Mimi siungi mkono hadi kesho.
Hawa SDs wanafuata tu script waliyopewa na wale Wamarekani. Kansa ya Chelsea iko kwa hao owners.
Kwa taarifa nilizonazo, ni watu wanaodhibiti kila kitu—kuanzia maamuzi ya juu, usimamizi wa timu, hadi sera za uendeshaji. Ukipishana tu na wanachotaka, unafukuzwa. Na anayeongoza mfumo huo ni Behdad Eghbali, ambaye ni mkali sana kwenye kufuata policies za project. Hata hivyo, kina Todd Boehly nao wako kwenye mtiririko huo huo.
Kwa hiyo kuwalaumu SDs, ambao ni waajiriwa tu wanaotekeleza maagizo, ni uonevu mkubwa. Tatizo haliko kwao; tatizo liko kwa wale wanaowaajiri na kuwaelekeza jinsi ya kufanya kazi.