Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Kinachonichosha kwa Potter ni kukumbatia wachezaj ambao wanacheza vibaya
Havertz n Mount week in week out wanacheza vibaya ila cha ajabu bado wataendelea kuanza.

1.. bKwa nini wengine wakicheza vibaya anawaweka bench ila hao wawili utasema wanapicha zake za magendo

Kwa dakik 15 alizocheza Datro Fofana kafanya+ mengi kuliko dakika 90 alizocheza havertz.

Potter soon watu wataanza kutokuwa na imani nae kama ataendelea hivi hiv kuwa clueless na kukumbatia zile takatak 2
Tulishasema mapema Potter sio kocha sahihi kwa hii timu msiweke matumaini yoyote kwake
 
Harry Potter ni bonge la kocha na anaweza kuwashusha daraja kama mambo yatakwenda vizuri, kitu cha msingi ni kumuunga mkono ili aonyeshe uwezo wake.
Screenshot_20230112_113321.jpg
 
Potter is not a top coach.. needs to be replaced.. I think Chelsea's problem is the coach
Exactly the problem yesterday was from technical side i have no doubt on individual ability shown.. Our coach is so average, the summer signings were so enough but Chelsea spirit is lost players are also lamenting about coaching
 
Mimi nikisema hapa kwamba Havertz ni takataka mnakataa na kumtetea kisa alifunga kwenye fainali. Ni upuuzi kumtetea kwa sababu hiyo, Havertz ndio inapaswa atoke wa kwanza kwenye dirisha kubwa.
Kweli kabisa, yani Auba kama angekuwa ni mwingireza hata acheze vibaya bado angepangwa na wala asingeondolewa kwenye kikosi cha UEFA.

Huwa nasema hiv Mount ndio star wa team ambae hapaswi kuwekwa bench.
Hajaanza kucheza vibaya leo, bali imekuwa kila gameweek.

Game ya mwisho ambaho hakucheza ilikuwa dhid ya city (league) na tulikuwa vizuri,

Ukiniambia mpk sasa kipi kinachomfanya Potter asimtumie Datro Fofana, sielewi maana mchezaj kila anapoingia anaonyesha kitu,
Jana kwa dakika 15 alizocheza kawapa tough game wale wakina Ream na Tete,
Ni tofauti na havertz miguu imekaa kama mlenda,
Oscar alikuwa soft ila hakuwa kama hivi Havertz.

Utaona wiki ijayo Mount na Havertz bado wanaanza
 
Na wale wanaomtetea kisa goli la uefa nawashangaa
Mkuu mimi sikubahatika kuangalia game jana ila nimeona highlights kwakweli nakiri dogo kazingua sana jana. Nasema hivyo kwa sabab0u mimi ni kati ya wanaomtetea na huwa simtetei eti kwa sababu kafunga goli la UEFA hii ni sababu ya kipuuzi sana na inaashiria sisi sio watu wa kuwafatilia wachezaji kiufundi zaidi badala yake tunaangalia performance kwa wakati husika.

Mimi binafsi nimeanza kumjua Havertz misimu miwili kabla hajasajiliwa Chelsea so kiufundi namuelewa sana. Toka amekuja Chelsea hajawa na performance nzuri kama ile tunayoiona akiwa Leverkusen na hata anapochezea timu ya taifa. Tuniulize sababu ni nini? Kama kuna mtu ameangalia WC hii ya 2022 kati ya wachezaji wa Germany waliokuwa na perfomance nzuri ukiachana na Musiala basi Havertz naye yupo.

Kitu pekee nachoona kinamsumbua Havertz ni swala la kisaikolojia tu. Naona bado ana pressure kutaka kuprove wrong kwamba ile price tag yake imelipa. Lakini pia aina ya wachezaji wanaomzunguka kule Leverkusen alikua na wachezaji wengi wajurumani wenzake na hata timu ya taifa kazungukwa na kina Gnabry, Musiala, Sane, Muller hawa ukiacha kuwa ni wajerumani wenzake pia ni mafundi wanatengeneza spaces inamsaidia.

Zipo factor nyingi ila nachoona dogo anahitaji msaada wa psychology zaidi kuliko kiufundi. Tumeshaanza kupata wachezaji wazuri akijengwa akawekwa sawa naamini tutakua na yule Havertz wa B. Leverkusen na Alemania. Pia hili tatizo lishawahi kumkumba hata Kepa lakini naona saivi katulia.

I stand to be corrected.
 
