Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Maplastic ya humu yanachekesha. Mengine yameuchuna yanazunguka zunguka tu humu kuingia hayataki.

Mengine yapo bize kusema Lampard out.

Mara Kai tumepigwa na werner ni kinabo.

Kai amegewa performance 5.9

Werner 6.5

Na Giroud 6.5

Lakini maajabu yake watu wanamlilia giroud wanaona werner kacheza makida makida.

Kuna kipindi lampard alikua anacheza 4 2 3 1. Werner akawa anacheza kama lmf mi nikasema werner hawezi onyesha potential kwa huko anapowekwa aliperform poa leipzig kwakua aliwekwa katikati na yusuf.

Hana skills za kumuwezesha kuwatoka watu so huwezi kumuweka mbali na goli. Jana kawekwa mbali na goli halafu kacheza kama rwf. Means kwa jana werner alikua ameandaliwa kutoa krosi tu.

Rwf hucheza left footed as anaweza kuassist/ cross na kuscore. Right footed ataweza kucross tu na siyo kuscore.

So kwa hiyo overall performance werner kafanya vizuri.

Tuje kwa kai. Kai ni AM una mchezaji kama huyu huwezi kumuweka mbali na forwards. Ndiyo maana katika 4 2 3 1 kai alikua anaperform vyema sana as ilikua nyuma yake kuna dmf wawili kisha yeye ni kupokea mpira kumtafuta tammy & co.

4 3 3 ya jana nafikiri ni ya kuhold angecheza 4 3 3 attacking (dmf wawili nyuma na amf) nafikiri kai angeperform poa.

Lampard siyo kocha mbaya. A guy pulled out top four huku lile gunia la misumari likionekana hakuna mwenye hamu nalo. Ni mapema sana kusema lampard ni kiazi.

Sijaangalia mpira ila ni kwa kuangalia formation na performance ratings considering previous games nilizoangalia.

Naweza kua wrong
Leo umeongea kimpira zaidi na point kubwa inaonesha wewe Ni mshabiki wa Chelsea sema umejificha kwenye koti la Arsenal ongera mzee baba
 
Leo umeongea kimpira zaidi na point kubwa inaonesha wewe Ni mshabiki wa Chelsea sema umejificha kwenye koti la Arsenal ongera mzee baba
We jamaa bwana.

Ukienda kwenye kila uzi utakuta naandika vitu kama hivyo. Kasoro nyuzi za city na tottenham as sijui kama zipo.
 
Hizo pass za haraka mbona hazionekani sasa? Jana nimeona pass za kinyonge zinaishia njiani, zinapotea, nyingi ni pass za nyuma kuliko kwenda mbele.

Hii style ya pasi ibadilishwe haina manufaa yoyote tunatumia wiki nzima kufika lango la mpinzani, tuje na approach nyingine iwe ya pasi 2 au tatu tumeshafika goli la mpinzani.

Tunao viberenge Werner + Pulisic watangulizie pass mbele wachanje mbuga.

Mbona zipo style nyingi za uchezaji Lampard asiwe jiwe abadilike
Kawa jiwe na Chelsea ndio hiyo inaachia ngazi taratibu
 
Ni jambo la kushanga sana. Safari hii bingwa wa ligi hakuna mwenye uhakika kukibeba.
Mwaka jana Liver mechi 38 kapoteza pts 15 tu
Mwaka huu mechi 13 kashapoteza pts 11, Ligi mwaka huu ubingwa ngoma nje nje
 
Mashabiki tunakuwa na hasira mwisho wa siku tunapoteza focus halisi ya tatizo.

Ukweli lazima ubaki kuwa ukweli, timu zetu hizi tatu Manchester United, Chelsea na Arsenal zina makocha wanaojifunza kuongoza timu kubwa na zenye pressure ya mashabiki. Kwa kifupi timu hizi ni kubwa sana kuliko uwezo wao.
Big point
 
hapo kwa ole kama atashindwa kujijenga muda huu sidhani kama ataweza kuwa mwalimu bora hapo mbeleni akielekea miaka 50, baada ya kustahafu soka alianzia career yake ya ukufunzi pale united reserve team, baadae akaelekea cardiff na molde na zote hizo ni timu ndogo sana kipresha,

kivyoyote bwana huyu alikuwa na muda mzuri sana wa kujijenga professional kwenye hiyo career yake ya ufundishaji huko alikotkea, now yupo united timu inayompa kila kitu anachokihitaji na still ameshindwa kudeliver matokeo bora na soka bora ndani ya uwanja licha ya uzoeefu aliokuwa nao, kibaya zaidi timu anayofundisha inamfanya muda wote awe na presha kubwa sana inayochangizwa na uhitaji wa matokeo bora yatakayoweza kurudisha morali ya ushindani wa makombe.

