Je, leo ni uhuru wa Tanzania Bara au Tanganyika?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,269
2,024
Wadau nawasalimu.Leo ni tarehe 9 Desemba 2023 Miaka 62 toka Nchi yetu ipatiwe Uhuru wake kutoka kwa Mwingereza.

Kilichonishangaza ni kusikia kuwa Eti Leo ni Miaka 62 ya Uhuru wa TANZANIA BARA Nchi ambayo Binafsi Siijui ipo wapi inapatikana wapi ina ardhi ya ukubwa gani inapakana na Nchi ipi na Rais wake ni nani.

Kusema Tunasherehekea Miaka 62 ya Uhuru wa TANZANIA BARA ni Upotoshaji Mkubwa kwa kizazi hiki na Vizazi vijavyo kwani hakujawahi kuwa na NCHI HIYO ya TANZANIA BARA.

Nchi iliyopata UHURU Miaka 62 iliyopita ni TANGANYIKA na NCHI ya TANZANIA ilipatikana baada ya MUUNGANO wa TANGANYIKA(Nchi iliyopata Uhuru Miaka 62) ilipoungana na Nchi ya ZANZIBAR.

Nchi ya TANZANIA BARA Haipo na Haijawahi kuwepo.
 
Yaani nilisahau hatakama leo ni siku ya UHURU na JAMHURI. Mkuu ahsante kunikumbusha
 
Una haki ya kusahau mkuu. Unaanzaje kukumbuka uhuru wa nchi yenye watu milioni 60 lkn inaongozwa na mtu kutoka nchi nyingine yenye watu milioni moja???!!!
 
Wadau nawasalimu.Leo ni tarehe 9 Desemba 2023 Miaka 62 toka Nchi yetu ipatiwe Uhuru wake kutoka kwa Mwingereza.
Kilichonishangaza ni kusikia kuwa Eti Leo ni Miaka 62 ya Uhuru wa TANZANIA BARA Nchi ambayo Binafsi Siijui ipo wapi inapatikana wapi ina ardhi ya ukubwa gani inapakana na Nchi ipi na Rais wake ni nani.
Kusema Tunasherehekea Miaka 62 ya Uhuru wa TANZANIA BARA ni Upotoshaji Mkubwa kwa kizazi hiki na Vizazi vijavyo kwani hakujawahi kuwa na NCHI HIYO ya TANZANIA BARA.
Nchi iliyopata UHURU Miaka 62 iliyopita ni TANGANYIKA na NCHI ya TANZANIA ilipatikana baada ya MUUNGANO wa TANGANYIKA(Nchi iliyopata Uhuru Miaka 62) ilipoungana na Nchi ya ZANZIBAR.Nchi ya TANZANIA BARA Haipo na Haijawahi kuwepo.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Hakuna nchi inaitwa Tanzania Bara hapa duniani.
 
Una haki ya kusahau mkuu. Unaanzaje kukumbuka uhuru wa nchi yenye watu milioni 60 lkn inaongozwa na mtu kutoka nchi nyingine yenye watu milioni moja???!!!
Sababu siyo hiyo mkuu,anae ongoza ni Mtanzania kama mimi na Wewe!
 
Serikali, Wananchi, Madaktari, mawaziri mpaka 2023 hawajui wao ni wenyeji wa nchi ipi, kuna wanaojiita ni Tanzania Bara, Tanzania, Tanganyika na wengine wanajiita ni Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Chawa Haki Ngowi anamripoti Samia kwamba tuna adhimisha uhuru wa Tanzania Bara [Uhuru wa Zanzibar ulikuwa lini?]

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na naibu wake Meriprisca Mahundi ni wasoshalisti wanatuambia ni uhuru wa Tanganyika, hii ni kweli na huyu pepo ameshaiona. Hawa ndio mashujaa wa Taifa hili.

Wana JF, 9-12- ni uhuru wa nchi gani?