Exactly the problem yesterday was from technical side i have no doubt on individual ability shown.. Our coach is so average, the summer signings were so enough but Chelsea spirit is lost players are also lamenting about coaching
Summer signing were not enough, tuliacha tatua maeneo ambayo yanashida

Player wengi walikiwa ni kwa ajili ya short term plan.

Game dhid ya leeds,southampton,dinaml zagreb zote hizi zilionesha mapungufu tena tukiwa tuko chini ya top coach.

Summer signing badala ya kutuimprove nikama zilitushusha
 
Kipindi cha Tuchel mchezaji akizingua game mojainayofuata anakula bench hii iliwasaidia sana kina Mount kuboresha viwango vyao. Game inayofuata Pottee asimuanzishe Havertz aanze na Fofana nimeona dogo ana touch nzuri. Pia itamuamsha Havertz
 
Havertz ni takataka tu inatosha kwa alicho fanya aondoke dirisha kubwa.
Mkuu mimi sikubahatika kuangalia game jana ila nimeona highlights kwakweli nakiri dogo kazingua sana jana. Nasema hivyo kwa sabab0u mimi ni kati ya wanaomtetea na huwa simtetei eti kwa sababu kafunga goli la UEFA hii ni sababu ya kipuuzi sana na inaashiria sisi sio watu wa kuwafatilia wachezaji kiufundi zaidi badala yake tunaangalia performance kwa wakati husika.

Mimi binafsi nimeanza kumjua Havertz misimu miwili kabla hajasajiliwa Chelsea so kiufundi namuelewa sana. Toka amekuja Chelsea hajawa na performance nzuri kama ile tunayoiona akiwa Leverkusen na hata anapochezea timu ya taifa. Tuniulize sababu ni nini? Kama kuna mtu ameangalia WC hii ya 2022 kati ya wachezaji wa Germany waliokuwa na perfomance nzuri ukiachana na Musiala basi Havertz naye yupo.

Kitu pekee nachoona kinamsumbua Havertz ni swala la kisaikolojia tu. Naona bado ana pressure kutaka kuprove wrong kwamba ile price tag yake imelipa. Lakini pia aina ya wachezaji wanaomzunguka kule Leverkusen alikua na wachezaji wengi wajurumani wenzake na hata timu ya taifa kazungukwa na kina Gnabry, Musiala, Sane, Muller hawa ukiacha kuwa ni wajerumani wenzake pia ni mafundi wanatengeneza spaces inamsaidia.

Zipo factor nyingi ila nachoona dogo anahitaji msaada wa psychology zaidi kuliko kiufundi. Tumeshaanza kupata wachezaji wazuri akijengwa akawekwa sawa naamini tutakua na yule Havertz wa B. Leverkusen na Alemania. Pia hili tatizo lishawahi kumkumba hata Kepa lakini naona saivi katulia.

I stand to be corrected.
 
Nikikumbuka humu ndan kuna watu walikuwa wanampigia chapuo Potter nabaki naishiwa nguvu.

Tungeenda kwa Luis Enrique kwa project tuliyonao ni mtu sahihi.

Tunaweza kuwa na wachezaj wazuri ila wakakosa kocha, inanikumbusha wakat tuliokuwa na MaZaCa(Mata,Hazard,Oscar) kocha akawa Di mateo
Bora Di mateo timu ilikuwa inacheza na magoli yalikuwa yanapatikana lakini huyu Potter hata goli 1 kupata ni shughuli
Timu mpaka inazidiwa magoli na Halland bwana uchezaji hauweleki kabisa
 
Maoni yangu kuhusu mechi ya Jana.

Nimeona wengi wakilalamika kuhusu viwango vya mount, kai havert na Gallagher na wengine Ziyech, unapokuwa mchambuzi na mzoefu wa kuangalia mechi ni vizuri ukaangalia tatizo la msingi kwanza kabla ujaenda kwenye matokeo nilichoona Jana chelsea ilikosa identity ya uchezaji au kwa jina lingine tunasema pattern style of playing ikafanya chelsea itumie uwezo binafsi ya wachezaji kunapokosekana Muundo sahihi wa uchezaji utafanya hata baadhi ya wachezaji wasionekane hatari mfano mzuri ni Mudryk ule upande wake haukutumika kabisa mipira ilikuwa haifikii.

