Andoni Iraola kufanya vizuri Bournemouth haimaanishi kwamba anafaa kwenye mradi wa Chelsea. Kiuhalisia, yeye ni Liam Rosenior toleo la 2.0; kocha anayejenga mfumo wake juu ya mbio nyingi na matumizi makubwa ya nguvu za wachezaji. Huo si mfumo unaolingana na kikosi cha Chelsea, na ungeongeza tu idadi ya majeraha ambayo tayari yametutesa kwa misimu kadhaa.
Wamiliki wa Chelsea bado hawajifunzi. Kila mara wanachukua makocha ambao falsafa zao hazilingani na aina ya wachezaji tulionao, halafu wanashangaa mambo yanapoharibika ghafla.
Kinachohitajika sasa ni kocha wa kiwango cha juu mwenye sifa kama za Maresca — mtu anayejenga mfumo tulivu, nidhamu uwanjani, na udhibiti wa majeruhi. Chini ya Maresca, kikosi kilipata balance, na hata wachezaji wetu wanaopata majeraha mara kwa mara waliweza kudhibitiwa vizuri kwa sababu mfumo wake ulihitaji akili na nidhamu zaidi kuliko kukimbia ovyo.
Kama wamiliki wanataka mafanikio ya muda mrefu, lazima waache kusaka “project coach” wa kusisimua na badala yake wamuajiri meneja anayolingana na wachezaji tulionao na si upumbavu wanaojaribu kulazimisha kila wakiajiri kocha.
View attachment 3577713