Naomba niseme kinachomuua Lampard
Hawa wachezaji wanaifanya Chelsea ikose Consistency
- Reece James - Tatizo lake kubwa ni kwenye kukaba hasa kwa kuacha space, mfano mechi na Leicester alikuwa kila mara akitoka out of position wakati Chelsea inashambuliwa na hivyo kumpa Barnes nafasi ya kushusha mashambulizi atakavyo
- Rudiger - Japo kaiprove tangu atoke majeruhi mwaka jana Rudiger amekuwa na tatizo la concetration na kujisahau na kuacha space kubwa kwenye final third ya Chelsea
- Viungo wote wa Chelsea hawako creative, hawajui kupeleka mashambulizi mbele, hawajui kutengeneza nafasi. Kovacic ule moto wake wa mwaka jana umezima kabisa, Kante mbinu zake za kupress na kuintercept ni kama imeshapitwa na wakati, Jorginho sijui kinachomsibu ni nini kwa sababu ule uwezo wake wa kuthibiti na kuamua mpira pale katikati uchezweje haupo tena
- Havertz ndio legelege toka aje kwenda mbele ni kama hana hamu ya kuichezea Chelsea. Mtu pekee ninayemuaona anajitahidi pale katikati ni Mason Mount
- Winga na strikers wetu ovyo kabisa. Odoi akitokea sub anakuwa mzuri ila akianza anakuwa kama kiazi, Ziyech bado hajarudi kwenye form kabla ya majeruhi, Pulisic anafight lakini mambo bado kabisa. Werner kila siku inapokucha ndio anazidi kuwa wa hovyo kabisa. Katika mechi kama tatu zilizopita na kwenda huko nyuma tatizo la Werner ilikuwa ni kosakosa kwenye kufunga, sasa tatizo lake limeongozeka hata kwenye kupasi amekuwa hajiamini, butua butua kwenye kufunga na butuabutua kwenye kutoa pasi. Tammy Abraham kama kawaida yakeanajitahidi ila uwezo wake ni mdogo, bado hajakoma kwenye Big matches. Giroud wa kawaida sana lakini kwa ukweli bado hajatumiwa kama inavyotakiwa na Lampard ni kama hana mpango naye tena anafocus kuwatumia wenye umri mdogo
- Wachezaji pekee wenye consistency ni Silva,Mount, Zouma, Mendy, Giroud**