Tunawataka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhi (LATRA) wasitishe mara moja, tangazo lao la kupandisha nauli za mabasi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Sisi wananchi wa nchi hii tunawataka, mamlaka ya Udhibiti usafiri wa Ardhi (LATRA) wasitishe mara moja, tangazo lao la kupandisha nauli, ambalo wao walisema zitaanza rasmi kesho kutwa, terehe 8 mwezi huu

Nimesema sisi watanzania, tunawataka hao LATRA wasitishe mara moja, tangazo lao, Kwa kuwa Kwa mujibu wa maelezo yao, walisema, wameidhinisha ongezeko Hilo, kutokana na ombi la wamiliki wa mabasi, kutokana na ongezeko la bei ya mafuta duniani

Hata hivyo njia ya mwongo ni fupi, kabla ya hata hayo makampuni ya mabasi hayajaanza kupandisha nauli hizo,kama walivyoidhinishiwa na hao LATRA, bei mpya ya mwezi huu wa Desemba, zilizoanza kutumika Leo, zinaonyesha kushuka sana, Kwa bei hizo za mafuta!

Kwa mfano hapa jijini Dar, ambapo petroli ilikuwa ikiuzwa Kwa shilingi 3,274 Kwa Lita, hivi sasa bidhaa hiyo imeshuka sana hadi kufikia shilingi 3,150 Kwa Lita!

Kwa kuwa hao LATRA walitwambia kuwa sababu kuu ya kukubali, hao wamiliki wa mabasi waendelee kutukamua sisi wananchi, ni kutokana na kupanda bei za mafuta, na Kwa kuwa bei hizo sasa zimeshuka sana, sioni sababu zozote za kuendelea kutugandamiza sisi wananchi, Kwa kuendelea kutubebesha huo mzigo wa upandishaji wa nauli.

Ndiyo maana nasisitiza sana, hao LATRA watangaze kusitisha tangazo lao la upandishaji wa nauli za mabasi mara moja.

Pia soma > LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
 
Back
Top Bottom