min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 47,643
- 131,590
Sio wazee tu hawa wanyama kama paka mbwa na wanyama pori wanajua kwa trial & errorHivi zamani huko kabla ya sayansi wazee waliwezaje kujua mimea tiba na magonjwa yanayotibu?
Sio wazee tu hawa wanyama kama paka mbwa na wanyama pori wanajua kwa trial & errorHivi zamani huko kabla ya sayansi wazee waliwezaje kujua mimea tiba na magonjwa yanayotibu?
ElezaPia tunaweza kueleza yenye kuchukiza pia kutoka huko kwenye sekta ya afya, usiangalie mambo kwa upande mmoja tu.
Kwa sababu unahisi nilichokuuliza ndio ulichojibu kumbe sivyo, ila acha nisikuchoshe.Kupinga au kubishania uthibitisho uliopo ni jambo moja, kutokuwepo uthibitisho ni jambo lingine kabisa. Wanaopinga uthibitisho wa kisayansi mfano Dunia kuwa duara (flat earthers), HIV kusababisha AIDS au uthabiti wa chanjo(anti-vaxxers) hao wanawekwa kwenye kundi la conspiracy theorists na pseudoscientists.
Kwenye Science Kuna
Natural Science
Social sciences
Archaeological science
Astronomy
Kwenye History kuna "scientific methods" za dating, Paleontology, forensic document examination n.k
Halafu unachosha sasa na maswali yako ambayo ulipaswa uwe unayafahamu wakati unamaliza kidato cha nne.
Tukileta hayo makisio ya uchawi si ndio huwa mnasema ni mambo tu tusiyoyajua ila sio uchawi?Leta makisio au uthibitisho wa uchawi na uganga tuubishanie.
ChaiHabarini wakuu
Leo nimeona nikumbuke matukio niliyoyashuhudia ambayo yananiweka mdomo wazi na sijui nilikuwa nawaza nini(nitabase zaid upande wa kiroho)
Kwanza kabisa mimi ni aina ile ya watu ambao tunataka kujua kila kitu hata kama ni vya hatari ila nitajilazimisha nijue tu.
MImi ni mkatoriki ila sikua nyuma sana kuna kipindi niliamua kulivalia njuga swala la dini na kuchimba kidogo juu ya imani kwa ujumla na kupata mwanga fulani kuhusu imani niliyopo hasa swala la kuitwa wakatorik tunaabudu sanamu, ukweli ni kwamba hatuabudu sanamu ila kuna gap dogo sana ukiteleza kidogo utaangukia kwenye kuabudu sanamu
Maisha yakaenda mm kama binadamu nilipitia mapito fulani kimaisha nikayumba kiuchumi..nilijaribu kutatua changamoto zangu mwisho wa siku nikaangukia kwenye mambo ya waganga..uganga kweli upo na somehow unafanya kazi na matokeo yanaonekana japo fix zipo nyingi sana (kila mganga atakuambia hii dawa ninayokupa mtu akikugusa tu anakwenda na maji)
Nafsi yangu ilikuwa inagoma sana kuamini mambo ya kiganga na uchawi ila ndo hivyo tena maji yalikua yanaifika shingoni nikawa najikuta tu naenda kupata msaada
SIku moja nilikaa nikajiuliza kwanini naenda kwa mganga na huko kwa mganga natajiwa jina la mungu, nikaona ngoja niuchimbe kwanza huo uganga na uchawi unafanyaje kazi na kwanini upo
Nilifanikiwa kusoma vitabu vinne vya uchawi na uganga (jina kapuni kwasababu ni vya hatari kidogo)
Ndani yake nilifunguka kiakili sana nikaja kugundua uganga ama uchawi kwanza kabisa unaanza na wewe kuwa na imani ya hicho unachokifanya
