyo katika ulipaji deni la kenya na vigezo vya kupata mkopo mpya ili kutimiza matumizi ya marekani katika nakisi ya bajeti
Ruto angeweza kukataa ili afe kiume marejani afu azikwe kihuni na wakenya pindi ambapo wangemuunga mkono awali kwa kukataa masharti kandamizi kisha wangemgeuuka nyumbani kenya pale ambapo serikali ingekosa pesa za kujiendesha ama kuhudumia wananchi matokeo yake huduma zianze kuwa mbovu na maisha kuwa magumu amapo wakenya wangesaau kuwa chanzo si yeye na wangemsulubu na kumbebesha lawama kwa kushindwa kuendesha nchi huku wakiwa washammaliza katika sanduku la kura sasa alichokifanya ndo siasa halisi ilipo na ndipo alipowapiga bao la kisigino wake ya na ana nafasi ya kuja kuyateka mageuza waliyo yaasisi na kuja kuyafya kuwa mtaji wa kisiasa huko mbeleni
Kaliacha bunge lipitishe muswada kisha kajifanya anakubali na haungi mkono wananchi hapo awali kawaacha waandamane na kumuinyesha nguvu yao na dunia kuona hasira za wananchi wa kenya kisha ndo atatumia video zao kwenda kuongea tena na wanaomdai kwa kujifanya yeye yuko tayari kutii masharti yao ila shid wakenya ni kichwa ngumu hivyo kuyatekeleza ni hatari kwake na kwao kwa hiyo wampunguzie mbinyo maana mwisho wa siku kenya ikiingaa katika machafuko itakuwa ngumu wao kupata haa hiko wanachotaka kw wakati hivyo bora wampunguzie masharti na kumpunguzia kiwango ili atawale kisha yeye atatoa offer nyingine ya rasilimali za kulinda mkopo ama ku restructure deni la taifa la kenya ili liweze kulipika bila kuathiri uchumi na mustakabali wa kenya katika kiwango kikubwa zaidi kinachotishiabamani na usalama wa nchi
Wazungu hawawezi kukataa la watakubali kwa masharti mepesi kwa ruto magumu kwa kenya ambayo kwa ruto itamuwezesha kumaliza awamu yake ya utawala huku akimuachia ajae mzigo wa mwiba kama yeye alivyoachiwa as long maslahi yake ya kisiasa na ya kundi lake hayataathirika sana kama yalivyo ya wakenya wakaida walioandamana
Wazungu watakubali maana kwa sasa dunia nzima inawanyooshea kidole kwa unyonyaji na ukoloni kana kwamba wako peke yao hivyo hawataki wapigiwe kelele zaidi na pia hawataki kuipoteza kenya kama nchi rafiki na eneo la kiushawishi ukizingatia eneo la kenya katika pwani ya afrika mashariki na bahari ya hindi achilia mbali kiuchumi kikeshi siasa na rasilimali maama wanajua kuibana sana kenya kutapelekea kenya ijipeleke zaidi katika mikono ya ushirika wa washindani wao ambao ni china urusi india irani uae saudi arabia turkey kumbuka china nae anaidai deni kubwa kenya ila yeye anauma na kupuliza kama hayupo
Saa wilium ruto kwa wananchi kawachezea mchezo wa kuk
Wepa lawama kwa changamoto zozote za kiuchumi zitakazoketwa na deni la taifa maana zitakaootokea atawaambia chanzo cha haya majanga ni ukubwa wa deni hivyo hatuwezi kopa zaidi ama mikopo ni migumu ndo maana niliongeza kodi ili nilipe madeni yaliyorundikwa na watangulizi wangu ambapo lengo langu niwatoe tujibane kwa muda ili tuitie nchi katika utumwa wa madeni na kupoteza uhuru kutokana na kudaiwa sasa nyinyi na millenial gen y na hasa gen z si ndo mlikuwa na kiherehere cha kukataa sasa mlitaka hiyo pesa alipe nani au itoke wapi sasa msione hali ngumu ni kupata mitaji na mikopo imekuwa ishu na athari ya deni la taifa ndo inaathiri riba thamani ya pesa ya nchi uwekezaji na akiba ya pesa za kigeni na ushindani wa kiviwanda hivyo matokeo yale ndo haya hicho nawaombabndugu zangu wakenya tushikamane na tusimame oamoja tutashinda 😆😊 msinilaumu mimi kosa si langu
Katika hili pia ruto ameweza kuteka agenda ya mustakabali wa kenya maana kupitia majadiliano ya kitaifa juu ya changamoto za kiuchumi za kenya ruto anakwenda kupata msingi wa kupenyeza ajenda zake kupitia makundi mbalimbali ya washiriki na msingi wa visingizio kupitia muafaka wa jumla wa marifhiano maana kutikeo hapo athari yoyote itahusishwa na sababu ya utekelezaji wa maadhimio ya wakenya ndo maana tunafanya hivi ama vile ama maazio yale ndo yameleta changamoto hizi hivyo kama mnakosoa basi tuvunje maadhimuo tupate mwelekeo mpya ama hapa natekeleza moango wenu kwa hiyo msinilaumu kukwamua kwake maana mlitaka wenyewe pale mlipopinga mpango wangu uliolenga kuwaokoa dhidi ya matatizo yaloletwa na awamu zili,opita.