media zinamuandama, mashabiki wanamuandama, wawekezaji wanamuangalia yeye na huku umri ukiendelea kumtupa kwa sababu ana miaka 48 na bado hajajijengea heshima inayostahili itakayozifanya timu nyenginezo washawishike kuhitaji huduma yake pindi atakapoondoka united.

kama atashindwa man utd huenda itakuwa ndio mwisho wa career yake ya ukufunzi, nani atakayemuhitaji pale pale ulaya kuu(german,england, france, spain).
=========

lampard bado anajificha kwenye kivuli cha uzoefu, baada ya kustahafu soka nakumbuka alitumia muda mwingi sana kufanya kazi ya pundit tofauti na mwenzake steven gerrard aliyeelekeza nguvu kazi kwenye fani ya ukocha.

bahati ya pili alipewa timu ya chelsea wakiwa na ban ya usajili na aliweza kuwapa tiketi ya UEFA msimu huu licha ya kwamba alikuwa akipata matokeo yasioridhisha baadhi ya nyakati, kuwapa nafasi ya UEFA akiwa na wachezaji mfano wa tomori, zouma, mount, abraham, odoi na wengineo ni tiketi nyengine inayomfanya aendelee kuaminiwa na wapiga kelele wa pale darajani.

bahati namba 3 jamaa anafundisha timu ambayo haina presha yeyote kubwa ukiachana na mzuka wa bossi kitambi abramovich, chelsea ameshapoteza mechi mbili mfululizo ila husikii legendary yeyote akimnyooshea kidole super frank, hata media za uingereza zimekuwa haziendeshi mijadala ya mara kwa mara juu yake.

kwa umri wake na cv yake ya kiuchezaji naamini anaweza kupata offer nyengine baada ya kuondoka chelsea, hivyo basi nakubaliana na wewe super frank bado ana nafasi zaidi ya kujijenga.

jana nilibahatika kuangalia mechi ya chelsea
  • lampard huongozwa na mazoea: hafanyi sub kwa sababu ya kiufundi bali huongozwa na mazoea, nimepitia forum thread nyingi za chelsea kwa kuanzia hapa mpaka reddit nipate kujifunza angalau dhumuni la kuingizwa abraham baada ya kutolewa giroud lakini hakuna aliyeweza kuja na tactical analysis yeyote.
  • timo werner ataendelea kulose possession ovyo kila mechi kama ataendelea kuchezeshwa pembeni, jamaa ni mweupe sana anapokuwa mbali ya goli. kama kocha anawajibika kumtafutia werner eneo sahihi la kiuchezaji, kule germany hakuwahi kuzipata goli 20 kwa kutokea pembeni
  • sitaki kumzungumzia kai harvetz, eneo lake sahihi linajulikana....tafuteni mechi dhidi ya crystal palace japokuwa hakuchangia goli lakini alicheza vizuri sana na ulegevu wake
  • chelsea wanapocheza na giroud mentality yao kubwa ni mpira wa krosi
  • hivyo basi chelsea wanahitaji mchezaji mwenye kuuelewa mchezo pindi wanaposhambulia, majirani zetu man city wanateseka sana kipindi hichi kumkosa mchezaji mwenye sifa hizo, miaka ya nyuma walipokuwa na mchezaji aina hiyo walitusumbua sana kupitia mfumo wao wa midfield wawili wanaoshambulia....namzungumzia mchezaji aina ya david silva au KDB.....kwetu tunao watatu wachezaji aina hiyo lakini mfundishaji anazingua....kule kwetu bruno anaweza kutengeneza open chance hadi 6 kwenye mechi moja kupitia angle tofauti lakini conversion rate ikawa 0
Uchambuzi kama huu ndio unatakiwa badala ya matusi na kashfa
 
Piga ua, Lampard yeye hajui kulinda goli kabisa na huu udhaifu ndio utamfanya ashindwe kuchukua kikombe chochote labda abadilike
 
Mkuu mbona iko open kabisa ni swala la Lampard aamue kubadilika badala ya kumuanzisha Kai amuanzishe Kovacic acheze na Mount na Kante. Hapo hakutakua na uchawi zaidi ya kusubiria uahindi na hapo mabadiliko yatakua ni madogo madogo tu.
Kai na Abraham wanatakiwa kupewa dakika chache tena kwenye mechi za mtelemko
 
Kai na Abraham kwenye kikosi cha Liverpool hawapati namba. Origi ni mzuri sana kuliko Abraham still anasugua bechi.

