Darasa: Maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika!

Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania...
Mimi binafsi huwa napingana na maswali ya walimu wanao uliza watoto maswali eti, tanzania ilipata uhuru wake 9.12.1961 hili si swali sahihi kwa wanafunzi
 
Tunajua kubwa Tanganyika ilipata uhuru 09/12/1961 kabla ya Tanzania kuzaliwa! Tanzania ilizaliwa 26.04.1964 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Je tarehe 09/12/ kila mwaka tunasherekia siku ya uhuru wa Tanganyika au Tanzania? Karibuni
 
TANGANYIKA
Ila sielewi serikali yetu ni nini inajitahidi kutuaminisha au ni nini wanajitahidi kukificha kwa hali na mali
Ugumu ni jina au sifa ya jina
Je wakisema Tanganyika ni kipi kinapungua napenda kujifunza hapa, na jee Tanzania ilizaliwa 9/12? Lipi tulishike?
 
Tanzania haikuwepo mwaka 1961 kwa kuwa ni matokeo ya muungano wa nchi mbili huru - Tanganyika na Zanzibar. Kwahiyo uhuru wa Tanzania haupo. Hata nchi ya kufikirika iitwayo Tanzania Bara haijawahi kupata uhuru kwa kuwa haikuwepo na hata sasa haipo!
 
Jina la Ubatizo ni TANZANIA sio TANGANYIKA.

Kwani Tanganyika alibatizwa kuwa Tanzania tarehe ya leo???

Kwani hata hiyo Tanzania mnayong'ang'ana nayo haina miaka 60. Mjitafakari

Siku ikifika kusheherekea ya miaka 60 ya Muungano na si uhuru mtakuja sema nini??

Mkumbuke Tanzania ni zao la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na haijawahi kutawaliwa.
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania, yaani Tanzanian National Day, na sio Tanganyika. Kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika lakini maadhimisho na sherehe ni ya uhuru wa Tanzania...
Hivi kwanini mwaka wa ngapi huu hwajakuteua?Au unalipwa hivi hivi.
 
Mkuu Mti wa Muwese, The Palm Tree , huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania, wewe ukiwemo, halafu mkiambiwa ukweli mna uwezo finyu wa uelewa, mnakasirika...
Nakubaliana nawewe kwa asilimia 100 kwamba mfano wako ni wakitoto kwa level za chekechea........ mind you that hapa ni JF tunataka FACT

Ziliungana nchi mbili na hakuna nchi jike wala nchi dume........ ni nchi mbili Tanganyika na Zanzibar

Kwa muktadha huo, sasa ni kwanini uhuru wa Zanzibar sio uhuru wa Tanzania bali uhuru wa Tanganyika ndio uwe uhuru wa Tanzania?

Mkija na hoja zenye mashiko hata kama hamna FACT basi angalau mje na hoja shawishi tunaweza kuwaelewa lakini sio kuja na hoja mifano ya ndoa za bint pasco

Kama tatizo ni jina Tanganyika angalau basi lingetumika jina Tanzania Bara ili kuhalalisha kwamba Tanganyika “alikufa”
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania...
Vipi kuhusu upande wa pili Zanzibar, Je wao leo sherehe inawahusu? Na vipi kuhusu Mapinduzi day yao huwa kuna recognition ipi? Bwana Pasi kutokana na michanganuo yako ya miwese fafanua kuhusu 26 April Muungano day....

Kwa.hiyo Tanganyika ndio aliolewa na Zenj ama vice versa.?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Pascal Mayalla ufafanuzi wako tafadhali
 
9th December mnaazisha nini

Uhuru wa Tanganyika
Nenda katafute kwenye kumbukumbu zako Tanzania ilitawaliwa na nchi gani?
Mwaka upi mpaka mwaka upi?

Haya mambo ya kujionea aibu ndo maana Tanganyika huwa haina muda wa kujadili mambo yake binafsi na wala haina bajeti yake.

Wakati huo kuna mambo yasiyo ya Muungano na hujawahi kusikia Wabunge wa Zanzibar wamemaliza kujadili mambo ya Tanzania wametoka ili Watanganyika wajadili yao. Na kwa bajeti ipi?

Mambo yamefinyangwa finyangwa tukiulizana watu wanakua wakali, Muungano usiguswe. Tuache kuficha uhalisia.

Ukitamka Tanzania =Tanganyika + Zanzibar.
Na kila mtu ilitawaliwa kivyake na kupata uhuru kivyake.
 
Mkuu kwa hiyo leo tunasherehekea uhuru wa Tanzania (Tanganyika isiyokuwepo) alafu very soon next January tutasherehekea uhuru wa Zanzibar??
Si ndiyo?

Je, wewe unaona sawa tu??
Ina utata sana. Sherehe kubwa kabisa ingepaswa kuwa Muungano. Otherwise Tanganyika iwepo sawia na Zanzibar
 
Kama vile nakupata kabisa ...kuna mantiki hapa

Back
Top Bottom