Faida nyingine ambayo ruto anapata ni kuweza kuwajua wabaya wake na makundi hatarishi kwake hivyo kujua namna ya ku deal nayo maana bila mvua kunyeha huwezi kujua panapovuja hivyo kwa sasa kupitia maasusi wake , washauri wake kamati zake za ulinzi na usalama rutio kashajua watu hatarishi kwake iwe wanasiasa wafanyabiashara wananchi wasomi viongozi wa dini n.K maana yake ni suala lla team ruto kuandaa mkakati wa kudeal nao iwe kupitia usimamizi wa rasilinali na nyenzo za kiutawala ama kuwagawa na kuwatawala ama kuwavutavkwake kwa kuungana nao ama kuwananiliu
Ruto kapata kundi lake la dhati la kusimama nao na kuendana nao na namna njema ya kuandaa mkakati wa kuvuka uchaguzi ujao maana kashaonja upande wa oili wa shilingi na ana nafasi ya kubalance karata zake kutokana na mafunzo intelejensia na washirika aliyokusanya hivyo anajua wapi ataoata mbegu na wapi atapanda na wapi atafukia
Ruto kapata kukwepa mbinyo mkali wa magharibi na kusogeza mbele fundo la kitanzi loje kumuangukia ajae pia ruto kwa sasa kapata fundisho la namna gani ya kudeal na mataifa makubwa na kukwepa migogoro yao isivagae siasa zako maana yamkini kupitia vuguvugu hili kapata msaada kwa hata asiowatarajia ama kakosa kwa aliowataraji achilia mbali kaona uwezo wa fitna za aliowaingilia na kujua wapi pa kuendelea kupiga na wapi pa kuacha kuomba msamaha
Mwisho ruto kaiona jasho machozi na damu ya wakenya vilivyomwagika si tu katika kupinga finance bill2024 bali kilio cha ugumu wa maisha na kudai mipango na utekelezaji sahihi wa kukuza ustawi na maisha ya wakenya maana wanateseka mno kwa mibinyobya kiuchumi inayowaonyesha wana uchumi mkubwa kwa gharama ya ustawi hafifu wa maisha
Yote kwa yote makala hii haijalenga kubeza juhudi za wakenya kulipambania taifa lao wala kubeza mchakato wao wa kujenga taifa lao bali kuwaonyesha upande wa pili wa karaa za kisiasa uchumi na nguvu zingine za kikanda na kidunia zinavyoweza chochea kutokea kwa baadhi ya mambo katika dunia yenye mengi yasiofahamika na wengi katika urahisi
Angalizo
Mageuzi na mapinduzi huwa vina asili ya kutekwa na kuua manufaa yake kwa walioyapigania iwapo walioyapigania hawatasumamia utekelezaji wake ama kuwa na umojawa kulinda misingi viingozi na mwelekeo wa mapinduzi hivyo niwasihi wakenya msijisahau mmeshinda goli moja mpira bado haujaisha hivyo bado hamjajihakikishia ushindi wala pointi 3 wala ubingwa . Aluta continua
Imeandikwa na
Ubongo wa mbongo
Nick mbatina.