Angalia wizara yalivyojichanganya juzi;

WhatsApp Image 2023-12-12 at 09.47.02 (1).jpeg

WhatsApp Image 2023-12-12 at 09.47.00.jpeg

WhatsApp Image 2023-12-12 at 09.47.02.jpeg

WhatsApp Image 2023-12-12 at 09.47.03 (1).jpeg

09-12-2023 Tanganyika inasherehekea miaka 62 ya uhuru wa bendera toka kwa mkoloni wa Kiingereza.

Nakumbuka wakati tunapata uhuru Hayati Bwana Kambarage Nyerere, baba wa Taifa alisema, pamoja na uhuru huo, bado kama nchi tulikuwa na kazi ya kufanya kuendelea na mapambano dhidi ya maadui watatu wa nchi yetu ambao ni:

1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Inasikitisha sana kuona ni wachache sana ambao wanafaidika na matunda ya uhuru huu "bandia" kutokana na kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa wameshindwa kutuongoza vyema katika kukabiliana na maadui hao watatu wa Taifa letu.
Watu wachache waliokula asali ya "uhuru " wa bendera inajumuisha "wandani wa serikali " walioziwa nyumba za Serikali na uncle Ben kwa bei ya Passo, yaani nyumba ya Masaki -ukubwa ni eka na nusu anauziwa Waziri kwa milioni nne, tena analipa kwa instalment, baada tu ya kununua anakata robo heka akauza kwa bilioni mbili.

Kwa wakazi wa Dar -kutoka Posta[Upanga magharibi] mpaka Mwenge -Maeneo ya St Peters pale akina Zakhia Meghji wamenunua, Fatma Magimbi, Jaji Kaganda amenunua pale pembeni ya Puma enerrgy, Nyumba zote Seifee Hospitals, zile Yard zote mnaziona ni nyumba za serikali watu wamegawiwa, hii laana tuspotubu na hawa watu kurudishiwa fedha na nyumba kurudishwa serikalini basi hakika

Imefikia hatua wale tunaowaamini kutuongoza, wanakwenda kutumikia matumbo yao na ya familia zao pamoja na marafiki zao. Na kwa bahati mbaya sana wakishapewa dhamana, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi hizo hata baada ya kustaafu!

Maisha yanazidi kuwa magumu kwa watu wa hali ya chini huku viongozi na wafanyabiashara wakubwa wakizidi kujilimbikizia ukwasi pasipo kujali maumivu ya wananchi wenzao.

Mbunge mmoja wa mkoa wa Pwani anafanya biashara na serikali, ana kampuni ya catering, anahudumia shughuli nyingi na ni conflict of interest.

kamati ya Bunge zinakodisha mabasi ya mbunge wa Morogoro kwa hela ya juu sana, watu wanakula matunda ya "uhuru wa bendera".

Hivyo kama Taifa, tunahitaji kubadili uelekeo, tufanye kila linalowezekana kuwaondoa madarakani viongozi hawa na badala yake tuweke wazalendo watakaokuwepo kwa ajili ya kusimamia maslahi ya wananchi wote kwa ujumla na kuhakikisha kila mwananchi anafaidi keki ya Taifa. Na hili kulifanikisha hilo, tunapaswa kufanya kila linalowezekana tupate Katiba mpya.

Katiba Mpya itatusaidia kuwadhibiti viongozi wetu na kuwafanya watutumikie kwa uzalendo na uadilifu, watake wasitake!
 
Mpaka sasa sijafahamu ni kwa nini baadhi ya makada wa ccm wanatuletea huu upotoshaji.

Tarehe 09/12 kila mwaka tunaadhimisha Uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

Halafu tarehe 12/01 kila mwaka Wazanzibari wanaadhimisha siku ya Mapinduzi yao ya mwaka 1965.

