Ila guys Barcelona ya zama hizi inaua sana vipaji vyake vya La masia kwa kukununua wachezaji mediocre sana wakati watoto wenye vipaji, utashi na DNA ya Barcelona wana waignore na kuwa demoralize huku wakiua potential, ability and talents za hawa madogo chipukizi.
Messi aliaminiwa sana na Rjikard licha ya umbo lake dogo na utoto wake na hakumuangusha na utoto wake ule ule bado aliwatia hat trick Real Madrid.
Sasa huyu Valverde yeye anamdharau sana dogo mmoja midfielder Fundi, mjanja mjanja, ana skills, touch, instinct na control ya world class ambayo Arthur hawezi kuipata, dogo huyu anaitwa Liqui Puiq ana miaka chini ya 18. Kwa kigezo kidogo kisicho na maana kwamba dogo ana mwili mdogo sana hivyo sio suitable kwake kucheza pale dimbani na kuminyana na midfielder majambazi wa box to box sababu bado hana physical strength.
Mungu anajua kuumbua sana wanafiki, mwezi wa 8 mwaka huu Barcelona walikutana na Ac Milan ya gattuso yenye midfielder wehu, majambazi wenye sumu na hasira muda wote bila sababu na dogo aliingia kipindi cha pili, alichozifanyia zile midfielder Gattuso mwenyewe baada ya mpira kuisha alipohojiwa hakuzungumzia lolote lile zaidi ya kutoficha mshangao wake kwa surprise ya dogo kuzichezesha kindumbwe ndumbwe midfielder zake muda wote wa mchezo na kubadilisha kabisa mchezo mzima bila Messi aliekuwa mapumziko baada ya world cup, Gattuso alisema dogo na umbo lake hilo dogo lakini anavyoufanya mpira miguuni mwake its pure work of art..its like poetry. Na sio siri siku hiyo alichakaza midfielder zote za Gattuso kwa pasi accuracy na skills za La Masia kabisa.
Nikadhani kwa yale madivataizi ya dogo labda atapewa priority ya kuanza first eleven ligi ikianza.. Lakini Hola! Ajabu anaanza Arthur anarusha mapumbu tu hana la maana analofanya uwanjani ukilinganisha na timu kubwa kama Barcelona yenye intensity na demand kubwa ya kumtaka player aadapt mapema zaidi mfumo wake na kujiadjust awe best.. For simple reason of playing along with the best. Arthur yeye anaadapt very slow na uwezo wake sio extraordinary kwa demand ya Barcelona labda Man U anaweza kufaa ila sio Barcelona.
Sasa unajiuliza kwanini Valverde asimpe nafasi mtoto Puig muda huu? Ambae amekubalika na midfielder katili kama Gattuso? Maana tatizo la Barcelona muda huu ni kukosa World class midfielder itakayomfanya Messi asiwe na task mbili kama sasa kufunga na kutoa pass za mwisho kama kiungo, apatikane kiungo anaejua kupiga killer pass na kufyonza mashambulizi ya wapinzani kwa kuboss midfield zone kama mtoto Puig ili king abaki na Kazi yake moja tu kuweka ngozi kambani na sisi mashabiki tumle muuza vodka wa 1xbet easily.
Kama kuna mchezaji Valvede anapaswa kumuamini sasa basi ni Riqui Puig.
Picha chini mtoto Puig akizichakaza midfielders za Gattuso ndani ya dakika 45 tu alizopewa.
Shukrani.
Nakala; aione Valverde
Maria batromeo
Lionel Messi
Luiq Puig