Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia, wastani wa Shilingi Bilioni 20 zimekuwa zikitolewa kila mwezi kwenda MSD

Irene Darton

Member
Feb 25, 2024
18
21
1. Ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika maeneo mbalimbali nchini yamewezesha Vituo vya kutolea huduma za Afya kuongezeka kutoka vituo 8,549 Mwaka 2021 hadi vituo 9,610. Hii ni pamoja na Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa, Kanda, Maalum na Taifa.

2. Ununuzi wa vifaatiba vya kisasa vya Uchunguzi wa Magonjwa mbalimbali ikiwemo;-

✅MRI kutoka 7 mwaka 2021 hadi 13 mwaka 2024

✅CT-Scan kutoka 13 Mwaka 2021 hadi 45 mwaka 2024

✅Digital X-RAY kutoka 147 mwaka 2021 hadi 346 mwaka 2024

✅Ultrasound kutoka 476 mwaka 2021 hadi 668 mwaka 2024

✅Echocardiogram kutoka 95 mwaka 2021 hadi 102 mwaka 2024

✅Cathlab kutoka 1 mwaka 2021 hadi 4 mwaka 2024

✅Pet Scan imenunuliwa 1 ambayo awali haikuwepo.

3. Idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini imeongezeka kutoka vitanda 86,131 mwaka 2021 hadi vitanda 126,209 Machi 2024.

✅Aidha idadi ya vitanda kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU) katika vituo vya umma imeongezeka kutoka vitanda 258 vya mwaka 2021 hadi kufikia vitanda 1,362 mwaka 2023.

4. Hali ya upatikanaji wa dawa na bidhaa za Afya inazidi kuimarika. Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia, wastani wa Shilingi Bilioni 20 zimekuwa zikitolewa kila mwezi kwenda MSD na hivyo kuwezesha Upatikanaji wa dawa muhimu na bidhaa nyingine za afya (aina 290) katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma kufikia asilimia 84 mwaka 2023, ikilinganishwa na asilimia 58 mwaka 2022.

#MguuKwaMguu2025 #MiakaMitatuYaRaisSamia
 
Back
Top Bottom