Na tarehe 26/04 kila mwaka ndiyo kuna maadhimisho ya huu Muungano wetu wa kidwanzi (Muungano wa changu changu, chako changu), kati ya Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964! Na huu ndiyo uliokuja kuzaa hili jina la Tanzania.

Kwa hiyo kama wansiasa wanataka kuifuta Tanganyika, basi waifute poa na Zanzibar. Yaani kuwepo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani! Na siyo hizi porojo za kuifuta Tanganyika kwa kuiita Tanzania Bara, huku Zanzibar ikibakia na utambulisho wake wa awali. Huu upuuzi ndiyo unaosababisha hata Muungano wenyewe uonekane ni wa kidwanzi.
 
Serikali, Wananchi, Madaktari, mawaziri mpaka 2023 hawajui wao ni wenyeji wa nchi ipi, kuna wanaojiita ni Tanzania Bara, Tanzania, Tanganyika na wengine wanajiita ni Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Chawa Haki Ngowi anamripoti Samia kwamba tuna adhimisha uhuru wa Tanzania Bara [Uhuru wa Zanzibar ulikuwa lini?]

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na naibu wake Meriprisca Mahundi ni wasoshalisti wanatuambia ni uhuru wa Tanganyika, hii ni kweli na huyu pepo ameshaiona. Hawa ndio mashujaa wa Taifa hili.

Wana JF, 9-12- ni uhuru wa nchi gani?

Angalia wizara yalivyojichanganya juzi;

View attachment 2840186
View attachment 2840159
View attachment 2840166
View attachment 2840167

09-12-2023 Tanganyika inasherehekea miaka 62 ya uhuru wa bendera toka kwa mkoloni wa Kiingereza.

Nakumbuka wakati tunapata uhuru Hayati Bwana Kambarage Nyerere, baba wa Taifa alisema, pamoja na uhuru huo, bado kama nchi tulikuwa na kazi ya kufanya kuendelea na mapambano dhidi ya maadui watatu wa nchi yetu ambao ni:

1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Inasikitisha sana kuona ni wachache sana ambao wanafaidika na matunda ya uhuru huu "bandia" kutokana na kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa wameshindwa kutuongoza vyema katika kukabiliana na maadui hao watatu wa Taifa letu.
Watu wachache waliokula asali ya "uhuru " wa bendera inajumuisha "wandani wa serikali " walioziwa nyumba za Serikali na uncle Ben kwa bei ya Passo, yaani nyumba ya Masaki -ukubwa ni eka na nusu anauziwa Waziri kwa milioni nne, tena analipa kwa instalment, baada tu ya kununua anakata robo heka akauza kwa bilioni mbili.

Kwa wakazi wa Dar -kutoka Posta[Upanga magharibi] mpaka Mwenge -Maeneo ya St Peters pale akina Zakhia Meghji wamenunua, Fatma Magimbi, Jaji Kaganda amenunua pale pembeni ya Puma enerrgy, Nyumba zote Seifee Hospitals, zile Yard zote mnaziona ni nyumba za serikali watu wamegawiwa, hii laana tuspotubu na hawa watu kurudishiwa fedha na nyumba kurudishwa serikalini basi hakika

Imefikia hatua wale tunaowaamini kutuongoza, wanakwenda kutumikia matumbo yao na ya familia zao pamoja na marafiki zao. Na kwa bahati mbaya sana wakishapewa dhamana, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi hizo hata baada ya kustaafu!

Maisha yanazidi kuwa magumu kwa watu wa hali ya chini huku viongozi na wafanyabiashara wakubwa wakizidi kujilimbikizia ukwasi pasipo kujali maumivu ya wananchi wenzao.

Mbunge mmoja wa mkoa wa Pwani anafanya biashara na serikali, ana kampuni ya catering, anahudumia shughuli nyingi na ni conflict of interest.

kamati ya Bunge zinakodisha mabasi ya mbunge wa Morogoro kwa hela ya juu sana, watu wanakula matunda ya "uhuru wa bendera".

