Labda waingie mitini kutokana na ubishi wenu kwa sababu ni kazi ngumu kujaribu kumuelewesha mtu kitu asichokielewa ilhali ametangulia kupinga hicho kitu asichokielewa.
Sasa mtu anatumia zile imani potofu za watu zenye kuhusishwa na uchawi na kusema hakuna uchawi ni imani potofu tu za watu kushindwa kuelewa mambo yalivyo, utafikiri imani potofu huwa zipo kwenye kwenye uchawi tu.
mimi binafsi hadi leo hii sijawahi kushuhudia mtu anayejitambulisha kuwa ni mchawi na akawa anaeleza mambo yenye kuwahusu wachawi na uchawi wao.
naam, basi tusubiri watu wanaojitambulisha wachawi, au walioujua uchawi waje tuone maelezo yao mkuu, ili mambo yasiwe mengi
kwasababu story zilizopo ni za kusikia kama tunavyosikia hapa kwa mdau mtoa mada
story za kusikika miongozni mwao ndo hizo za kusababishia watu matatizo/magonjwa nk, hapo tukiwa tunauliza unafanyaje kazi lengo lake ni kuangalia mfano mkoloni kaja na bunduki nini kilishindikana kuwapiga magonjwa au kuwatoa akili wawe mazezeta wakoloni
wengine wanasema zinaleta pesa, mali nk au hata mtu tunaweza sema akaingia nyumbani kwa mtu kwa njia zisizo za kawaida sasa njia hii haiwezi tumika kwenda kuchukua hata madini au fedha madukani? zikatumika kujitajirisha?
sasa ukiuliza maswali kama haya wanasema hivyo sio uchawi unavyopiga kazi --- sasa watupe namna ulivyo na unapigaje kazi ili tupime upya tuachane na story za kusikia,
mwisho wa siku kama hapo mtoa mada kasema kasoma vitabu kama vinne, wadau wameomba avitume au hata aweke majina --- mpaka muda huu jambo hilo halijafanyika na anasema ni vitabu vya hatari
sasa kwa muktadha huo kwanini tusiendelee kutumia story zinazovuma tu huku mtaani mkuu?
mada za hivi karibu kila siku zinaishia kwa kutokukubaliana, hapa karibuni at least ule uzi wa yule jama aalienda kwao tanga "alsisi" niliishia mwanzomwazo tu sjui nini kiiendelea ila alikua anajaribu kueleza matukio mbalimbali kwamba huyo jamaa anaweza mwambia hata mambo ya mbele, watu wakawa wanamuuliza mambo ya uchaguzi 2025 utakuaje naye sidhani kama alikua anajibu kwenye sekta hiyo.
so mwisho wa siku watu wanataka kitu cha kutesti