Rais wa JMT Mh Samia Suluhu Hassan amesema hana wazo la kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2025.

View attachment 1887958
Chanzo: Gazeti la CCM, Uhuru
Kwa utamu uliopo Ikulu huwa nakuwa mgumu sana Kumuamini Mwanasiasa tena hasa hasa Rais aliyeko Madarakani akiwahi mapema kusema kuwa hatogombea tena Urais wakati hata Miezi yake 6 tu Ofisini bado hajaikamilisha.
 
Huo ni pumbaza jinga.

Subiri by 2025, kampeni za hapa na pale za kumshinikiza na kumchukulia fomu zitapamba moto.
Hakuna kitu kama hicho mama mwisho wake 25 tunamtaka kassim majaliwa kuwa raisi
 
Nadhani watu waangalie vizuri maneno aliyosema Bi Mkubwa. Atakuwa amesema kitu kama hiko hapa chini:

^amesema hana uwezo wa kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu 2025.^
 
Na ni vizuri iwe hivyo.
Majaliwa 2025 kijiti ni chako baba, Tunakuombea
Tukitaka majaliwa lazima tumuombee mama azidi kuvulunda ndipo ccm na wabunge wanaweza kumkubali majaliwa kwa kuwa watakuwa wamepoteza mvuto kwa wananchi na jina la jpm litakuwa juu sana kwa raia hivyo watalazimika kumpa majaliwa maana watanzania wanataka raisi mwenye logic kubwa na kauli moja
 
Bado watanzania tunamuhitaji sana, kwa jinsi anavyo upiga mwingi tunaamini anatosha hadi 2030 atakuwa amekamilisha ungwe yake ya kuongoza kwa miaka 10.
taratibu na desturi za chama ni kwamba Rais aliyeko madarakani ataongoza/kugombea kwa mihula miwili hivyo muhula wa pili wa Rais Samia unaanzia 2025 hadi 2030 (10).
itakapo fika hiyo 2025 matakwa ya watanzania ndio yatakayo amua. sio yeye.
jambo la msingi kwa sasa ni kuomba uzima na afya.
Tunamuombea Mungu ampe afya na uzima.
kazi iendelee.
 
Ukweli usiopingikika ni kuwa Mama amepima Upepo na ameshaona maono kuwa "Hatoshi". Na kwa mwenye uwelewa wa hali ya Kisiasa kwa sasa nchini analiewelewa hili dhahiri bila ya yeye kusema lolote.
 
Nini faida ya kusema hivi sasa hivi, zaidi ya kuwafanya watu waache kufanya kazi na kupanga timu za 2025 ?

Hata kama hauna mpango si ufanye siri yako...
Faida ni kupunguza kunyoshewa vidole maana watu watasema anamalizia muda wake
 
Halafu wakikutana na katibu mkuu wao wanalalamika ooh miezi sita hawana mshahara sasa kwa trash kama hizi, mshahara mnapewa wanini
 
Bado watanzania tunamuhitaji sana, kwa jinsi anavyo upiga mwingi tunaamini anatosha hadi 2030 atakuwa amekamilisha ungwe yake ya kuongoza kwa miaka 10.
taratibu na desturi za chama ni kuwa Rais anaye ongoza ataongoza/kugombea kwa mihula miwili (10).
itakapo fika hiyo 2025 matakwa ya watanzania ndio yatakayo amua. sio yeye.
Au ana hofu gani pengine sijui kwamba eti pengine :) Tanzania sasa maprezidenti hawawezi kukamilisha sekenditemu!???
 
Kwa utamu uliopo Ikulu huwa nakuwa mgumu sana Kumuamini Mwanasiasa tena hasa hasa Rais aliyeko Madarakani akiwahi mapema kusema kuwa hatogombea tena Urais wakati hata Miezi yake 6 tu Ofisini bado hajaikamilisha.
Siyo kweli ingekuwa mama kapokea kijiti toka kwa kikwete basi ikulu ingekuwa tamu sana ila ukumbuke kapokea kijiti toka kwa magufuli machine ya mipango na kazi
 
Huyo mama kapwaya mnoo ! Akili zenyewe hana ! Uraisi sio masihara jamani ! CCM ni zaidi ya balaa ! Shime shime tukiondoe madarakani kidemokrasia tupate kupumua mweeee ! #KATIBAMPYAMUHIMUSANA
kwanza tumuondowe Gaidi namba moja Tz. a.k.a mr. DJ
 
Back
Top Bottom