Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa

NINA UHAKIKA MKUBWA KABISA KWENYE HOTUBA YAKE LEO RAIS ATASHINIKIZA SPIKA AENDELEE KUWA MBUNGE NA BAADAYE SPIKA WA BUNGE LIJALO ......ILE KUAGA JANA ILIKUA SEHEMU YA MCHEZO
 
nimeufurahia sana utawala huu wa awamu 5, fumba na kufumbua miaka 5 imekatika!! hii ni kutokana na aina ya kipekee ya uongozi wa Rais Magufuli, kasi yake ya kuleta maendeleo imefanya siku ziwe chache! ndio maana nadhani hata miaka mitano tutakayo mpa tena octoba 2020 bado .....lkn tunamuombea kwa Mungu ampe afya na uzima akamilishe malengo aliyo yakusudia kwa watanzania.
Mungu mlinde Rais wetu huyu ambaye ni zawadi ya watanzania
 
Leo tarehe 16 Juni 2020, Rais Magufuli analivunja bunge kwa ajili ya kufanya matayarisho ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, ambapo uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika kwa wakati mmoja.

Bunge la 11 lilifunguliwa na Rais Magufuli Novemba 20, 2015 baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tutawaletea kile kinachojiri kutoka bungeni.

FUATILIA:



UPDATES:
Marais Wastaafu, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu Dr Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu Dr Gharib Bilal wakiwa Bungeni mjini Dodoma wakisubiri kusikia hotuba ya kulivunja Bunge Leo kutoka kwa kwa Rais Dk John Magufuli


09:24am - Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wameshafika katika Ukumbi wa Bunge na pia wapo Viongozi wa zamani

09:36 Rais Magufuli awasili kwenye viwanja vya Bunge, akaribishwa kwa Wimbo wa Taifa na kukagua Gwaride Maalum

09:49 Rais Magufuli aingia Bungeni kusaini kitabu cha wageni

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu hili ndio bunge bovu na la kijinga lililo na spika duni kuliko mabunge yote duniani kwa sasa
 
Rais tayari kaweka saini kwenye miswada yote hivyo tayari zimekuwa sheria
 
Ndugai anataja miswada 60 iliyopitishwa na kuwa sheria baada ya Rais kweka sahihi kuwa sheria
 
Back
Top Bottom