Hivyo kama Taifa, tunahitaji kubadili uelekeo, tufanye kila linalowezekana kuwaondoa madarakani viongozi hawa na badala yake tuweke wazalendo watakaokuwepo kwa ajili ya kusimamia maslahi ya wananchi wote kwa ujumla na kuhakikisha kila mwananchi anafaidi keki ya Taifa. Na hili kulifanikisha hilo, tunapaswa kufanya kila linalowezekana tupate Katiba mpya.

Katiba Mpya itatusaidia kuwadhibiti viongozi wetu na kuwafanya watutumikie kwa uzalendo na uadilifu, watake wasitake!
tanganyika ni nchi ya wakoloni na waliotawaliwa wakati wa hiyo tanganyika nadhani wapo wachache tu hivi sasa...

wanachi na vijana wengi wanachofahamu Tanzania pekee, hiyo tanganyika ya wakoloni ni historia tu haina maana yeyete tena..
 
Joined may 2023 , brought up na maziwa ya Cerelac.

Kwahiyo USA iliyopata uhuru miaka 300 iliyopita na George WAshington kizazi cha sasa hakuji wala historia yao haiwasaidii?

hii nchi , kuna watu wa kufunga kamba na kuwahamishia Burundi!
wewe ni kati ya Wapuuzi wa mwisho baada ya alinacha.
 
Mpaka sasa sijafahamu ni kwa nini baadhi ya makada wa ccm wanatuletea huu upotoshaji.

Tarehe 09/12 kila mwaka tunaadhimisha Uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

Halafu tarehe 12/01 kila mwaka Wazanzibari wanaadhimisha siku ya Mapinduzi yao ya mwaka 1965.

Na tarehe 26/04 kila mwaka ndiyo kuna maadhimisho ya huu Muungano wetu wa kidwanzi (Muungano wa changu changu, chako changu), kati ya Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964! Na huu ndiyo uliokuja kuzaa hili jina la Tanzania.

Kwa hiyo kama wansiasa wanataka kuifuta Tanganuika, basi waifute poa na Zanzibar. Yaani kuwepo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani! Na siyo hizi porojo za kuifuta Tanganyika kwa kuiita Tanzania Bara, huku Zanzibar ikibakia na utambulisho wake wa awali. Huu upuuzi ndiyo unaosababisha hata Muungano wenyewe uonekane ni wa kidwanzi.
Kuna madaktari na maprofesa ni aibu kukufundisha, kabisa wanajitoa ufahamu wakijua kweli na kuwa wandanganya.
 
Joined may 2023 , brought up na maziwa ya Cerelac.

Kwahiyo USA iliyopata uhuru miaka 300 iliyopita na George WAshington kizazi cha sasa hakuji wala historia yao haiwasaidii?

hii nchi , kuna watu wa kufunga kamba na kuwahamishia Burundi!
wewe ni kati ya Wapuuzi wa mwisho baada ya alinacha.
kwamba joined feb.2016 unapanic na kukosa content kiasia hiki, na kwamba mihemko na ghadhabu zako zitabadili fikra na uelewa wa vijana kuhusu kitu Tanganyika ya kikoloni na isiyokuwepo na isiyo na maana yoyote?

ndio maana nasema mko na mbebaki wachache sana na hamna contents za kushawishi wasiokijua hicho kitanganyika, mtabaki kuyaporomosha tu bila kuwa na sababu muhimu za kubadili fikra za wasiokihitaji wala kukijua hicho kitanganyika chenu....
 
Mtaa wa Bongoyo-Oysterbay, nyumba zote zilizokuwa mali ya Serikali, viongozi wafanyabiashara na wakuu wa vitengo wamejimilikisha mali ya umma. Ukoloni bado upo tu, nchi imeshikwa na wakoloni weusi.
 
