Duniani kote usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote. SGR tulitegemea kuwa kiama cha usafiri wa mabasi na malori, imeshindikana

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Duniani kote usafiri wa reli ndiyo usafiri wa bei rahisi sana kuliko usafiri mwingine wowote. Malengo makuu ya kuboresha usafiri huu kwa kiwango cha SGR yalikuwa:

~Trip moja ya treni ya mizigo ingaliweza kusafirisha mzigo wa sawa na semi-trailers za malori 500 kwa mara moja, kwa spidi ya 120 kph na kwa bei ya sawa na bure ukilinganisha na malori.

Yaani mzigo wa ukubwa huo wa semi trailer 500 ungeweza kuondolewa kutoka bandari yetu ya Dar es Salaam kila siku na kufikishwa Mwanza au Kigoma ndani ya masaa 10 au 12 tu. Hakungalikuwa tena na mrundikano wa mizigo pale bandari ya Dar es Salaam.

Hata hizo bandari kavu zilizoko mkoa wa Dar es Salaam zingalikosa kazi. Bandari kavu zingalijengwa Mwanza na Kigoma. Uchumi wa nchi ungepaa kwa kasi kubwa na ndani ya muda mfupi tungeifikia Singapore ambayo uchumi wake unategemea bandari tu.

Barabara zetu zingalidumu zaidi kwani usafiri wa malori unalifikia kiama chake. Hata hizo ajali lukuki za barabarani zinazosababishwa na malori haya katika njia hizi kuu zingalifikia tamati. Traffic police wetu wangetafutiwa kazi zingine.

~ Hivyo ndivyo ingalikuwa kwa usafirishaji wa abiria. Trip moja ya passenger train yenye urefu wa si chini ya kilomita 3 ingalikuwa sawa na mabasi yasiyopungua 500 na wangalisafirishwa kwa raha kwa spidi ya 170 kph.

Yaani kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza au Kigoma ni mwendo wa saa 7 tu, kwa bei ya chee ukilinganisha na mabasi ambayo nayo yalikuwa yafikie kiama chake kwa njia hizi kuu za uchumi wa nchi na kuokoa uharibifu wa barabara zetu na ajali lukuki za barabarani. Uchumi wa nchi ungalipaa na wananchi wangalipata furaha.

Bahati mbaya kabisa matarajio hayo ya wananchi yameshindikana kufikiwa. TRC imepanga nauli za train hizo za spidi kubwa kuwa mara tatu ya bei za usafiri wa mabasi. Kwa sasa mtu anasafiri kwa basi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa nauli ya Sh 55,000 hadi 65,000.

Hii ni nauli ya kupanda kwa mafuta kwa sababu ya Ukraine. Kabla ya hapo ilikuwa Shs 35,000 hadi 45,000 na tunategemea hiyo Ukraine itakapokwisha bei hizi zitarejea. Sasa TRC wamepanga ziwe Sh 150,000 kwani hadi Dodoma tu ni Sh 75,000. Yaani ni karibu sawa na nauli ya ndege. Hawa Waha na Wasukuma wetu kweli watazipanda hizo treni?

Bado TRC hawajatoa nauli za mabehewa ya mizigo. Kwa mantiki hiyo hiyo bei inayotarajiwa ni mara tatu ya bei ya kukodi lori la semi trailer. Hivyo tutegemee mambo kubaki kama kawa. Matajiri wa malori na mabasi wamekataa kufika kiama.

Wameshinda hiyo vita na inasemekana hata hizo treni za SGR zitaendeshwa na wafanya biashara binafsi kwa mtindo wa PPP (private public partnership)! Ni wajanja, wametupokonya SGR yetu tuliyoijenga na tunaendelea kuijenga kwa kodi zetu. Zingine tumekopa lakini tutazirejesha kwa kodi zetu.

Mapendekezo:
1. Nauli ya abiria kutoka Dar had Mwanza isizidi Sh 25,000 kwa economy class. Yaani isizidi nusu ya nauli ya basi. Hayo madaraja mengine mnaweza kuweka mnavyotaka. Hao wanaoishia njiani hususani Dodoma ziende kwa uhusiano huo wa umbali hadi Mwanza.

2. Behewa la mizigo bei yake isizidi theluthi moja ya bei ya kukodi lori.

3. Hakuna mantiki ya kuwa na tofauti ya nauli kati ya MGR inayotumia dizeli na SGR inayotumia umeme. Kwa vyovyote vile uendeshaji (running cost) ya ile ya umeme ni rahisi kuliko ile ya dizeli.

TRC lazima ijue kuwa jukumu lake ni kutoa huduma na si biashara ya kutaka kurejesha kile serikali imewekeza kwenye huo mradi wa SGR. Wanachotakiwa ni kukusanya tu pesa itakayowawezesha kulipa mishahara ya staff wao na mambo mengine ya uendeshaji.

