siku ya kufa Mbwa basi Pua zote zinaziba.
Chelsea leo wanaingia uwanjani kwa Bayern yaani Alianz Arena wakienda kujaribu kuushangaza Ulimwengu.
Hawana rekodi yoyote na kombe hili, ni moja ya timu ndogo ktk mashindano haya, hawapewi nafasi ya kulichukua kombe hili, na kama yupo Mshabiki anayeweka Pesa nyuma ya Chelsea basi atakuwa anayataka Majanga kwa lazima.
Bayern Bavaria Munchen wakiwa ktk uwanja wao wa nyumbani ambao ni wa kisasa chini ya Nahodha Philip Lahm wako ktk hali nzuri ya kimchezo, wanatambulika kuwa ni moja ya timu kubwa Barani Ulaya wakiwa wamebeba kombe hili mara 4, wanapewa nafasi kubwa ya kunyanyua kombe hili kwani kufika kwao Fainali ni wazi kuwa wengi wenye utimamu kichwani tulikutaraji.
Wakiwakosa Wachezaji wao kama Mgogo Alaba, Batstuber na Gustavo Bayern wameonekana kuto kutetereka tofauti na wapinzani wao ambao kwa kuwakosa Terry, Meireres na Ramirez wameonekana kupwaya na hata baadhi ya washabiki wa Chelsea wameonekana kutokuwa tayari kwa mchezo wa leo.
All in all dobi wa kweli utamjuwa siku akipewa nguo nyeupe...