Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 58,962
- 132,583
Mkuu Mzee Mwanakijiji, japo mimi siko Team Lowassa, wala team yoyote, ila namsupport huyu 'jamaa yangu', kiukweli tangazo hilo is a mistake!, kwanza namfahamu huyo jamaa aliyesaini hapo anajiita Mshauri wa Siasa wa Team Lowassa Makao Mkuu, the way alivyoiweka ni misleading, watu wanaweza kudhani ni kweli huyu ndie mshauri wa Team Lowassa, kiukweli huyu ni kiongozi wa fb group na whatsup group linalojiita team lowassa na huyu ndio mshauri wa group hilo.Labda wengine mmeshaliona hili:
My Take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana Lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.
Mimi nimeiangalia video moja hiyo ya kukaa, ni bonafide genuine, kuhusu hali ya afya ya 'jamaa yangu' hata mtu mwenye macho tuu ya kawaida, hahitaji kutumia darubini au hadubini kuona au kuelezwa kuwa mzee ni mgonjwa, ila, hali ya afya ya mgombea sio miongoni mwa sifa, vigezo au sababu ya kukubalika au kukataliwa, kwa sababu inachohitaji CCM sio kiongozi bora, kama CCM inataka kiongozi bora itampitisha Jaji Agustino Ramadhani. CCM haihitaji kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kuihamisha Tanzania hapa ilipo kuifikisha kule ilikopaswa kuwepo. Ingehitaji kiongozi wa aina hii ingempitisha Prof. Mhongo, Dr. Magufuli au Prof. Mwandosya. Rushwa na ufisadi sio tatizo kwa CCM, kwa sababu CCM ndie mzazi, mlezi na msimamizi mkuu wa rushwa zote na ufisadi wote unaolitafuna taifa hili.
CCM inachohitaji ni ushindi tuu!. CCM inataka kushinda tuu uchaguzi kwa landslide victory, kwa njia yoyote ile, na kwa mbinu zozote, yaani by hooks and crooks!. Kiongozi wa kuwapatia CCM hiyo landslide victory ni huyu 'jamaa yangu', hiyo afya ataimarishwa na yule yule anayesimamia kuhakikisha 2015 'jamaa yangu anatinga Ikulu ya Magogoni au kupitia CCM au kupitia njia nyingine yoyote!.
Ikitokea ni yeye akapitishwa na CCM, then huyu ndie rais wetu 2015!. Ikitokea asipitishwe na CCM, chama chochote atakachojiunga nacho ndicho chama kitakachoishika ikulu yetu!. Hii hali ya afya tunamuachia YEYE ambayo huyu 'jamaa yangu' ameishasema wazi kuwa "nayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!.
Kwa sasa zimebaki siku 10 tuu muhimu!.
Pasco