 
Duniani kote usafiri wa reli ndiyo usafiri wa bei rahisi sana kuliko usafiri mwingine wowote. Malengo makuu ya kuboresha usafiri huu kwa kiwango cha SGR yalikuwa...
Kwa Sasa Serikali imeshikwa na wenye pesa na hata wenye mamlaka wako kwenye kundi la wenye pesa na ni wafanya biashara.

Kwa Kuwa wenye nguvu hao wamewekeza kwenye mabasi na malori, Kwa urahisi wameitumia akili Ndogo kwamba Usafiri wa Treni SGR uwe ni Bidhaa au huduma mbala wa Usafiri wa Ndege, wameondoa Ushindani wa SGR Kwa Usafiri wa barabara.

Kwa uchache tu
 
Wapi duniani usafiri wa treni ya haraka bei rahisi? Tupe mfano wa nchi 3 tu duniani?

Mtu uko Chato huko hata Dubai tu hujafika unaleta uongo wako hapa.
Hizi treni zetu ni za mwendo wa kawaida kwa ulimwengu wa leo. Hizo za enzi za Hitler tulizokuwa tunatumia, dunia ya sasa walisha achana nazo.

Treni ya maximum speed ya 160 kph (sawa na ya Noa) ndiyo ya kawaida tu. Hizo za maximum speed ya 40 kph kama zile tulizo nazo ni za dunia ya kale, na lengo letu ni kuzi phase out tutakapokamilisha ujenzi wa reli yenye geji inayotakiwa. Hatutakuwa tena na hiyo MGR maeneo ambako SGR imekamilika. MGR ya kwenda Kilimanjaro hadi Arusha ndiyo itakuwa ya mwisho kuwa phased out. Huu ndiyo ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Hizo za mwendo wa haraka unazosema zinaitwa bullet trains. Zinakimbia mwendo kasi wa kuanzia 350 kph hadi 650 kph. Yaani ni ndege za chini. Kwa speed hiyo kubwa nyingi zake huelea tu juu ya reli by magneto, hazina magurudumu - no friction energy loss. Zingine zinazungukwa na vacuum, yaani zinapaa ndani ya vacuum, hazipambani na upepo kama zile ndege za angani.

Zinavuta mabehewa machache sana, ni za abiria tu na ni kwa safari fupi fupi tu na hasa kama usafiri wa mijini. Sisi hatuna mpango wa kuleta treni za aina hiyo, kwanza hata hii SGR haina uwezo wa kuzipitisha (support). Hata huko ulaya na kwingineko ziko chache sana tu na zingine bado ziko kwenye majaribio/ utafiti - wanataka ziweze kukimbia kwa zaidi ya spidi ya 1,000 kph.
 
Bandari kavu Kigoma kwamba unapeleka makontena Goma pekee?
Yanapelekwa DRC ambayo ni nchi kubwa na tajiri kuliko nchi zote za Afrika. Ila utajiri wake unaporwa na mataifa mbalimbali ya dunia hii hadi nchi ya Rwanda, wamebaki wakipigana wenyewe kwa wenyewe!

Tunataka Kigoma iwe kama Dubai, kijografia iko kwenye strategic location. Hizi treni za kisasa zingaliwezesha hili. Hii ni vita ya kiuchumi. Mabepari wenye mabasi na malori kama wewe lazima watapinga hili.
 
Duniani kote usafiri wa reli ndiyo usafiri wa bei rahisi sana kuliko usafiri mwingine wowote. Malengo makuu ya kuboresha usafiri huu kwa kiwango cha SGR yalikuwa...

Dr Akili,

Tatizo lako kwenye mijadala unasema "Dunia kote" bila kuwa na data. Kwa nchi nyingi za EU bei ya ticket za treni ya mwendo kasi ni zaidi ya ticket za ndege.

Lakini lingine mfano usafiri wa malori sio mbaya inategemea nchi gani hata nchi za wenzetu mfano hapa US usafiri wa malori ni mkubwa sana kiasi kwamba kuna upungufu wa madereva.

Hii ni kwasababu ya kuongezeka kwa mitandao na watu kununua vitu mitandaoni. Hivyo sio kweli inabidi tutengeneze barabara zetu vizuri bado na hii reli sana sana itapunguza tu mizigo sio kumaliza
 
Kwa mantiki hii, huu mradi tayari ni white elephant.........maana umetumia pesa nyingi za nchi hadi tunakopa kama tumepagawa vile na bado hauna msaada wowote kwa wananchi walio wengi, hopeless!!
Tatizo ni wananchi na si mradi.
Mnapenda vya dezo mno
 
Tatizo ni wananchi na si mradi.
Mnapenda vya dezo mno
Vya dezo kwa lipi? Kwani hiyo SGR na hizo treni zimegharimiwa na nani?

Kwa taarifa yako huo mradi ni wa wananchi wote wa Tanzania. Wao ndiyo wameugharimikia na wataendelea kuugharimia kupitia kodi zao.

Si mali ya hao wajanja wachache pekee yao. Wananchi ndiyo wenye mamlaka ya kupanga hiyo nauli ya treni yao na siyo hao akina Kadogosa, Mbawala na wafanya biashara za mabasi na malori.
 
Back
Top Bottom