Binti wa dukani alitafutiwa kazi hii kwa taabu sana ila cha ajabu hajamaliza hata mwaka ana mimba, Ntalaumiwa nikiweka binti mwengine?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Binti alifika dukani mwezi wa kwanza mwaka huu, Ni binti ambae sijawahi kuwa na tatizo nae kasoro hivi karibuni

Siku ya ambayo duka halifunguliwi / mapumziko huwa ni Jumapili lakini kwa sasa hali imebadilika, Kwa takribani wiki 5 mfululizo zilizopita ni lazima siku moja wapo kati ya Jumatatu hadi Ijumaa hafungui duka mara aniambie kichwa kinauma, msiba, homa, usafiri, n.k. ila kuna taarifa nikapata huwa anaenda kliniki, mimba iliyoanza kuonekana kwa mbali imethibitisha hii taarifa.

Tatizo sio mimba bali ni kutofungua duka siku ambazo sio za mapumziko anaenda clinic ama kutokuja kwa sababu zengine ambazo zinahusiana na hio mimba.

Binafsi nina kazi nyingine huwa namuachia duka, baadhi ya siku za jioni naenda kuhesabu mzigo na kukagua hesabu, hivyo akiwa hayupo duka linafungwa.


Sasa nawauliza,

Je, Kiuhalisia binti wa dukani anaweza kuendelea na kazi zake bila kushuka uwezo wake wala mambo yake binafsi kuingilia mambo ya ofisi akiwa na mimba?
 
Kupata mimba sio kosa,
Ila duka kufungwa kila mara ni tatizo..
Zungumza nae,mpe mapumziko siku ya clinic.
Mkishindwana tafuta mwingine.
 
Binti alifika dukani mwezi wa kwanza mwaka huu, mshahara laki na nusu, allowance elf 4 kila siku, mkoani.

Kwa takribani wiki 5 mfululizo zilizopita ni lazima siku moja wapo kati ya Jumatatu hadi Ijumaa hafungui duka (Jumapili ni siku ya mapumziko), alikuwa anazuga kichwa kinauma mara msiba mara homa, n.k. ila kuna taarifa nikapata huwa anaenda kliniki, mimba iliyoanza kuonekana kwa mbali imethibitisha hii taarifa.

Binafsi nina kazi nyingine huwa namuachia duka, baadhi ya siku za jioni naenda kuhesabu mzigo na kukagua hesabu, hivyo akiwa hayupo duka linafungwa.

Sasa nawauliza,

Je, Kiuhalisia binti wa dukani anaweza kuendelea na kazi zake bila kushuka uwezo wake wala mambo yake binafsi kuingilia mambo ya ofisi akiwa na mimba?
Mkuu huwa mnafuata taratibu za ajira au mnajiendea tu?

Ukiajiri mtu kwako haruhusiwi kupata haki yake ya msingi kama sex?

Huyo ni binadamu heshimu haki zake, jambo la msingi asikiuke makubaliano.

Kama akiwa mgonjwa hutamruhusu akatibiwe?
 
uwezo wake wa kazi utashuka mara dufu.. mimba bado Changa tu hafungui duka siku5 huoni anakutia hasara?
 
Back
Top Bottom