Pili ni lazima kuwe na roho ambayo inakupa muongozo wa nini cha kufanya ili kufanikisha jambo lako
mtu ili kuwa mchawi kwa level wa chini kabisa inaweza kumchukua wiki tatu mpaka miezi 18 mpaka kuweza kufanya mambo ambayo yapo kinyume na mungu japo hivyo vitabu vinaita hiyo ni elimu safi na tuitumie kwa wema
TAtu. Uchawi ama uganga ni lazima uende kinyume na muumba hata kama majina yanayotamkwa ni ya muumba ila pale yanatamkwa kama dhihaka tu na hilo ndio lengo kuu ili uchawi uweze kufanya kazi
Uchawi unahusisha zaidi matumizi ya alama hasa nyota,duara na pembe, ukimaliziwa na maneno maalumu ili kuipa nguvu pamoja na imani ya kwamba unachokitamka kinakwenda kutokea
Matumizi ya vitu kama chumvi, hirizi,talasin ni mabaya sana kwasababu yanakufa uhisi nguvu inatoka kwenye hivyo vitu na sio muumba(mnaoshauriana kutumia chumvi ili kujikinga ama kusafisha nyota naomba mnisamehe bure)
NIliyoyashuhudia kwenye hiyo elimu ni makubwa sana na yalinifanya niujue ulimwengu na kujikita zaidi kwa muumba wangu na kuachana kabisa na hizo imani
Nguvu za giza zipo ila zile ni njia za mkato tu ambazo zinampumbaza mwanadamu na kumpeleka shimoni, ukiingia huko lazma upotee tu iwe kwa kujua ama kutokujua
Dunia ina mengi sana na mimi sio mwandishi mzuri wa magazeti hivyo naishia hapa kukiwa na swali lolote nitajitahidi kulijibu ama nikishindwa nitasaidiwa na mliopo humu
😂😂😂😂😂😂😂😂😂Siwezi kuacha tunguli
Una amini kuhusu Mungu?Uchawi ungekuwepo kweli na ungekuwa unafanya kazi kweli, Africa ingekuwa bara tajiri sana.
Kila mwafrika angetajirika kupitia huo uchawi.
Uchawi siku zote una aminiwa na watu wajinga na watu duni maskini.
Sijakuuliza kama mie mchawi au sio mchawi, nimeuliza mchawi ni nani?Wala usiende mbali, Wewe mwenyewe mchawi /mshirikina, mleta uzi naye pia mchawi
Ni kama vileVp kuhusu bahati mbaya?
Kwa sababu ni makisio dhaifu sana , makisio ya historia na evolution watu wanayosoma wanayafanyia utafiti na bado wanaacha mlango wazi kwa mawazo mbadala ukosoaji na hata kurekebisha ikibidi, sio kama nyie wachawi ambao tayari mmeshafikia conclusion na ni experiences zenu binafsi tu.Tukileta hayo makisio ya uchawi si ndio huwa mnasema ni mambo tu tusiyoyajua ila sio uchawi?
nadhani alisema inafanya vizuri, sio ipo vizuri --- nchi tajir hizo kukua kiuchumi mara nyingi zinakua kwa asilimia ndogo ukilinganisha za kwetu kwa indicators zilizopo bongo ilikua na asilimia nyingi so ni sahihiKwani wewe ulikubali aliposema Tanzania ipo vizuri kiuchumi kushinda Marekani?
nisaidie hapo pm nduguSiwez weka public mtu kama anataka aje pm nitatoa vile basic kwanza
zipo pia ni chances tu yani leo hii mtoto akizaliwa gaza hapo baada ya miaka mi5 kina netany wakipiga bomu, imagine kuna wadau wengi sana duniani wanafurahia, ila ukizaliwa hapa bongo probability ya kukumbana na bomu ni almost haipoVp kuhusu bahati mbaya?
