Ududu
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 1,020
- 556
Hata mimi siamini kabisa kama huyu mzee kafikia huku!!!Haya ni moja ya matumizi mabaya ya Mb zako Mzee Mwanakijiji.
Last edited by a moderator:
Hata mimi siamini kabisa kama huyu mzee kafikia huku!!!Haya ni moja ya matumizi mabaya ya Mb zako Mzee Mwanakijiji.
Lowasa anaumwa hata ukimwangalia usoni tu anaonyesha dalili ya kutaka tiba ya kimwili na kiroho.
Du, afadhali wewe mkuu umekuja na vipimo vya macho,
lakini huyu Lowasa ni Mbunge, ni Mjumbe wa NEC ya CCM na pia ni mwenyekiti wa moja ya kamati muhimu za bunge. haya magonjwa yanakuja baada ya kugombea uraisi? Kwanini tusiamini hizi ni siasa za maji taka toka kwa wapinzani wake wa kisiasa? Du, ile ya Richmond vp imefail????!!!
Mimi jamani naomba kuuliza maana hili limeshatangazwa sana hapa..!!!
Inasemekana kwamba Lowassa anaumwa Parkinson Disease, hili limesemwa sana hapa ndani, na huu ugonjwa unasemekana athari kubwa ni kumsababishia mtu kutetemeka na baadhi ya viongo vya mwili kukosa nguvu.
Swali je ugonjwa huu unasababisha hitulafu yoyote kwenye Ubongo? Je waweza kisababisha kifo?
Lowassa mwenyewe amepata kusikika akisema Ugonjwa na uzima ni neema kutoka kwa Mungu. Akadai kwamba yeye ni mzima wa afya. Akasema yeyote mwenye mashaka na afya yake akishawishi chama chao watengeneze utaratibu wa kila mgombea/mtiania Urais kupimwa ili ijulikane nani mgonjwa na nani mzima. Sasa mbona hatujasikia mrejesho toka kwa wagombea wengine wakishinikiza kwenda kipima ili kupata vidhibiti vya kumzuia Lowassa "Kihalali" kugombea nafasi hiyo kuliko wanavyomchafua bila uthibitisho?
Nijuavyo mimi kunamagonjwa ambayo matokeo yake yanaonekana hadharani na mengine ni ngumu kujua bila vithibitisho vya Daktari. Sawa twaweza kusema Lowassa mgonjwa hata tu atakapoonekana kujikwaa na kudondoka. lakini hao wagombea wengine ni wagonjwa kiasi gani? Au kwasababu hawajawahi kujikwaa na kuanguka? Mbona Kikwete amekaa na ugonjwa huo alioenda kutibiwa Us kwa. miaka takribani tisa madarakani bila mtu kujua? Je upi ni ugonjwa hata, Saratani ya kibofu au Mtetemo wa viongo vya mwili? (Haijathibitika)
Nimeona kina FaizaFoxy Nyunyu OLESAIDIMU na wengine wakijaribu kumshambulia Pasco kwa utetezi wake Lowassa, Je mnajua afya za wagombea wengine wa ccm? Au kwasababu wao miili yao inaficha magonjwa yao ndani kwa ndani?
BACK TANGANYIKA
Kuuguwa na kuumwa si kufa. Usivichanganye, hizo ni sababu tu za kufa ikiwa utakufa, unaweza ukaumwa usife haraka na yule mzima akafa ghafla. - Kumbuka hilo.
Huo ugonjwa unasababisha usahaulifu na kuchanganya maneno pia. Ushahidi wa Lowassa kuwa na usahaulifu na kuchanganya maneno ni pale alipokuwa anahutubia mkutano wa kutangaza nia Arusha, naomba isikilize hotuba yake, alisema kuwa Makamu wa Rais wa kwanza Sheikh Amri Abeid, kwa kujiamini kabisa kumbe alikuwa amesahau kuwa Amri Abeid ni jina la kiwanja anachohutubia na pia kachanganya badala ya Abeid Karume kuwa ni Makamu wa Rais wa kwanza yeye kampachika jina la Amri Abeid.
Mnataka nini zaidi ya huo ushahidi wa wazi kabisa?
Atakapo katwa jina muendelee kumfariji sio mnamkimbia tena
Ndio utajua binadamu tulivyokuwa wanyama kasoro mkia. Sasa hivi Money and Fame unaweza kumuuza hata baba yako mzazi..Na hakuna watu waongo na walaghai kama Wabongo, nadhani duniani tunaweza kuongoza sema hayajawahi tokea mashindano yake tu!.Mi nimeaiangalia video ya mzee Lowasa inatia huruma. Hata kama humpendi huyu mzee utamhurumia ukiiangalia hii video. Hivi kwa nini familia yake wanamwacha anajidhalilisha kiivi? Kwa nini wasimshauri apumzike na kutafuta matibabu?
kwa bahati nzuri na kwa mda maalumu nimekuwa karibu na huyo anayetajwa humu....mengi nimeyashuhudia na ni zadi ya haya yanayosemwa humu...ni ukweli usiopingika kwamba lowassa anauwa tena anaumwa sana...hali yake si nzuri kabisa. siku za mwanzo kabla hajabadili utaratibu wa maisha hasa nyakati za usiku alikuwa anapata shida sana anapolala, kugeuka hawezi. ikitokea daktari amechelewa kumdunga sindano na kumpa vidonge basi atavimba vidole,miguu, kutembea hataweza na akitembea basi atajikokota sana, hataweza hata kupiga mswaki, achilia mbali kushika kikombe cha chai....
kuna siku alikuwa arusha kuonana na baba askofu wa katoriki wakati wa mazungumzo alimba udhuru zaidi ya mara sita kwenda kujisaidia haja ndogo hata baada ya kuonyeshwa mahali pa haja hiyo bado aliomba mtu wake ampeleke (siku natangazia nia arusha alikwenda haja ndogo mara mbili akitkea pale jukwaa kuu)...alitembea kwa shida sana, vidole vilikuwa vikitetemeka sana,na baada ya mazungumzo mzee alishindwa kupanda kwenye gari..kunyanyua mguu ilikuwa ni shida sana mpaka akasaidiwa....
lowasa hapo alipo hawezi kugeuza shingo..anageuka mwili mzima ..ngozi ya mwili wake imebadilika kwa kiasi kikubwa ..weupe alio nao wa sasa si kawaida, hawezi hata kukunja nne...hatua ilipofika kwa sasa analala chumba kimoja na daktari wake na mkewe chumba kingine ili daktari aweze kumwangalia kwa ukaribu...
wakati flani kwenye mazungumzo alisikika akisema anatamani awe rais wa nchi hata kwa wiki mbili tu...hata hivyo tahadhari zote zimezingatiwa katika kumpata rais wa nchi anayefaa ...
Kama zimefanyiwa Slow motion watupe zile original tuzione.