Ukweli usiopingikika ni kuwa Mama amepima Upepo na ameshaona maono kuwa "Hatoshi". Na kwa mwenye uwelewa wa hali ya Kisiasa kwa sasa nchini analiewelewa hili dhahiri bila ya yeye kusema lolote.
Nasikia alisema kwamba alimwelewa sana Chuma, alifundishwa akafundishika!!! :) Nilivyoona anakohoa kama mara elfu hivi na kitu pale akihutumia BRT kwa dakika 3 (ieleweke Lowassa, pamoja na uzee na ugonjwa wake, alikuwa anahutubia dakika hadi 5 nzima!!!), basi nikathibitisha hapo tumepigwa!!!
 
Siyo kweli ingekuwa mama kapokea kijiti toka kwa kikwete basi ikulu ingekuwa tamu sana ila ukumbuke kapokea kijiti toka kwa magufuli machine ya mipango na kazi
Hawa viwavi wanaoshangilia kuupiga mwingi kwa Bi Mkubwa, katu hawawezi kukuelewa.
 
Hoja dhaifu sana hii Ndugu. Pole mno.
Dhaifu kwako hata kwenye mpira unapo poteza mchezaji bora lazima utafute mchezaji bora ,na huyo mchezaji lazima atatakiwa kufiti pengo la aliye ondoka ,mama mwenyewe alisema kazi aliyo achiwa na magufuli ni kubwa
 
inaonyesha Rais wetu hana uchu wa madaraka kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao wapo tayari kuuwa na kulipua kwa ajili ya kusaka madaraka!! Rais Samia sio mtu wa hivyo, ni mtu anaye tambua kuwa cheo ni dhamana na ni mzigo mzito.
watu wengine anapewa nafasi ndogo tu anataka kuuwa wenzake!! wengine wana ng'ang'ania vyeo mpaka wanaifia ktk vyeo vyao!!!.
kuna watu wana foji mpaka umri wa kuzaliwa ilimradi asistaafu mapema!! wapo kibao, hawataki kuachia vijana!!! haswa kwenye utumishi wa umma kuna watu wanaifia kwenye vyeo vyao hawataki kabisa kupumzika!
 
Tukipata Katiba mpya itatupa Rais Bora na si bora Rais. Huu uongozi wa kupata kwa kubahatisha shida ndio inaonekana sasa kwa udhaifu kiuongozi kuwa wazi kabisa.
 
Hawa viwavi wanaoshangilia kuupiga mwingi kwa Bi Mkubwa, katu hawawezi kukuelewa.
Hawana akili awajui kuwa hata kikwete angechukua nchi mara ya pili baada ya magufuli lazima angelazimika kupambana sana ili kufiti pengo la jpm ingembidi kutoka ikulu kuchapa kazi tifauti na hapo nyuma
 
Kwani Gwajima alisemaje kabla ya kugombea ubunge?
Hili gazeti liwekwe kwenye makumbusho ya taifa kwa ajili ya hadidu za rejea.
 
Hawana akili awajui kuwa hata kikwete angechukua nchi mara ya pili baada ya magufuli lazima angelazimika kupambana sana ili kufiti pengo la jpm ingembidi kutoka ikulu kuchapa kazi tifauti na hapo nyuma
Usimtaje kabisa huyu mtu wako na JPM kwenye sentensi moja :)
 
Dhaifu kwako hata kwenye mpira unapo poteza mchezaji bora lazima utafute mchezaji bora ,na huyo mchezaji lazima atatakiwa kufiti pengo la aliye ondoka ,mama mwenyewe alisema kazi aliyo achiwa na magufuli ni kubwa
Wewe ulikuwa unajua John Pombe Joseph Magufuli angekufa lini mpaka uone kuwa ndiyo alikuwa kila Kitu kwa Maendeleo ya Tanzania na kwamba Wengine ama wasingefaa au hawawezi kufanya makubwa zaidi yake?
 
That's a political language. Angesema: ^Sitagombea 2025,^ tungemwelewa!!! Leo hana wazo la kugombea; vipi wazo hilo likimjia kesho au keshokutwa, kama hili la ^ugaidi^ wa Mr Hai!???
Huyu hata mwaka hajamaliza keshaanza kuwaza uchaguzi 2025! Asije akawa mgombea pekee huyu!
 
Back
Top Bottom