Shida ni kushindwa kuelewa kwamba kuna mchawi na kuna uchawi, hao ambao sijui wanaingia nyumba za watu kimazingara ni wachawi na ndio nasema sijawahi kuona mtu akijitambulisha mchawi akaeleza hayo mambo yao ya kichawi hata humu hutoona akija mtu aseme yeye ni mchawi na kuanza kujielezea.naam, basi tusubiri watu wanaojitambulisha wachawi, au walioujua uchawi waje tuone maelezo yao mkuu, ili mambo yasiwe mengi
kwasababu story zilizopo ni za kusikia kama tunavyosikia hapa kwa mdau mtoa mada
story za kusikika miongozni mwao ndo hizo za kusababishia watu matatizo/magonjwa nk, hapo tukiwa tunauliza unafanyaje kazi lengo lake ni kuangalia mfano mkoloni kaja na bunduki nini kilishindikana kuwapiga magonjwa au kuwatoa akili wawe mazezeta wakoloni
wengine wanasema zinaleta pesa, mali nk au hata mtu tunaweza sema akaingia nyumbani kwa mtu kwa njia zisizo za kawaida sasa njia hii haiwezi tumika kwenda kuchukua hata madini au fedha madukani? zikatumika kujitajirisha?
sasa ukiuliza maswali kama haya wanasema hivyo sio uchawi unavyopiga kazi --- sasa watupe namna ulivyo na unapigaje kazi ili tupime upya tuachane na story za kusikia,
mwisho wa siku kama hapo mtoa mada kasema kasoma vitabu kama vinne, wadau wameomba avitume au hata aweke majina --- mpaka muda huu jambo hilo halijafanyika na anasema ni vitabu vya hatari
sasa kwa muktadha huo kwanini tusiendelee kutumia story zinazovuma tu huku mtaani mkuu?
mada za hivi karibu kila siku zinaishia kwa kutokukubaliana, hapa karibuni at least ule uzi wa yule jama aalienda kwao tanga "alsisi" niliishia mwanzomwazo tu sjui nini kiiendelea ila alikua anajaribu kueleza matukio mbalimbali kwamba huyo jamaa anaweza mwambia hata mambo ya mbele, watu wakawa wanamuuliza mambo ya uchaguzi 2025 utakuaje naye sidhani kama alikua anajibu kwenye sekta hiyo.
so mwisho wa siku watu wanataka kitu cha kutesti
Mtu kusema uchawi haupo pengine ni kutokana na taarifa alizonazo za masimulizi ya huo uchawi.Umeeleza sawa sawia kabisa.
Sasa mtu amekuja humu akaeleza kwamba uchawi hakuna na akatoa hoja kwamba uchawi ungekuwepo basi afrika ingekuwa tajiri? Unamuuliza ki vp afrika ingekuwa tajiri kama uchawi ungekuwepo?
Hapo hapo haujaeleza kitu chochote chenye kupingana na maelezo yake wala hakuna ulichompinga, ila mtu badala ajibu anaanza kukuuliza definition ya uchawi? Wakati swali aliloulizwa halipo tofauti na huo muktadha tunao ukusudia.
Mwengine anasema uganga hauna nguvu yeyote, ni kwamba waganga wanacheza tu na akili za mtu. Unamuuliza vp mganga anaweza kucheza na akili yangu endapo mimi nikienda kwake mganga na kutaka huyo mganga amfanyie mtu uchawi yani amroge mtu mwengine?
Mtu anakuja kukuuliza kuroga ndio nini? Uchawi ndio nini?
Sasa ni vyema mtu mwenyewe ukaeleza mie najua definition hii ya neno uchawi, kuliko kudhani mtu mwengine hajakuelewa na kuanza kumtaka akupe definition ya uchawi, matokeo yake mnaweza mkaanza kubishana kuhusu definition tena.
Kwa nini siku hizi baada ya smartphones kuwa nyingi na nyumba nyingi mjini kuwa na CCTV cameras hakuna tena zile habari za wachawi kuanguka kutoka angani kwa ungo, habari zilizokuwa zinatoka kila siku kwenye magazeti ya Shigongo??Shida ni kushindwa kuelewa kwamba kuna mchawi na kuna uchawi, hao ambao sijui wanaingia nyumba za watu kimazingara ni wachawi na ndio nasema sijawahi kuona mtu akijitambulisha mchawi akaeleza hayo mambo yao ya kichawi hata humu hutoona akija mtu aseme yeye ni mchawi na kuanza kujielezea.