Pamoja na majeruhi mengi yaliyowakumba Liverpool still hawafungwi, wanatoa draw au ushindi hiyo ndio maana ya kucheza kibingwa.

Ametoa DRAW na Everton sisi tumefungwa
Amemfunga Wolves kipigo kikali sisi tumefungwa
Amemfunga Tote sisi tumetoa DRAW.

Lazima tuwatumie Liverpool kama reference ya kuwa title contender.
Vip astonvilla nao ilikuaje kwa LIVAPOOLI
 
Adjustments.jpg
 
So ulitaka kikos cha msim uliopita ndio kianze
Tomori,alonso,abraham,kepa,rudiger,azplicueta ndio kikosi kilichocheza msim uliopita hicho

Au point yako ni ipi hapo??
We jamaa kila kitu huwa unatetea, Lampard ni mpuuzi. Yaani kocha yeye yupo yupo tu amekariri sub mpk dk.70 ndio afanye sab. haijalishi kama mchezaji kaboronga au vipi. Na sub zake ni atoke Girod aingie Abraham, au abraham ainge Giroud. Na nyingine Atoke Havertz aingie Kova au Kova aingie Havertz basiii amemaliza.
 
We jamaa kila kitu huwa unatetea, Lampard ni mpuuzi. Yaani kocha yeye yupo yupo tu amekariri sub mpk dk.70 ndio afanye sab. haijalishi kama mchezaji kaboronga au vipi. Na sub zake ni atoke Girod aingie Abraham, au abraham ainge Giroud. Na nyingine Atoke Havertz aingie Kova au Kova aingie Havertz basiii amemaliza.
lampard,ole,arteta wote wapo sawa tu
wanachofanya wanapeana mda wa kutuumiza mashabiki(maumivi per wik)
akiianza artetaa atafanya vibayaa wa wik kadhaaa then kijiti anampa ole kikitoka hapo kinaenda kwa lampard na cycle restarts.in short hawafaii kwa hiz timu kubwa
kwa msimu ulioisha wote watadai wamepata mafanikio ole na lampard kufuzu uefa,arteta kuchukua fa
wakati sio vitu vya kujisifia kwa hiz timu kubwa kabisaa
 
Mkuu, uhalisia uko hivi.
Chelsea imeanza kuvuna mashabiki (kwa hapa Tanzania) mwaka 2005.

Wengi wa mashabiki ni masalia wa Liverpool walio kata tamaa na timu yao.

Kuanzia msimu wa 2005 watoto wadogo (wajomba zetu) wengi walianza kuishabikia Chelsea, wengi wao ni waliozaliwa 1993+ .

Kwahiyo usitegemee ushabiki wa heshima kutoka kwa watoto wa lika hilo.
Ukiingia uzi wowote wa mpira ukakuta matusi ni shabiki wa chelsea ndiye atakua anatukana watu.
 
ni suala la mda tu sio kwa msimu huu ligi ngumu sana

Mkuu kama sasa hivi hafungwi atafungwa lini ?maana sasa Hivi wana injury Za hatari lakini bado wanaongoza ligi.

Kama unafatilia vizuri ligi sio ngumu kwa liverpool,kilichotokea liverpool kikosi chao asilimia kubwa wachezaji wao wanaumia na wengine wameumia beki ya kati yote ya Liverpool ina injury safu inaongozwa na Fabinho ambae yeye namba yake ni kiungo wa kati. Na jana kuna dogo William kacheza beki ya kati kutoka timu ya watoto amecheza ndio mechi yake ya kwanza kwenye Epl lakini bado tumepata matokeo

Sasa wakirudi wote tuliowazoe wakina Thiago,vvd,Jota,Gomez, na wengine Fabinho akisogea mbele pale sijaona timu ya kumfunga liverpool pale anfield.
 
Mkuu kama sasa hivi hafungwi atafungwa lini ?maana sasa Hivi wana injury Za hatari lakini bado wanaongoza ligi.

Kama unafatilia vizuri ligi sio ngumu kwa liverpool,kilichotokea liverpool kikosi chao asilimia kubwa wachezaji wao wanaumia na wengine wameumia beki ya kati yote ya Liverpool ina injury safu inaongozwa na Fabinho ambae yeye namba yake ni kiungo wa kati. Na jana kuna dogo William kacheza beki ya kati kutoka timu ya watoto amecheza ndio mechi yake ya kwanza kwenye Epl lakini bado tumepata matokeo

Sasa wakirudi wote tuliowazoe wakina Thiago,vvd,Jota,Gomez, na wengine Fabinho akisogea mbele pale sijaona timu ya kumfunga liverpool pale anfield.
Huo huwa tunauita utabili wa hali ya hewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom