Masanja Kadogosa: Kukatika kwa umeme hakutakwamisha utendaji wa Reli ya SGR

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Mkurugenzi wa Shirikla la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa wakati anazungumza na kutoa maelekezo kabla ya safari ya kutokea Dar - Moro mapema leo, Februari 26, 2024.
Snapinsta.app_429907418_795767822590947_4582168767238296139_n_1080.jpg

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza majaribio ya Treni ya Umeme ya Kisasa ya (SGR) kutoka Mkoani Dar es Salaam hadi Morogoro huku ikielezwa kuwa Huduma rasmi za Usafiri huo zinatarajiwa kuanza Mwezi wa Julai, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TCR), Masanja Kadogosa amewataka Wananchi waondoe hofu kuhusu tatizo la kukata umeme katika safari za treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kuwa reli hiyo ina mkondo wa umeme unaojitegemea.

Kadogosa amesema hayo Februari 26, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa safari ya majaribio ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

"Tuna mkondo unaojitegemea kwa ajili ya reli tu, hatuingiliani na mtu yeyote, na mkondo huo umeunganishwa kwenye gridi kubwa na vyanzo vyote vya umeme ndani ya nchi hii," amesema Kadogosa.

Pia, amesema kuunganishwa kwa reli hiyo katika vyanzo vyote vya umeme vilivyoko nchini ni tafsiri kwamba haiwezi kukwama kwa sababu ya kukatika umeme.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom