Shemsa Mohammed: CCM Haitambeba Mtu Katika Uchaguzi Mkuu Ujao, 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,081
1,004

Shemsa Mohammed: CCM Haitambeba Mtu Katika Uchaguzi Mkuu Ujao, 2025

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amesema chama hicho hakitambeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani na kuwa atabebwa kutokana na matokeo yake ya kukitumia chama hicho pamoja na wananchi.

Mohammed aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kichama mkoani humo ambayo inaendelea mkoa mzima wa ajili ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

"Chama chetu hakitarajii kuja kumbeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu bali kazi zake ndizo zitakazo mbeba," alisema Mohammed.

Alisema ziara hiyo ambayo inafanyika Tarafa kwa Tarafa na jana Aprili 20, 2024 walikuwa Tarafa ya Nung'hu Wilaya ya Maswa ambapo walifanya kikao cha ndani kilichuhudhuriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Kata, Matawi, Mashina, Mabalozi wa CCM, Wazee Maarufu, Viongozi wa Dini, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji,Kamati za Utekelezaji za Jumuiya zote ndani ya Chama.

Alisema kikao hicho kilienda sambamba na kusikiliza kero na changamoto za wananchi zilizoibuliwa na Viongozi hao ambapo Serikali ilizitolea ufafanuzi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.

Wananchi wa mkoa huo wametumia ziara hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi kwenye Sekta za Afya, Maji, Miundombinu, Elimu, Nishati yenye thamani ya zaidi Sh. Bilioni 4.01 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi April 2024.

WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.48.jpeg
 
Attachments

 • WhatsApp Video 2024-04-21 at 05.36.11.mp4
  69.5 MB
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.14.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.14.jpeg
  252.7 KB · Views: 5
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.22.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.22.jpeg
  386.6 KB · Views: 5
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.25.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.25.jpeg
  209.5 KB · Views: 6
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.20.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.20.jpeg
  457.3 KB · Views: 6
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.05.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.05.jpeg
  465.5 KB · Views: 4
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.43.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.43.jpeg
  393 KB · Views: 4
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.49.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.49.jpeg
  258 KB · Views: 4
 • WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.55.jpeg
  WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.55.jpeg
  322.2 KB · Views: 5
Hivyo ndivyo inavyotakiwa, hakuna kubebana. Wale wapuuzi wanaotaka yule mtalii wao apewe fomu ya peke yake hatutakubali sisi kama watanzania wazalendo.
 
Shemsa Mohammed: CCM Haitambeba Mtu Katika Uchaguzi Mkuu Ujao, 2025

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amesema chama hicho hakitambeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani na kuwa atabebwa kutokana na matokeo yake ya kukitumia chama hicho pamoja na wananchi.

Mohammed aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kichama mkoani humo ambayo inaendelea mkoa mzima wa ajili ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

"Chama chetu hakitarajii kuja kumbeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu bali kazi zake ndizo zitakazo mbeba," alisema Mohammed.

Alisema ziara hiyo ambayo inafanyika Tarafa kwa Tarafa na jana Aprili 20, 2024 walikuwa Tarafa ya Nung'hu Wilaya ya Maswa ambapo walifanya kikao cha ndani kilichuhudhuriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Kata, Matawi, Mashina, Mabalozi wa CCM, Wazee Maarufu, Viongozi wa Dini, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji,Kamati za Utekelezaji za Jumuiya zote ndani ya Chama.

Alisema kikao hicho kilienda sambamba na kusikiliza kero na changamoto za wananchi zilizoibuliwa na Viongozi hao ambapo Serikali ilizitolea ufafanuzi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.

Wananchi wa mkoa huo wametumia ziara hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi kwenye Sekta za Afya, Maji, Miundombinu, Elimu, Nishati yenye thamani ya zaidi Sh. Bilioni 4.01 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi April 2024.
Anataka kusema kwamba Polisi na TISS hawatahusishwa tena kwenye Operesheni za kupoka ushindi ili wagombea wa Chama chake cha Siasa watangazwe kwamba ni Washindi katika Uchaguzi wa Siasa ?
 
Anataka kusema kwamba Polisi na TISS hawatahusishwa tena kwenye Operesheni za kupoka za ushindi ili wagombea wa Chama chake cha Siasa watangwe kwamba ni Washindi katika Uchaguzi wa Siasa ?
Hapana, anamaanisha kwenye chaguzi za ndani za ccm, kwenye uchaguzi wa kitaifa vyombo vya Dola vitaendelea kuibeba ccm.
 
Shemsa Mohammed: CCM Haitambeba Mtu Katika Uchaguzi Mkuu Ujao, 2025

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amesema chama hicho hakitambeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani na kuwa atabebwa kutokana na matokeo yake ya kukitumia chama hicho pamoja na wananchi.

Mohammed aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kichama mkoani humo ambayo inaendelea mkoa mzima wa ajili ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

"Chama chetu hakitarajii kuja kumbeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu bali kazi zake ndizo zitakazo mbeba," alisema Mohammed.

Alisema ziara hiyo ambayo inafanyika Tarafa kwa Tarafa na jana Aprili 20, 2024 walikuwa Tarafa ya Nung'hu Wilaya ya Maswa ambapo walifanya kikao cha ndani kilichuhudhuriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Kata, Matawi, Mashina, Mabalozi wa CCM, Wazee Maarufu, Viongozi wa Dini, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji,Kamati za Utekelezaji za Jumuiya zote ndani ya Chama.

Alisema kikao hicho kilienda sambamba na kusikiliza kero na changamoto za wananchi zilizoibuliwa na Viongozi hao ambapo Serikali ilizitolea ufafanuzi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.

Wananchi wa mkoa huo wametumia ziara hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi kwenye Sekta za Afya, Maji, Miundombinu, Elimu, Nishati yenye thamani ya zaidi Sh. Bilioni 4.01 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi April 2024.

View attachment 2969683
Asante, na Amina. Yaani na iwe hivyo. Asibebwe mtu. Kazi yake imbebe
 
Na aseme kabisa hata samia hakuna kubebwa eti achapishiwe fomu yake peke yake.
 
Back
Top Bottom