Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
sasa tutashinda kwa kura zaidi ya 40000,kifo cha ccm kimewadia!
 
Wanasubiria na jimbo la Segerea ili tufanye chaguzi mbili kwa wakati mmoja (Arusha Mjini na Segerea). No way Mahanga ile kesi hawezi kuipangua. Tunatoa mbunge mmoja wanaingia watatu CDM...
 
kama suala la matusi basi kila mbunge alitukana mbona nao hawajapigwa chini?
jaji kama yule sikudhani kama hatatumia busara ya kujali chaguo la wananchi,kuangalia garama za kurudia uchaguzi ni kubwa sana...,
Mkuu,hapo nyekundu, Mh. Lema amevuliwa ubunge kwa sababu ya matusi? Mimi sidhani kama hiyo ndiyo sababu kuu. Ninawaomba waliokuweko mahakamani na wanaokijua kisa kizima watuwekee hapa. Lakini ikiwa amevuliwa ubunge kwa matusi, na unasema kila mbunge alitukana, unataka kusema suala la matusi liachwe liendelee kama aibu aliyoitia Lusinde Tanzania kule Arumeru.

Na hapo kijani, hii nchi imeoza, watendaji hawajali Taifa linagharamika vipi, hawajali shida za wananchi. Viongozi wamezowea kula kupitia jasho letu, wanafaidika na mashaka yetu. Umeme ukikosekana, wanaofaidika ni wauza mafuta na majenereta, unadhani hawa wako tayari Tanzania iwe na umeme wa kudumu? Madaktari wakigoma, hispitali binafsi zinafanya biashara nzuri, na nyingi zao zinaendeshwa na vigogo au jamaa zao, kwa hivyo mgomo ni mtaji kwao. Na kila kero inayotokea TZ - ukosefu wa bidhaa muhimu kwa mfano - ujue kuna mtu nyuma yake anafaidika nalo, na pengine husababisha makusudi litokee ili apate manufaa.

Kwa hivyo, hata kurejewa kwa huo uchaguzi, kuna wachache wanalifurahia - viwanda vya uchapishaji, wenye usafiri, mafuta, mahoteli, posho kwa watendaji, yale maji ya washwasha, risasi.... wanataka vitumiwe wakanunue vyengine...kwa hivyo nani atajali mwananchi wa kawaida anateseka vipi?
 
Nataka kujua kama hukumu ilosomwa na huyo kiazi inamkataza kamanda lema kugombea tena ubunge au imetangaza mshindi wa pili ndo atangazwe mbunge
 
Mkuu,
Wanajitesa tu hawa wanaccm...hawataenda mbali!

Haya Matokeo tuliyatarajia tena hasa baada ya CCM KUPIGWA GOLI LA KISIGINO KULE ARUMERU.

Hivyo bado wana uchungu wa kunyanganywa jimbo, wameona heri wapunguze na majimbo ya Upinzani.

Ni pesa nyibgi sana zimetumika Arumeryu, sasa na Arusha mjini ukitrudiwa ni kiama kwa Taifa kwani gharama wanazotumia CCM kwenye kampeni siyo za chama bali za za Taifa.

Tusubiri mfumuko wa bei na kuanguka kwa uchumi katika Tanzania sasa.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hivi ccm inatafuta nini jamani!Arumeru haijawapa fundisho tu! Arusha wasahau kufukuta huko! Labda waende lindi,hata huko watu wamefunguka macho! Hawatashinda arusha hata wahonge watu ndege! Wangeacha hizo pesa za kurudia uchaguzi zikajenge mahospitali na kulipa walimu mishahara jamani! Hii nchi inaniudhi mimi khaaaaa!nipeni updates za mpendazoe na makongoro kwa anaefahamu wapendwa!!
 
Hakuna cha kupoteza kwa CDM.... Kwa hilo umaarufu wetu unazidi kuongezeka mara dufu! Hatuta kata rufaa wala kuilaumu mahakama bali tutaishitaki kwa wananchi siku ya uchaguzi mapema mwezi June 2012.
Nawaomba wananchi wakae kwa utulivu na wajiandae kwa ukombozi rasmi wa jimbo la Arusha mjini haki haipokonyi bali hucheleweshwa!
Mungu ibariki CDM!
 
HAHAAHAHAAH.....naruhusiwa kucheka kidhungu?
Duh Mkuu wewe huwa hulipi Kodi au huoni huruma pesa za wanaolipa kodi na kupoteza muda...
Hii issue haikuwa about Kura, hata wakirudia uchaguzi leo tunajua outcome, kwahio at the end of the day tutakuwa tunapata kilekile kwa gharama ya juu na kupoteza muda.., ofcourse sheria ni msumeno ila sioni sababu ya kucheka, because I can see only loosers here and the biggest loosers are Arusha's residents and Tanzania's Taxpayers
 
Huu us.e.nge ytaendelea hadi lini? serikali haioni kuna mambo mengine ya kufanya zaidi ya kuchaguana chaguana kila siku? tumechoka na sera uchwara bwana waache ujinga bwana
 
Bora hao wanasimamia wanachokiamini kuliko hawa.

Wa nini sasa watu wamesoma na upeo mkubwa afu wanafanya mabaya zaidi kuliko hata wale ambao hawajasoma?

mabaraza ya asili ndio itakuwa tena mambo ya washili kule meru au umesahau?
 
Nawashauri sisiem wasilete timu uwanjani, tuwachapa kinoma, alafu hiyo pr yetu itakuwa juu balaa!
 
Haijawahi tokea viongozi wa ccm kupongeza ushindi wa chama pinzani ila huu wa Arumeru. Na walipofanya hivyo wengi tulishtuka kwa kujua kuwa kuna kitu nyuma yake. Baadhi tulizani ni kutaka kuficha aibu yao kwa kile kilichotokea Mwanza kwa wanachama wa ccm kuwakatakata mapanga wabunge wa Chadema. Hata hivyo imethihirika wazi kwamba sii hilo tu kumbe walikuwa washapanga na hakimu anaesikiliza kesi ya Lema na kujua kwa hakika kwamba watatengua ubunge wake. Hivyo pengezi zao anespected zilikuwa ni kichaka cha kujionyesha kwa mbele ni waungwana kumbe kwa nyuma wameficha kisu cha kudhuru.
Hata hivyo magwiji wa sheria tunaomba mtujuze inakubaliwa je mtu kuwa kadhalilishwa bila yake anaedaiwa kudhalilishwa kudai hivyo? Maana hatukumuona huyo Batilda Burudani kutokea mahakamani kutoa ushahidi.
.
 
Napenda kuuliza chai chapati maharage (ccm) watatumia miujiza gani kuziba pengo la kura 20,000 arusha mjini? Kwani uchaguzi uliopita mgombea wao aliachwa kwa tofauti hiyo kubwa ya kura.

Ushauri wangu ni kuwa wasijisumbue kuweka mgombea maana wataaibika zaidi.
 
Wagamba wanasema Lema alitumia matusi wakati wa kampeni zake,ila ameruhusiwa kugombea tena jimbona,makamanda mkoooo tayarii?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom