Darasa: Maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika!

Elimu yetu huenda inatupunguzia uwezo wetu wa asili wa kufikiri. Maana pamoja na elimu kusifika, maprofesa kuongezeka tumeshindwa kama taifa kutambua Uhuru 9/12/1961 ni kipande cha Nchi ya Tanzania yaani Tanganyika.
 
Happy Birthday Tanzania.
Miaka 60 sio mchezo....tumefanya mengi mazuri na kazi bado inaendelea.
tunafahamu kuwa maendeleo sio kama vile kujaza maji kwenye ndoo......bali maendeleo ni jambo endelevu.........kazi iendeleee....
Tungepata viongozi wanaofikiri tungekuwa mbali zaidi.
Norway,China,india, malaysia, indonesia tulilingana nao,wao walipata viongozi wanaofikiri wapo mara mia mbele yetu
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania...
Hichi ulichoandika kimejaa upotoshaji mkubwa. Kuweka kumbukumbu sawa hapa JF.

1. Tanzania ni taifa lililoundwa mwaka 1964, umri wa taifa hili mpaka sasa ni miaka 57. Hivyo haliwezi kusherekea tukio la miaka 60 iliyopita likiwa kama taifa.

2. Tanzania haikuwahi kuwa koloni la taifa lolote, hivyo haiwezi kusheherekea kumbukumbu ya uhuru wake.

3. Tanzania ni muungano wa mataifa mawili tofauti (Tanganyika na Zanzibar) yenye historia tofauti sana za kupata uhuru wake. Tanganyika ilipata Uhuru wake kutokea kwa muingereza mwaka 1961 na Zanzibar ilipata 'uhuru' wake kwa njia ya mapinduzi kutoka kwa utawala wa sultan kutoka Oman mwaka 1964. Huwezi kuziweka pamoja hizo nchi mbili kihistoria unapozungumzia suala la kupata Uhuru.

4. Nchi ya Tanganyika ndio ilipata Uhuru wake tarehe 9 ya mwezi Desemba, 1961, na ndio ingepaswa kusheherekea kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wake leo.
 
Mdogo wangu Paschal nimeona unaungana na hoja ya Uhuru wa Tanzania SIYO Tanganyika. Naomba utusaidie kujua mambo yafutayo;

1. 9/12/1961 kulikuwepo na Tanzania?

2. Je Tanganyika au Tanzania Bara imewahi kubadili jina ikajiita Tanzania? If yes,lini na kwa hati gani?

3. Tukisema Uhuru wa Tanzania tunamaanisha hata Zanzibar walipata Uhuru wao 9/12/1961?

4. Kama Zanzibar inatarehe yake yakupata Uhuru ambayo naamini ni siku ya Mapinduzi, tunasemaje Tanzania ilipata Uhuru mwaka 1961 tukijua kilichopata Uhuru ni sehemu tu ya Tanzania ambayo ni Tanganyika?

5. Kwa uelewa wako Mapinduzi ya Zanzibar yanaweza kutambua kama siku ya Uhuru ya Zanzibar?

6. Hoja Yako ya kusherekea ya Sasa ( present) umeitoa kwenye nyaraka gani?

Nauliza haya baada ya kuona mada zako zote zimeacha lakuna kwenye maeneo hayo: Nikutakie siku njema ya Uhuru wa Watanganyika
Kwa Mtazamao wangu mimi leo ni kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika mengine ni siasa tu, Dec 9 1961 hakuwa na Nchi inayoitwa Tanzania Bara.
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania, yaani Tanzanian National Day, na sio Tanganyika. Kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika lakini maadhimisho na sherehe ni ya uhuru wa Tanzania!.

Kufuatia baadhi ya watu kuwa kwenye sintofahamu ni maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ama Tanzania?.

Hivyo nimejitolea kutoa somo hili ambalo naamini litakuwa ni very benefisho kwako.


Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.
Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.
Paskali
Ila Paskali 🤣🤣🤣
 
Mambo mengine ni kujiaibisha na kujishushia hadhi ya mtu kwenye jamii. Mambo mengine yako wazi na yaki kwenye kumbukumbu za maandishi na hakuna siku tuliyosikia kubadilika kwa kilichokuwepo tangu mwanzo.

Katika historia ya dunia hakuna nchi ilipata uhuru inaitwa TANZANIA.

Nchi iliyopata uhuru kwa tarehe hii na kwenye ardhi hii ni TANGANYIKA.

TANZANIA inatakiwa kusheherekewa siku ya MUUNGANO wa TANGANYIKA na ZANZIBAR.

Tusiyumbishwe na hulka zetu na kuoneana aibu. Kama kuna ushahidi dhidi ya hayo hapo juu yalete.

Hata wenzio wanakushangaa

View attachment 2037920
Kwahiyo shida ni jina tu?

Tanganyika na Tanzania?

Tunamaanisha Uhuru wa nchi, naamini tungekuwa na serikali moja tungeadhimisha siku ya leo.

Hatuna Tanganyika kwa sasa, huwezi kusema uhuru wa Tanganyika it's no sense...

Anyway kuelewa inahitaji uwe great thinker.
 