Serikali, Wananchi, Madaktari, mawaziri mpaka 2023 hawajui wao ni wenyeji wa nchi ipi, kuna wanaojiita ni Tanzania Bara, Tanzania, Tanganyika na wengine wanajiita ni Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Chawa Haki Ngowi anamripoti Samia kwamba tuna adhimisha uhuru wa Tanzania Bara [Uhuru wa Zanzibar ulikuwa lini?]

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na naibu wake Meriprisca Mahundi ni wasoshalisti wanatuambia ni uhuru wa Tanganyika, hii ni kweli na huyu pepo ameshaiona. Hawa ndio mashujaa wa Taifa hili.

Wana JF, 9-12- ni uhuru wa nchi gani?

Angalia wizara yalivyojichanganya juzi;

View attachment 2840186
View attachment 2840159
View attachment 2840166
View attachment 2840167

09-12-2023 Tanganyika inasherehekea miaka 62 ya uhuru wa bendera toka kwa mkoloni wa Kiingereza.

Nakumbuka wakati tunapata uhuru Hayati Bwana Kambarage Nyerere, baba wa Taifa alisema, pamoja na uhuru huo, bado kama nchi tulikuwa na kazi ya kufanya kuendelea na mapambano dhidi ya maadui watatu wa nchi yetu ambao ni:

1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Inasikitisha sana kuona ni wachache sana ambao wanafaidika na matunda ya uhuru huu "bandia" kutokana na kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa wameshindwa kutuongoza vyema katika kukabiliana na maadui hao watatu wa Taifa letu.
Watu wachache waliokula asali ya "uhuru " wa bendera inajumuisha "wandani wa serikali " walioziwa nyumba za Serikali na uncle Ben kwa bei ya Passo, yaani nyumba ya Masaki -ukubwa ni eka na nusu anauziwa Waziri kwa milioni nne, tena analipa kwa instalment, baada tu ya kununua anakata robo heka akauza kwa bilioni mbili.

Kwa wakazi wa Dar -kutoka Posta[Upanga magharibi] mpaka Mwenge -Maeneo ya St Peters pale akina Zakhia Meghji wamenunua, Fatma Magimbi, Jaji Kaganda amenunua pale pembeni ya Puma enerrgy, Nyumba zote Seifee Hospitals, zile Yard zote mnaziona ni nyumba za serikali watu wamegawiwa, hii laana tuspotubu na hawa watu kurudishiwa fedha na nyumba kurudishwa serikalini basi hakika

Imefikia hatua wale tunaowaamini kutuongoza, wanakwenda kutumikia matumbo yao na ya familia zao pamoja na marafiki zao. Na kwa bahati mbaya sana wakishapewa dhamana, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi hizo hata baada ya kustaafu!

Maisha yanazidi kuwa magumu kwa watu wa hali ya chini huku viongozi na wafanyabiashara wakubwa wakizidi kujilimbikizia ukwasi pasipo kujali maumivu ya wananchi wenzao.

Mbunge mmoja wa mkoa wa Pwani anafanya biashara na serikali, ana kampuni ya catering, anahudumia shughuli nyingi na ni conflict of interest.

kamati ya Bunge zinakodisha mabasi ya mbunge wa Morogoro kwa hela ya juu sana, watu wanakula matunda ya "uhuru wa bendera".

Hivyo kama Taifa, tunahitaji kubadili uelekeo, tufanye kila linalowezekana kuwaondoa madarakani viongozi hawa na badala yake tuweke wazalendo watakaokuwepo kwa ajili ya kusimamia maslahi ya wananchi wote kwa ujumla na kuhakikisha kila mwananchi anafaidi keki ya Taifa. Na hili kulifanikisha hilo, tunapaswa kufanya kila linalowezekana tupate Katiba mpya.

Katiba Mpya itatusaidia kuwadhibiti viongozi wetu na kuwafanya watutumikie kwa uzalendo na uadilifu, watake wasitake!
Kafanye mambo yako upunguze umaskini wako na wa familia yako
 
Back
Top Bottom