Hoja yake haipo kwenye maana, hoja ipo kwenye mechanism ya utendaji kazi huo uchawi.
Mtu kama anaweza kupotea na kwenda popote kwa sekunde bila kuonekana, then hatutegemei mtu huyu awe ana lala njaa kwake.
Kuna stori kwamba wachawi wanakuja night kali kuloga kupitia kuta za nyumba, mezani unaweza kuwa umeacha kibunda cha maana na wakati huo wao makwao maisha magumu wamepika mlenda, lakini wao wanakuja kukukaba na kukukanda kanda na matako yao then wanasepa.
Ukiuliza watu wanaoamini hizi stori za uchawi wanakuambia kwenye ulimwengu wa kichawi pesa haina thamani ndio maana mchawi hachukui hizo hela.
Lakini mchawi huyo huyo aliyeacha hicho kibunda mezani kwako, eti anakuja kukuibia tena kwenye duka lako kupitia chuma ulete.
Na at the same time unaweza kutana na story kuwa fulani kanunua uchawi.
Sasa hapa mnatuacha njia panda. Hatujui ni muda gani katika ulimwengu wa kichawi pesa inakuwa na thamani na muda gani pesa ni hitaji la lazima.