Tanganyika ilitaka Zanzibar iwe kolono lake Cha kushangaza Tanganyika ndo imekuwa koloni la Zanzibar , Watanganyika wanatapatapa Kama mfa maji hawajui hata taifa lao liko wapi na utambulisho wao Kama Wana Tanganyika
 
Mdogo wangu Paschal nimeona unaungana na hoja ya Uhuru wa Tanzania SIYO Tanganyika. Naomba utusaidie kujua mambo yafutayo;

1. 9/12/1961 kulikuwepo na Tanzania?

2. Je Tanganyika au Tanzania Bara imewahi kubadili jina ikajiita Tanzania? If yes,lini na kwa hati gani?

3. Tukisema Uhuru wa Tanzania tunamaanisha hata Zanzibar walipata Uhuru wao 9/12/1961?

4. Kama Zanzibar inatarehe yake yakupata Uhuru ambayo naamini ni siku ya Mapinduzi, tunasemaje Tanzania ilipata Uhuru mwaka 1961 tukijua kilichopata Uhuru ni sehemu tu ya Tanzania ambayo ni Tanganyika?

5. Kwa uelewa wako Mapinduzi ya Zanzibar yanaweza kutambua kama siku ya Uhuru ya Zanzibar?

6. Hoja Yako ya kusherekea ya Sasa ( present) umeitoa kwenye nyaraka gani?

Nauliza haya baada ya kuona mada zako zote zimeacha lakuna kwenye maeneo hayo: Nikutakie siku njema ya Uhuru wa Watanganyika
Huyu Pasco asipotoshe tunasherekea Uhuru wa Tanganyika wala siyo Uhuru wa Tanzania. Ukweli utabaki hivyo mpaka mwisho wa Dunia. Pasco usipojua kaa kimya nayo ni busara, kuliko kui paka tope taaluma yako hauitendei haki. Kutaka madaraka kusikutese ukafikiria kwa tumbo badala ya kichwa. Nasisitiza TUNASHELEKEA UHURU WA TANGANYIKA.
 
Huu ujinga wakupotosha historia ya taifa letu inatufanya tuje kuonekana watu wajinga zaidi uko mbele.Nakwanini tupotoshe historia yetu.nini shida,au kuna kitu gani cha maana,cha muhimu na lazima hadi tufikie uko.Mbona wenzetu nzanzibar wao wamesimama na historia yao,au ni lini tuliwahi kuwasikia wakiazimisha sherehe za mapinduzi ya Tanzania visiwani......Mbona mataifa mengine yaliyoungana hatuyaoni wakiwa na uku kujikana kama sisi.Haya mamiungano yapo tu na huwa yanavunjikaga kwasababu swala la kuwepo kwa muungano inategemea na mawazo ya jamii husika kwa kipindi hicho,kwahiyo ata huu wakwetu leo upo lakini miaka 70 ijayo hunaweza usiwepo.sasa ni aibu taifa kubwa na zuri kama hili kuona kuna watu wazima,wasomi na viongozi wakijitutumua kupotosha historia ya taifa lao.ni aibu sana.
 
Watu mna maneno Yani mnasema kabisa eti Tanganyika kaolewa kwa Zanzibar na ndo Mana kakubali hadi kubadilisha jina lake,eti kisa kapenda hadi kafa kaoza ndo Mana kakabidhi kila kitu kwa Mme wake it means kashindwa hadi kujitawala hivo kaamua kumpa Mme wake amtawale.

Hii ni dharau kubwa maana ni zaidi ya umbumbumbu,nimeumia kwa kweli wachache wanatutawala wengi as if sisi huku Tanganyika ni mazuzu na sisi huku hatuluhusiwi kuongoza kwao ,huu ujinga ufike mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama imefikia Kutamka neno TANGANYIKA mnaona tabu mpaka siku ya UHURU wa Tanganyika mnasema Tanzania Kama sio UZUZU ni nini?
Sasa nimemfahamu KARUME Baada ya mapinduzi tu alipotangaza kuwa watoto wote Zanzibar lazima wasome bure mpaka secondary.
 
Hawa jamaa wanasababisha hata kuwafundisha watoto wetu iwe ngumu kweli. Nawengine waking vituko hivi hawaelewi kati ya yale yanayofundishwa darasani na yanayofanywa na viongozi wa nchi hii. Hili swali la UHURU likiiulizwa kwenye mitihani ya CIVICS huwa wanakosa. Maana vitabu vinasema mengine na watawala wanaleta uzushi mwingine
 
Kwahiyo shida ni jina tu?

Tanganyika na Tanzania?

Tunamaanisha Uhuru wa nchi, naamini tungekuwa na serikali moja tungeadhimisha siku ya leo.

Hatuna Tanganyika kwa sasa, huwezi kusema uhuru wa Tanganyika it's no sense...

Anyway kuelewa inahitaji uwe great thinker.
Haimake sense kwako kwasababu umekubali kupoteza historia yako.Jina ni utambulisho tu ila hapa hoja sio jina bali hilo jina linamtambulisha nani.kwasababu bila utambulisho maana yake hicho kitu hakipo.je ni kweli tanganyika haipo?
 
Back
Top Bottom