Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Olachuga a.k.a ole chunya karibu chama kubwa aseno de guners mabigwa wa epl usiulize epl ipi ila karibu mno

London is red
 
Fununu za usajili zinasema Chelsea inamfukuzia Donnaruma. Yaani ikimsajili itakua na makipa wawili ambao kiwango chao kinawaruhusu kua first team.

Nafasi ya ukipa hadi umpiku mwenzako ni ngumu sana. Martinez akaona bora aende Villa ili awe kikosi cha kwanza, Mendy alikubali kuja chelsea akijua wazi anakua kikosi cha kwanza.

Donnaruma hawezi kuja kama hatohakikishiwa kuanza. Au labda recruitment ya chelsea ina mpango wa kumtimua mendy.

So chelsea itakua na mendy, kepa, cech na donnaruma kwenye benchi
Tuwape william
 
Watatu hawa kumridhi Lampard, Mazungumzo ya kumtimua yameanza
Madai ni kwamba Lampard kapewa muda na hakuna hata dalili za mbinu zake kuleta matunda yeyote pale darajani

  1. Tuchel - Katika timu kubwa alishaifundisha Dotmund miaka miwili na PSG miaka miwili na nusu ligi ya wakulima wining %age ni 74 akiwa PSG
  2. Allegri amefundisha muda mrefu vitimu vidogo, Juve kifundisha miaka 5 na wining %age ya 70% akiwa Juve
  3. Avram Grant - Hana uzoefu wowote zaidi ya kuifundisha Chelsea 2007/8 na Westham 2010/11. Hakutoka Chelsea vizuri kwani wachezaji hawakumpenda kwa sababu ufundishaji wake ni wa kizamani mno miaka 25 iliyopita na hakuwa na mbinu zozote za kisasa kwa wakati huo wa 2007/8. Sasa tuko 2021, si atakuja na mbinu za miaka 40 iliyopita?
Hii ishu ya Lampard kugewa ultimatum niliiona sehemu. Katika hao makocha bora Allegri, Tuchel miyeyusho, ligi ya wakulima na kikosi kama kile aliyoyafanya hata hayampendezi Mungu.
 
Naomba niseme kinachomuua Lampard
Hawa wachezaji wanaifanya Chelsea ikose Consistency
  1. Reece James - Tatizo lake kubwa ni kwenye kukaba hasa kwa kuacha space, mfano mechi na Leicester alikuwa kila mara akitoka out of position wakati Chelsea inashambuliwa na hivyo kumpa Barnes nafasi ya kushusha mashambulizi atakavyo
  2. Rudiger - Japo kaiprove tangu atoke majeruhi mwaka jana Rudiger amekuwa na tatizo la concetration na kujisahau na kuacha space kubwa kwenye final third ya Chelsea
  3. Viungo wote wa Chelsea hawako creative, hawajui kupeleka mashambulizi mbele, hawajui kutengeneza nafasi. Kovacic ule moto wake wa mwaka jana umezima kabisa, Kante mbinu zake za kupress na kuintercept ni kama imeshapitwa na wakati, Jorginho sijui kinachomsibu ni nini kwa sababu ule uwezo wake wa kuthibiti na kuamua mpira pale katikati uchezweje haupo tena
  4. Havertz ndio legelege toka aje kwenda mbele ni kama hana hamu ya kuichezea Chelsea. Mtu pekee ninayemuaona anajitahidi pale katikati ni Mason Mount
  5. Winga na strikers wetu ovyo kabisa. Odoi akitokea sub anakuwa mzuri ila akianza anakuwa kama kiazi, Ziyech bado hajarudi kwenye form kabla ya majeruhi, Pulisic anafight lakini mambo bado kabisa. Werner kila siku inapokucha ndio anazidi kuwa wa hovyo kabisa. Katika mechi kama tatu zilizopita na kwenda huko nyuma tatizo la Werner ilikuwa ni kosakosa kwenye kufunga, sasa tatizo lake limeongozeka hata kwenye kupasi amekuwa hajiamini, butua butua kwenye kufunga na butuabutua kwenye kutoa pasi. Tammy Abraham kama kawaida yakeanajitahidi ila uwezo wake ni mdogo, bado hajakoma kwenye Big matches. Giroud wa kawaida sana lakini kwa ukweli bado hajatumiwa kama inavyotakiwa na Lampard ni kama hana mpango naye tena anafocus kuwatumia wenye umri mdogo
  6. Wachezaji pekee wenye consistency ni Silva,Mount, Zouma, Mendy, Giroud**
 
Chelsea fc under LAMPARD

Werner flop
Ziyech flop
Pulisic flop
Giroud flop
Odoi flop
Kante flop
Joginho flop
Azipu flop
Kovacic flop
Keppa flop
Rudger flop
Barkley flop
Abraham flop
Harvetz flop

Basi Lampard apewe pesa ya usajili anunue wachezaji 8 wapya.
Giroud ajaflop sema nafasi apewi na hata akipewa nafasi hizo chache anafanya kweli kwahiyo mtoe kwenye Hiyo list.
 
Chelsea fc under LAMPARD

Werner flop
Ziyech flop
Pulisic flop
Giroud flop
Odoi flop
Kante flop
Joginho flop
Azipu flop
Kovacic flop
Keppa flop
Rudger flop
Barkley flop
Abraham flop
Harvetz flop

Basi Lampard apewe pesa ya usajili anunue wachezaji 8 wapya.

Mbinu bana hao hawajafloap unafikir akipewa rogers au yule kocha wa spurs wa zaman darajan patakuwa sehem rahisi?
 
chelsea kazaneni hiko kijiti mumpe liverpool, wakati arsenal tunazingua mlijiona wajanja, mlituacha point 11, muda huu zimebaki 2,

au nasema uongo ndugu zangu?

msema kweli ni mpenz wa Mungu....
 
chelsea kazaneni hiko kijiti mumpe liverpool, wakati arsenal tunazingua mlijiona wajanja, mlituacha point 11, muda huu zimebaki 2,

au nasema uongo ndugu zangu?

msema kweli ni mpenz wa Mungu....
Kwani mmepona?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom