Rais Samia ana uwezo wa kununua hata helikopta yake binafsi kwa hela yake mwenyewe kutokana na kufanya kazi kwa miaka mingi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeamua nitoe darasa dogo hapa la elimu kwa watanzania wenzangu wenye mawazo ya kijima. Katika kampeni za 2015 hayati Edward lowassa aliyekuwa mgombea wa CHADEMA alisema yeye kipaombele chake ni Elimu,Elimu ,Elimu. Aliongeza pia kuwa anauchukia sanaaa umaskini. Lakini nimegundua na kuelewa kuwa CHADEMA na vijana wake hawakuelewa kwanini mgombea wao wa kukodi alisema hivyo.

Kwa hakika Elimu ya utambuzi inahitajika sana kwa watanzania,maana inaonyesha wengine pamoja na kuwa wamekwenda shule lakini bado ujinga haujawatoka kabisa katika vichwa vyao ,bali ndio ujinga umeongezeka zaidi kana kwamba walikwenda shuleni kusomea ujinga kwa miaka yao yote.

Hii ni baada ya kuona CHADEMA na vijana wake eti wanashangaa saa ya Mh Rais na kuanza kuweka bei zao na kipi hela hiyo ingefanya. Hivi ndugu zangu ni saa ya bei gani ambayo Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania anaweza akashindwa kuinunua kwa pesa yake binafsi inayotokana na malipo ya mishahara yake iliyopo kisheria tokea alipoanza utumishi wa umma? Mfano tu mwaka 2020 kwa mujibu wa John Heche wa CHADEMA alisema kuwa wabunge walipewa kiinua mgongo cha millioni 272. Hapo bado hajaweka mishahara aliyokuwa anatunza pamoja na posho mbalimbali za vikao bungeni pamoja na vile vya kamati na ziara zake.

Je, yeye Mheshimiwa Rais ambaye alikuwa ni makamu wa Rais alipata kiinua mgongo cha shilingi ngapi ambayo ni haki yake? Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania amepata viinua mgongo mara ngapi vya ubunge na kama waziri? Kwa sababu bunge la 2015 na hata 2010 alikuwepo. Sasa iweje leo hii ushangae saa ya mheshimiwa Rais na kuanza kusema mara zingejenga madarasa kadhaa . tangia lini mshahara wa mtu binafsi ukawa wa kujengea madarasa? Yaani yeye afanye kazi kwa jasho halafu aje akujengee wewe madarasa ya watoto wako ambaye wewe unakataa hata kuchangia hata mahindi tu debe moja kwa nusu muhula ili mwanao ale chakula au uji au Kande akiwa shuleni?

Nani kutoka CHADEMA aliyetumia kiinua mgongo chake au mishahara yake kujengea madarasa? Nani kutoka CHADEMA au yeyote yule anayehoji amewahi kuchukua mshahara wake ukawa mali ya umma ambao anapaswa kupangiwa matumizi yake? Tangia lini kipato cha mtu binafsi kikawa na masharti ya namna ya kutumia? Yaani kazi afanye mwingine halafu matumizi apangiwe na mwingine? Hivi huu siyo ukichaa kweli? Siyo uwendawazimu huu? Siyo kukosa akili na kuwa na mawazo ya kijinga na kimaskini haya? Siyo kukosa afya ya akili huku? Yaani mshahara wa mtu alioutolea jasho lake na maumivu yake aanze kupangiwa na watu namna ya kutumia? Kwamba asinunue atakacho na kupenda? Faida yake ni nini sasa ya kufanya kazi?

Kwanini watanzania tunakosa akili kiasi hiki? Hoteli ya sugu pale Mbeya Desderia ina thamani ya shilingi ngapi? Si amejenga kutokana na pesa alizopata kutoka bungeni? Je nani alitangulia kuwepo bungeni kati ya Mheshimiwa Rais na sugu? Sasa iweje leo kiongozi kama Rais ambaye amepita hatua zote na ngazi zote za uongozi mpaka kufika ofisi kuu kuliko zote ashindwe kununua kwa pesa yake saa ya mkononi?

Yaani wasanii na watoto wa majuzi kama Diamondi au harmonize waweze kufanya hivyo ndio iwe kwa Rais? Kwanini tunakuwa na mawazo ya kimaskini kiasi hiki watanzania? Kwanini tunakuwa na mawazo ya kichawi hivi watanzania? Mawazo haya hayawezi kutupeleka kwokwote na popote kule zaidi ya kubakia maskini wa akili na kipato. Ili uwe tajiri fanya kazi kwa bidii, juhudi, maarifa na kujituma kwa hali ya juu sana.usichague kazi bali fanya kazi yoyote ile ilimradi haivunji sheria na ni halali mbele ya sheria na mbele za Mungu.

Wivu wa kijinga huu ndio umetawala hata katika jamii yetu ambapo mtu anaona wivu hata akisikia tu mtoto wa jirani yake kaolewa au kapata kazi ya ualimu huko namtumbo au Mbozi. Au kaona jirani kajenga nyumba na kuezeka bati la msauzi au kafungua duka au kanunua gari au pikipiki au kapika nyama au kapaka rangi nyumba yake au anasomesha mtoto chuo kikuu. Tumejaa roho za wivu tu na kijinga jinga tu.ndio maana wengi hatuendelei na kupiga hatua maana mioyo yetu imejaa wivu na roho mbaya ,chuki na vinyongo vya kijinga.

Mtu akiendelea na kupiga hatua za kimaendeleo utasikia mara huyu saizi ni Freemason au mara amebeba nyota za wenzake au ni mchawi au ni mwizi au ni fisadi .yaani tunakuwa na mawazo ya kijinga na kimaskini maskini tu yakufurahia mtu anapopata mateso na shida katika maisha yake. Ndio maana siyo ajabu unakuta mtu hana kitu ila anafurahia sana mtu wa jirani yake au rafiki akifirisika au akipoteza kazi au gari lake likipata ajali na kuharibika kabisa, bila kujua kuwa huyo ndiye angekuwa mtu wa kwanza kuja kumbeba usiku akiwa na mgonjwa au mjamzito.au hata kumkopesha pesa ili mwanae aende hospitali kupata matibabu.

Rais Samia anao uwezo hata akitaka kununua helikopta anaweza kufanya hivyo kwa pesa yake binafsi bila shida yoyote ile.pia lazima ifahamike kuwa Rais anao uhuru wa kujinunulia na kuvaa chochote kile alichojinunulia kwa pesa zake mwenyewe bila shida.lakini pia ifahamike ya kuwa mshahara wa Mheshimiwa Rais siyo wa kujengea madarasa au kujengea zahanati au vituo vya afya au barabara. Hivyo vyote vitafaywa kwa kodi zetu wenyewe watanzania tunazopaswa kulipa kisheria.akifanya kutoa hela yake mfukoni kumsaidia mtu kupata matibabu au kumnunulia mtu cherehani au kumpa mtu mtaji Ni kwa hiyari yake ,upendo wake ,ukarimu wake ,utu wake na siyo kwamba ni lazima afanye hivyo.

Mbona wapo watu wapo mitaani wana mapesa wana kula wanasaza na kutupa vingine majalalani huku kwa jirani watoto wanalala na njaaa? Hamjaona wengine wanaagiza magari mapya ya kutembelea huku wewe jirani hapo hapo umelala ndani mwako huna pesa hata ya panadol?

Watanzania tupendane , tuombeane mazuri,tubarikiane, tushikamane,tuinuane na kugusa maisha ya watu pale tunapokuwa na nafasi,tuwe wenye huruma,upendo,ukarimu, unyenyekevu na utu.tuache wivu na mawazo ya kimasikini.hatuwezi kubarikiwa kama tukiwa na mawazo na roho za kwanini hata siku moja.anayetoa na mpaji ni Mungu Pekee, kwa hiyo usimuonee wivu wala kumpiga Majungu yule aliyepewa kwa leo.wewe kaa sali ,omba ,fanya kazi kwa bidii ili na wewe kesho Mungu aguse maisha yako na kuleta nuru ndani ya kaya yako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
IMG-20240206-WA0025.jpg
 
Ndugu admini helkopta atanunuwa aniapeleka wapi watu watasema kataifisha mkuu watu hwatamuelewa kazi nyingi ni zake siyo zetu
 
Kabla hujahoji mali za mtu inapaswa umjue huyo mtu utafutaji wake ukoje

Mama samia amewai kuwa makamu wa rais . Je mshahara na posho za makamu wa rais ni ndogo ?

Mama samia amewai kuwa waziri miaka kibao , je mshahara wa waziri ni mdogo
?

Mama samia amewai kuwa mbunge miaka kibao, je mshahara wa mbunge ni mdogo ?

Mama samia amewai kufanya kazi Taasisi za kimataifa miaka kibao, je mshahara na posho wa hizo multinational ni mdogo?

Mama samia ni Rais kwa sasa , je mshahara na posho za rais ni ndogo ?
 
Kabla hujahoji mali za mtu inapaswa umjue huyo mtu utafutaji wake ukoje

Mama samia amewai kuwa makamu wa rais . Je mshahara na posho za makamu wa rais ni ndogo ?

Mama samia amewai kuwa waziri miaka kibao , je mshahara wa waziri ni mdogo
?

Mama samia amewai kuwa mbunge miaka kibao, je mshahara wa mbunge ni mdogo ?

Mama samia amewai kufanya kazi Taasisi za kimataifa miaka kibao, je mshahara na posho wa hizo multinational ni mdogo?

Mama samia ni Rais kwa sasa , je mshahara na posho za rais ni ndogo ?
Lakini awezi kununua helkopta binafsi akaiendesha kwa pesa zake….
 
Back
Top Bottom