Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,898
- 942
MKUTANO MKUU WA CCM JIMBO LA MUFINDI KUSINI
UWASILISHAJI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI (CCM) 2020 - 2023
Mbunge wa Mufindi Kusini ambeye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amekabidhi kontena lenye shehene yenye vifaa mbalimbali vya Hospitali ya Wilaya ya Mufindi vyenye thamani ya Tsh. bilioni 1.8 December 16,2023, vifaa hivyo ni misaada aliyoitafuta yeye mwenyewe kutoka nje ya Nchi.
Mhe. Kihenzile amegawa pia baiskeli kwa Watu wenye mahitaji maalumu katika Jimbo la Mufindi kusini na mitungi ya gesi kwa vikundi vya Mama lishe, mashine ya uzalishaji wa vifaranga zenye thamani ya Tsh. milioni 10, mashine ya kufyetulia matofali yenye thamani ya milioni 15 na amekabidhi pia vyerehani 10 vya kushonea kwa vikundi vya Wanawake pamoja na pikipiki 16 kwa kila Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Mufindi Kusini.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Wahusika na Mgeni rasmi kwenye hafla ya uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2023 Issa Gavu, katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Mufindi kusini uliofanyika katika viwanja vya Mbalamaziwa, vifaa hivyo vimewasili nchini wiki hii kutoka nje ya Nchi.
Katika hatua nyingine Wajumbe wa Mufindi kusini wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mbunge wao huyo kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na wamemshukuru Rais pia kwa kuidhinisha fedha za miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika jimbo la Mufindi Kusini.
Katika hatua nyingine, Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum mbele ya Mgeni Rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Issa Gavu wameadhimia kwa kauli Moja kumchangia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Fomu ya kugombea Urais Mwaka 2025 - 2030.
Aidha, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Issa Gavu amepokea Michango ya kila mjumbe na kila kata katika jimbo la Mufindi Kusini na kukamilisha Jumla ya Tsh. Milioni mbili laki mbili arobaini na Saba mia saba hamsini, (Tsh 2,247,750) za kumchukulia Fomu Ndg . Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais 2025 - 2030 kupitia tiketi ya CCM.
Attachments
-
GBfihgWW8AAAIEs.jpg93.2 KB · Views: 3
-
GBfihgVXIAE8NPn.jpg50.6 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-12-16 at 5.05.22 PM.jpeg38.2 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-12-16 at 5.05.23 PM (1).jpeg46.6 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-12-16 at 5.05.25 PM.jpeg52.5 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-12-16 at 5.05.26 PM.jpeg59.1 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-12-16 at 5.05.27 PM (1).jpeg52.3 KB · Views: 2