Navyoelewa mie uchawi yeyote anaweza kuufanya maana ni ujuzi tu wa kujua ukifanya hivi na vile inapatikana athari gani, lakini mchawi kabisa tunakuwa tunazungumzia kitu chengine.
Halafu mkuu sijui kwanini umeshikilia sana hilo suala sijui wakoloni na kuiba bank, unachokifanya ni kukataa yale matukio yenye kuhusishwa na uchawi iwe wizi, kupata mali au kusababisha madhara kwa hoja ya kwamba ni story tu hazina ushahidi halafu unaenda kuchagua matukio ambayo hujawahi kusikia yakifanyika yakihusishwa na uchawi ndio unataka et hayo matukio kuwa ndio ushahidi wa kutokuwepo uchawi hii mie inanishangaza kwa kweli kwa sababu haueleweki unatafuta ukweli wa uchawi au ufanisi ama nguvu ya uchawi?
Kwa sababu hata sasa wapo watu wanaamini uchawi ila yapo mambo ambayo hawaamini kama huwezekana kwa njia ya uchawi.
Uchawi ungekuwepo kweli na ungekuwa unafanya kazi kweli, Africa ingekuwa bara tajiri sana.
Kila mwafrika angetajirika kupitia huo uchawi.
Uchawi siku zote una aminiwa na watu wajinga na watu duni maskini.
Siamini kwenye kuamini.Una amini kuhusu Mungu?
Ni sahihi kusema kwamba neno bahati hutumika kumaanisha kukosa ujuzi wa kujua sababu za hayo matukio kutokea kwa namna yalivyotokea au yanavyotokea?zipo pia ni chances tu yani leo hii mtoto akizaliwa gaza hapo baada ya miaka mi5 kina netany wakipiga bomu, imagine kuna wadau wengi sana duniani wanafurahia, ila ukizaliwa hapa bongo probability ya kukumbana na bomu ni almost haipo
hapo naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi chake, kwa sababu wote tunataka kuwasikia hao wachawi ila inakua ngumu.Shida ni kushindwa kuelewa kwamba kuna mchawi na kuna uchawi, hao ambao sijui wanaingia nyumba za watu kimazingara ni wachawi na ndio nasema sijawahi kuona mtu akijitambulisha mchawi akaeleza hayo mambo yao ya kichawi hata humu hutoona akija mtu aseme yeye ni mchawi na kuanza kujielezea.
Navyoelewa mie uchawi yeyote anaweza kuufanya maana ni ujuzi tu wa kujua ukifanya hivi na vile inapatikana athari gani, lakini mchawi kabisa tunakuwa tunazungumzia kitu chengine.
dhana ya ukoloni binafsi unaweza sema ndo kipimo changu cha juu sana kwa story za uchawi , kama tunaweza kukubaliana mtu anaweza tumia uchawi akamdhuru mtu mtu, akafanya aumwe, arukwe na akili, afe hapa afrika sidhani kama tungehitajika kubeba bunduki kupambana na mkoloni au wala tungehitaji kwenda UN kuomba uhuru wala kumuomba malkia uhuru --- magavana wa kikoloni wale na wanajeshi wao wangekua wanapigwa kipapai tu kweisha habari yao, sasa hapa hua kuna mgogoro kwa kua tunaambiwa haufanyi kazi katika namna hii --- na ukiuliza sasa unafanya kazi vipi , wanaoleta story za uchawi mara nyingi wanakimbiaHalafu mkuu sijui kwanini umeshikilia sana hilo suala sijui wakoloni na kuiba bank, unachokifanya ni kukataa yale matukio yenye kuhusishwa na uchawi iwe wizi, kupata mali au kusababisha madhara kwa hoja ya kwamba ni story tu hazina ushahidi halafu unaenda kuchagua matukio ambayo hujawahi kusikia yakifanyika yakihusishwa na uchawi ndio unataka et hayo matukio kuwa ndio ushahidi wa kutokuwepo uchawi hii mie inanishangaza kwa kweli kwa sababu haueleweki unatafuta ukweli wa uchawi au ufanisi ama nguvu ya uchawi?