Tukija kwa hawa wachezaji wanaolalamikiwa kufanya vibaya tuanze Kai huyu jamaa ni bonge la mchezaji ila anachezeshwa sehemu isiyo sahihi hadi leo Kai namtazama kama mchezaji anayeweza kucheza kwenye no 10 ila sio striker sijui kwanini kocha halioni Hili? Mount katengeneza nafasi mbili za wazi Jana lakini watu wanamponda japo hatukuwa na Muundo mzuri wa uchezaji, Gallagher kajituma Sana lakini kuna sehemu anatakiwa awe improved na kocha hasa kwenye kwenye Technical ability, Ziyech japo kaathirika na Muundo mzima wa uchezaji wa jana lakini aliweza kutoa chance nzuri Sana kwa kai lakini haikutumiwa vizuri

NB: Tuna wachezaji wazuri Sana tumewasajili na wote wameonesha Wana kitu chakuoffer kwenye team hivi pata picha Enzo acheze na Kante au Kovacic pale Kati?
Binafsi naona solution ni kumfukuza kocha kabisa hakuna njia nyingine tofauti, Moja ya sababu kuu naona Potter hatufahi chelsea imekaa wiki mbili bila kucheza game yoyote Jana ndio wakaja kucheza unajiuliza hizo wiki mbili mbona ni nyingi walikuwa wanafanya nini? Kiasi ambacho unaona kabisa imecheza kama vile walikosa msimamizi mazoezini.

juan david
lembu
Covax
Cash Money Forever
johsee
Mkuu naunga mkono hoja haswa ya uwezo wa kocha maana kaja na cheap notion kwamba anatengeneza timu kama kichaka alichokuwa anajifichia Lampard those days na mimi mwanzo nilikuwa naunga mkono.ni kweli kizuri kinahitaji muda sasa baada ya miezi 4 najaribu kuitafuta philosophy na pattern ya uchezaji ya mwalimu siioni yaani kocha gani hana identity ya uchezaji kwa mantiki hiyo huwezi kuwa na guts za kusema kwamba wachezaji fulani hawafai completely maana wanakosa muunganiko wa mawazo ya kiuchezaji. Kwa case ya Mount naona ni kama inayomkuta Trend Arnold ni wachezaji wazuri ila wametumika sana kwenye umri mdogo na haswa kwenye matumizi ya nguvu hiyo wanafatigue ya mwili na akili wanafaa tu kuwa na playing time ndogo kwa muda. Kingine, why timu haina madhara kabisa kwenye set pieces kona zinapigwa kama mpira wa shule ulioangukia barabarani alafu mpita njia anaupiga urudi uwanjani
 
Kweli kabisa, yani Auba kama angekuwa ni mwingireza hata acheze vibaya bado angepangwa na wala asingeondolewa kwenye kikosi cha UEFA.

Huwa nasema hiv Mount ndio star wa team ambae hapaswi kuwekwa bench.
Hajaanza kucheza vibaya leo, bali imekuwa kila gameweek.

Game ya mwisho ambaho hakucheza ilikuwa dhid ya city (league) na tulikuwa vizuri,

Ukiniambia mpk sasa kipi kinachomfanya Potter asimtumie Datro Fofana, sielewi maana mchezaj kila anapoingia anaonyesha kitu,
Jana kwa dakika 15 alizocheza kawapa tough game wale wakina Ream na Tete,
Ni tofauti na havertz miguu imekaa kama mlenda,
Oscar alikuwa soft ila hakuwa kama hivi Havertz.

Utaona wiki ijayo Mount na Havertz bado wanaanza
Oscar alikuwa anakaza kuliko huyu Havertz, pia Oscar alikuwa mwepesi sana na maamuzi ya akili usimfananishe kabisa na Havertz.

Madueke, Enzo, Fofana, Gallagher, Cucu, Badishiele walicheza vizuri sana.

Enzo hatujapigwa akiendelea kucheza vizuri kama jana.

Wepesi wa mashambulizi bado hatujawa fiti sana maana kuna nafasi za kaunta ataki zingeweza kutupa mafanikio jana hata kwa goli 2 lakini ndiyo hivyo tena.

Kona hatujafaulu kabisa katika kutengeneza mashambulizi hatari.

HP alifanya subs nzuri isipokuwa ana ujinga wa kukumbatia matatizo (Havertz na Mount).

Mechi ya jana ilipaswa Chelsea ishinde ili kuwajengea wachezaji kujiamini kwa mechi zijazo.
 
Kwenye Youtube mashabiki wanawalalamikia wachezaji wanne hivi
  1. Ziyech
  2. Gallagher
  3. Cucurella na
  4. Havertz
Wanasema hao wachezaji hawakutakiwa kuanza kabisa
Gallagher jana alipambana sana mi namtetea kwakweli yani kila sehemu alikuwa akikaba na ku-press mipira kwa kasi sana kama ile nafasi aliyoichopu kwenda kwa Fofana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom