Tatizo kubwa la treni zetu sio spidi ndogo bali uendeshaji, mabasi ya mwendokasi yatupe funzo.

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,625
46,270
Kauli ya Waziri Mbarawa kwamba treni yetu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu sio ya mwendokasi imeibua taharuki na kelele nyingi sana kutoka kwa raia wengi wakiona kama wamechezewa mchezo wa kijanja wa karata tatu.

Pamoja na haya yote lazima tufahamu chanzo cha matatizo ya sekta ya reli Tanzania sio hasa spidi. Reli za TAZARA, kati na Kaskazini zimekuwa katika hali mbaya kwa sababu kukosekana management nzuri ya uendeshaji.

Hiyo SGR hata kama itatumia nusu tu ya muda wa mabasi katika safari yake inatosha sana kukidhi mahitaji ikiwa itaendeshwa kwa ufanisi yani tiketi ziwe zinapatikana bila usumbufu na bei sawa na mabasi, muda utazingatiwa, usafi utakuwepo, usalama wa mizigo utakuwepo na hakutafanyika uharibifu wa mabewa yake na miondombinu mengine.

Tofauti na hapo SGR hata kama ingekuwa bullet bado tu itageuka kuwa kama mradi wa mabasi ya mwendokasi au shirika la ATCL. Kuna watu wengi sasa hivi wanaona ni bora dalala za kawaida kuliko huo usafiri wa yanayoitwa mabasi ya mwendokasi, tujifunze kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom