Madaktari wetu hasa nyie vijana wa sasa mjitafakari sana utendaji kazi wenu!

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,

Hiki kisa nimekutana nacho sio siku nyingi.

Huyu dada alikuwa anafanya kazi mahali fulani, sasa katika majukumu yake akakutana na mteja(Mzee) ambaye hufika hapo kupata huduma.

Mzee akaanza kumtaka kimapenzi huyo dada lakini kwa maelezo ya huyo dada akawa akimzungusha muda mrefu,sasa kwakuwa huyo mzee yupo huu mkoa kikazi kwa miezi kadhaa huwa anaenda hapo mara kwa mara baada ya shughuli zake.

Sasa huyu dada sikuhio akawa amemkubalia na baada ya kazi waende kwa kwahuyo mzee kufanya yao,katika process za anasema condom ilipasuka.

Sasa asubuhi wakati huyu dada anataka kuondoka aliona kopo fulani la dawa ambalo alilitilia mashaka,akamuuliza Mzee akasema kwamba hilo kopo ni la rafiki yake ameweka tu humo kwake,sasa akamuuliza iweje rafiki rafiki yako aweke dawa zake humu na yeye ana chumba chake na vinakaribiana tu,hakupata majibu ya kujiridhisha hivyo akaingia wasiwasi sana,akamwambia kama vipi itabidi wakapime afya zao,yule mzee alikubali ila akasema Itabidi iwe baadae akishatoka kazini.

Basi wakaachana kwamba badae akirudi waende kupima afya,ila huyu dada akili yake haikutulia akaona apite Kituo cha afya binafsi(cha dini)kuuliza jambo.

Alipofika akaonana na daktari fulani kijana akamueleza ilivyokuwa ila akamwambia lile kopo la dawa liliandikwa LA 75,ila alishindwa kuchukua kidonge mle,cha kushangaza daktari kamwambia eti kalete kopo lake tuone ndio tutajua ni dawa gani,dada akamwambia kwa namna ilivyokuwa isingewezekana mimi kuchukua hata kidonge achilia mbali kopo ila maandishi yaliyoandikwa kwenye vidonge ameyashika vizuri ni LA 75 anaomba ajue ni za nini? akaambiwa eti sio rahisi kujua kwa kutaja maandishi ya kidonge tu labda apate kopo.

Sasa yule dada akaondoka hapo hospitali kachanganyikiwa zaidi kuelekea nyumbani,sasa wakati anapita akaniona nimekaa duka la dawa nje,mhusika alitoka(akaniachia kwa muda).

Alipofika jinsi tu alivyokuwa anapumua nikajua atakuwa na shida,akaniambia kaka naomba nisaidie,akanieleza kisa kizima na jinsi alivyojibiwa pale hospitali,Sasa kwa tukio lile na mimi nikawa na tahadhari,nikawambia una uhakika kiliandikwa hivyo akasema anauhakika,ukweli kile kidonge mimi nilikuwa sikijui,nikaamua niingie tu google nikaingiza ''LA 75 tablet uses",majibu yake yalinishtua sana,wakati huo yeye anajipepea huku akiniuliza vipi umepata jibu,ukweli jibu nilishalipata ila nikawambia bado ili nijue namwelezaje,nikatafuta tena ili nijiridhishe,nikamkaribisha kiti akae kwamba bado natafuta(kumbe najipanga).

Akaanza kusisitiza niambie tu kama umepata,ikabidi nimwambie''matokeo
yanaonyesha ni dawa ya kutibu watu wenye HIV lakini subiri nipate uhakika kwanza lakini majibu ya mwanzo ndio hayo Du! alichoka yule dada hadi nikamhurumia,akasema "nimeisha halafu nilimnyonya hadi mb..."

Ikabidi nimpigie dada mmoja ni muuguzi nikamwambia niambie hizo dawa unazijua?,akasema sizijui ngoja nimuulize Mfamasia hapa,mfamasia akasema hizi code huwa kila moja ina kazi yake kwahio mpaka amsubiri sijui nani amuulize nikaachana nao,nikampigia muuzaji wa duka la aliyeniachia nikamweleza tukio akasema ngoja acheki na dokta mmoja mzoefu,baada ya muda akanirudia akasema hizo dawa ni kwa ajili ya wagonjwa wa UKIMWI na ni zile kali wanaita second line,yaani kama mgonjwa alipewa dawa za ARV halafu hazionyeshi matokeo basi ndio anaanzishiwa hizi dawa.

Sasa hapo ikabidi nimpe ukweli tu jinsi ulivyo lakini nikamwambia bado anaweza kujikinga asiambukizwe kwakua yuko ndani ya saa 72,kwahio tukakubaliana aende nyumbani kujiandaa baada ya muda anikute pale ili nimpe maelekezo ya namna ya kufanya,kwa jinsi alivyokuwa hajatulia anataka kukojoa pembeni ya duka na lipo barabarani bajaji zinapita hapo,ikabidi nimwambie choo kipo nikampa funguo akaenda kujisitiri.

Baada ya muda alirudi akanikuta nipo na muuza duka tukampa maelezo aende hospitali ya Mkoa akawaeleze hali halisi watampa dawa za kujikinga ambazo atakunywa kwa mwezi mzima(PEP).

Kweli alienda akatoa maelezo wakampima kama hakua na HIV kabla,wakakuta negative wakampa vidonge,akapita pale kushukuru angalau akili ilishakaa sawa japo alikuwa haamini kama dawa anazomeza zitamuokoa,yule mpenzi wake hata simu zake ikawa hapokei tena inaita tu(kumbuka walikubaliana kwenda kupima wote).

Baada ya mwezi mmoja alimaliza zile dawa japo kwa taabu maana anaishi na mama yake na hakutaka ajue na anasema ni dawa kali na alipopimwa akakuta hana maambukizi yeyote, alinitafuta kunishukuru,alikuwa na furaha sana,akaniletea na hela ya soda akasisitiza sana niichukue,nilichoshukuru ni kwamba niliweza kumtoa kwenye lile janga,Ila alichosema yeye mwenyewe kwa mdomo wake ni kwamba anahisi yote haya ni Mungu amemuonya ili abadilike kwahio akasema hatarudia tena kufanya ujinga,kama akipata mtu awe ni wa kumuoa na wapime kwanza.

Yule Mzee hakuwahi kupokea tena simu yake na alishaondoka pale,inaonekana alishamaliza kazi iliyomleta pale.

Sasa nikajiuliza hivi yule daktari alishindwa nini kumsaidi huyu dada?ina maana kwa mtandao wake na wenzake alishindwa kweli kupata jibu akamsaidia mtu asiathirike na HIV?alishindwa hata ku-google?Yaani huyu dada ilikuwa ateseke maisha yake yote sababu ya daktari mmoja kutojali,au ndio matumizi mabaya ya akili?

Kweye Kichwa cha uzi nimewataja madaktari vijana ili waone hili tukio,na sio hili pekee mimi mwenyewe nimeshakutana na matukio kadhaa ya hawa madaktari vijana mpaka mtu unajiuliza kama daktari kapita chuo kweli?na pia nimesikia malalamiko ya wengi tu kuwahusu.

Mfano wa kwanza, miezi kadhaa nilimsindikiza mzee wangu kupatiwa tiba ya tezidume,alikuwa na appointment na daktari,huyu Dokta kasoma Ulaya,mzee alishafanyiwa operation ya kwanza ile ya kukwangua(hawapasui)hospitali moja Dar mwaka Jana,ila akaanza kusumbuliwa tena,ikaonekana uvimbe umerudi tena,ndio akapata connection na huyu Daktari, Huyu Dokta anatumia njia tofauti,hafanyi operation ila anaingiza catheter mpaka kwenye tezi (trans urethral)halafu anaingiza dawa kuyeyusha na halirudi tena,kinachofuata ni kukojoa tu mikojo ya ule uchafu kutoka, huku ukitumia dose na kupumzika hospitali kwa siku kadhaa,hakuna maumivu wala vidonda.Sasa dokta anashangaa kwanini watu wanaendelea kupasuliwa wakati hizi procedure rahisi zipo kwenye vitabu?anasema huko kwenye hospitali nyingi anakozunguka kufanya hii procedure kwa wagonjwa wake anakutana na kesi ya akina mama wajawazito kupasuliwa hovyo bila sababu kabisa,anasema mtu kachelewa kidogo tu kujifungua dokta anasema aandaliwe kufanyiwa operation,anasema ameshaokoa kina mama wengi kufanyiwa operation bila sababu na wakajifungua salama kabisa,sasa unaweza ukaona jinsi hali ilivyo.

Mfano wa pili,niliwahi kumpeleka mtoto alikuwa anahoma,hana hamu ya kula na anatapika,sasa nikamkuta dokta kijana tu nikamweleza,wakati namweleza yeye anaitikia tu huku anajaza vitu kwenye PC,baada ya dakika chache akasema nenda maabara,kufika maabara mtoto akapimwa Choo, mkojo na damu,majibu yalipotoka hana ugonjwa,tukarudi kwa yule dokta akasema mtoto hana shida labda mabadiliko ya hali ya hewa tukapewa dawa za maumivu tukaondoka japo sikuridhika, kufika nyumbani mtoto bado anachemka,ikabidi kesho turudi tena palepale, safari hii nikamkuta mzee mmoja(Clinical officer),kwanza akampakata mtoto yeye mwenyewe,wakati namueleza yeye anamkagua mtoto, joto la mwili baadae akambembeleza afungue mdomo,ndio akajua kumbe mtoto ana matezi, sasa unaweza ukaona hata utofauti na namna huyu dokta na yule wa jana yake,yule hata kusikiliza tu Ilikuwa shida.

Mwisho,Nawapongeza sana madaktari vijana na wazee wanaofanya kazi kwa weledi mkubwa kuisaidia jamii katika hali zote vijijini na mijini ila wapo waoharibu hii tasnia hasa vijana na wanafanya madaktari vijana waonekane hawajitambui .

Nini maoni yako?

Tujitafakari katika hili.

N:B Picha sio ya mhusika.

Ahsante.

IMG_20230508_175145.jpg
1683557407574.jpg
 
Maelezo marefuuu wakati CTC pep ni buree famasia mnamatatizo gani cjui
Tatizo lako wewe unafikiria hapa naleta vita kati ya Famasia na daktari,siko katika fani yoyote katika hizo mbili

Halafu sijauliza kuhusu CTC pep mimi,nimehoji matumizi mabaya ya akili ya daktari kumtaka mgonjwa akalete kopo la dawa wakati mazingira yalikuwa hayawezekani.,

We ni dokta kijana?
 
Naelewa ila kwa scenerio hyo ilikua haihitaji hata maswali ni kuvuta test kit na kupima HIV na kumpa PEP ila huenda huyo dada hakumpa kisa kizima So DK awezi kuota tu na kuanza kufanya matibabu ,Ndio dawa zina code kama hyo Lamivudine LV,Stavudine d4T hizi zinaingiliana kuna za Watoto,Watu wazima na wamama wenye mimba n.k acha lawama
 
Analazimisha nipima kitu ambacho siumwi, mi namueleza mengine yeye anataka mengine kabisa
Hilo nalo tatizo tiba ni majadiliano baina ya daktari na mgonjwa sasa yeye anataka umsikilize yey tu
 
Kwa watoto akiwa mdogo huwa namtafuta Kubhoja alinisaidia sana.

TMJ Lab techs waoga sana kutoa damu watoto wadogo, waliwahi tupa vifaa tumpe Dr amtoe mwenyewe
 
Naelewa ila kwa scenerio hyo ilikua haihitaji hata maswali ni kuvuta test kit na kupima HIV na kumpa PEP ila huenda huyo dada hakumpa kisa kizima So DK awezi kuota tu na kuanza kufanya matibabu ,Ndio dawa zina code kama hyo Lamivudine LV,Stavudine d4T hizi zinaingiliana kuna za Watoto,Watu wazima na wamama wenye mimba n.k acha lawama
Hakuna cha huenda,lawama lazima zimuendee tu,Daktari kapewa maelezo yote ambayo mimi alinipa,kama hakupewa maelezo kwanini alimtaka akalete kopo?

Alipoambiwa kwamba kopo haliwezekani kuletwa kwanini sasa hakumpima HIV na kumpa PEP?
 
Kwa watoto akiwa mdogo huwa namtafuta Kubhoja alinisaidia sana.

TMJ Lab techs waoga sana kutoa damu watoto wadogo, waliwahi tupa vifaa tumpe Dr amtoe mwenyewe
Lab techs anaogopa kutoa damu mtoto?mbona kazi sasa
 
Kuhusu kopo la Dawa kwa kiasi kikubwa Dokta alikuwa sahihi, huwezi kusema ni dawa fulani kwa maelezo tu ya mdomo, hata bila kuona picha.

Ila kuhusu negligence ni kweli kabisa, Sekta ya Afya mtu usipokuwa makini unaweza kupoteza Ndugu kwa uzembe wa hawa wahudumu wetu.

Imekuwa ni kawaida kabisa siku hizi unamweleza Dokta tatizo lako yeye anachezea simu, ukimaliza tu kujieleza anakwambia nenda Mahabara. They don't care..

Kuna Hospitali moja kubwa sana maeneo ya Mbezi, natamani sana wahudumu wake wawe makini pale, maana uwekezeji uliofanyika pale haufanani kabisa na huduma za watendaji wake, kuanzia Mapokezi mpaka kwa Madaktari wake, full nyodo na pia kubahatisha matibabu..

Nina baadhi ya watu nawafahamu wanakwambia ukifika pale uwe na Daktari wako kabisa, kisha uombe Mapokezi wakudirect kwake. Na ukishamalizana naye Umpoze Dokta kidogo ndiyo mtaenda sawa.. Ukijiendea kikauzu kauzu utaishia kupewa huduma kikauzu kauzu hivyo hivyo..
 
Wakuu,

Hiki kisa nimekutana nacho sio siku nyingi.

Huyu dada alikuwa anafanya kazi mahali fulani, sasa katika majukumu yake akakutana na mteja(Mzee) ambaye hufika hapo kupata huduma.

Mzee akaanza kumtaka kimapenzi huyo dada lakini kwa maelezo ya huyo dada akawa akimzungusha muda mrefu,sasa kwakuwa huyo mzee yupo huu mkoa kikazi kwa miezi kadhaa huwa anaenda hapo mara kwa mara baada ya shughuli zake.

Sasa huyu dada sikuhio akawa amemkubalia na baada ya kazi waende kwa kwahuyo mzee kufanya yao,katika process za anasema condom ilipasuka.

Sasa asubuhi wakati huyu dada anataka kuondoka aliona kopo fulani la dawa ambalo alilitilia mashaka,akamuuliza Mzee akasema kwamba hilo kopo ni la rafiki yake ameweka tu humo kwake,sasa akamuuliza iweje rafiki rafiki yako aweke dawa zake humu na yeye ana chumba chake na vinakaribiana tu,hakupata majibu ya kujiridhisha hivyo akaingia wasiwasi sana,akamwambia kama vipi itabidi wakapime afya zao,yule mzee alikubali ila akasema Itabidi iwe baadae akishatoka kazini.

Basi wakaachana kwamba badae akirudi waende kupima afya,ila huyu dada akili yake haikutulia akaona apite Kituo cha afya binafsi(cha dini)kuuliza jambo.

Alipofika akaonana na daktari fulani kijana akamueleza ilivyokuwa ila akamwambia lile kopo la dawa liliandikwa LA 75,ila alishindwa kuchukua kidonge mle,cha kushangaza daktari kamwambia eti kalete kopo lake tuone ndio tutajua ni dawa gani,dada akamwambia kwa namna ilivyokuwa isingewezekana mimi kuchukua hata kidonge achilia mbali kopo ila maandishi yaliyoandikwa kwenye vidonge ameyashika vizuri ni LA 75 anaomba ajue ni za nini? akaambiwa eti sio rahisi kujua kwa kutaja maandishi ya kidonge tu labda apate kopo.

Sasa yule dada akaondoka hapo hospitali kachanganyikiwa zaidi kuelekea nyumbani,sasa wakati anapita akaniona nimekaa duka la dawa nje,mhusika alitoka(akaniachia kwa muda).

Alipofika jinsi tu alivyokuwa anapumua nikajua atakuwa na shida,akaniambia kaka naomba nisaidie,akanieleza kisa kizima na jinsi alivyojibiwa pale hospitali,Sasa kwa tukio lile na mimi nikawa na tahadhari,nikawambia una uhakika kiliandikwa hivyo akasema anauhakika,ukweli kile kidonge mimi nilikuwa sikijui,nikaamua niingie tu google nikaingiza ''LA 75 tablet uses",majibu yake yalinishtua sana,wakati huo yeye anajipepea huku akiniuliza vipi umepata jibu,ukweli jibu nilishalipata ila nikawambia bado ili nijue namwelezaje,nikatafuta tena ili nijiridhishe,nikamkaribisha kiti akae kwamba bado natafuta(kumbe najipanga).

Akaanza kusisitiza niambie tu kama umepata,ikabidi nimwambie''matokeo
yanaonyesha ni dawa ya kutibu watu wenye HIV lakini subiri nipate uhakika kwanza lakini majibu ya mwanzo ndio hayo Du! alichoka yule dada hadi nikamhurumia,akasema "nimeisha halafu nilimnyonya hadi mb..."

Ikabidi nimpigie dada mmoja ni muuguzi nikamwambia niambie hizo dawa unazijua?,akasema sizijui ngoja nimuulize Mfamasia hapa,mfamasia akasema hizi code huwa kila moja ina kazi yake kwahio mpaka amsubiri sijui nani amuulize nikaachana nao,nikampigia muuzaji wa duka la aliyeniachia nikamweleza tukio akasema ngoja acheki na dokta mmoja mzoefu,baada ya muda akanirudia akasema hizo dawa ni kwa ajili ya wagonjwa wa UKIMWI na ni zile kali wanaita second line,yaani kama mgonjwa alipewa dawa za ARV halafu hazionyeshi matokeo basi ndio anaanzishiwa hizi dawa.

Sasa hapo ikabidi nimpe ukweli tu jinsi ulivyo lakini nikamwambia bado anaweza kujikinga asiambukizwe kwakua yuko ndani ya saa 72,kwahio tukakubaliana aende nyumbani kujiandaa baada ya muda anikute pale ili nimpe maelekezo ya namna ya kufanya,kwa jinsi alivyokuwa hajatulia anataka kukojoa pembeni ya duka na lipo barabarani bajaji zinapita hapo,ikabidi nimwambie choo kipo nikampa funguo akaenda kujisitiri.

Baada ya muda alirudi akanikuta nipo na muuza duka tukampa maelezo aende hospitali ya Mkoa akawaeleze hali halisi watampa dawa za kujikinga ambazo atakunywa kwa mwezi mzima(PEP).

Kweli alienda akatoa maelezo wakampima kama hakua na HIV kabla,wakakuta negative wakampa vidonge,akapita pale kushukuru angalau akili ilishakaa sawa japo alikuwa haamini kama dawa anazomeza zitamuokoa,yule mpenzi wake hata simu zake ikawa hapokei tena inaita tu(kumbuka walikubaliana kwenda kupima wote).

Baada ya mwezi mmoja alimaliza zile dawa japo kwa taabu maana anaishi na mama yake na hakutaka ajue na anasema ni dawa kali na alipopimwa akakuta hana maambukizi yeyote, alinitafuta kunishukuru,alikuwa na furaha sana,akaniletea na hela ya soda akasisitiza sana niichukue,nilichoshukuru ni kwamba niliweza kumtoa kwenye lile janga,Ila alichosema yeye mwenyewe kwa mdomo wake ni kwamba anahisi yote haya ni Mungu amemuonya ili abadilike kwahio akasema hatarudia tena kufanya ujinga,kama akipata mtu awe ni wa kumuoa na wapime kwanza.

Yule Mzee hakuwahi kupokea tena simu yake na alishaondoka pale,inaonekana alishamaliza kazi iliyomleta pale.

Sasa nikajiuliza hivi yule daktari alishindwa nini kumsaidi huyu dada?ina maana kwa mtandao wake na wenzake alishindwa kweli kupata jibu akamsaidia mtu asiathirike na HIV?alishindwa hata ku-google?Yaani huyu dada ilikuwa ateseke maisha yake yote sababu ya daktari mmoja kutojali,au ndio matumizi mabaya ya akili?

Kweye Kichwa cha uzi nimewataja madaktari vijana ili waone hili tukio,na sio hili pekee mimi mwenyewe nimeshakutana na matukio kadhaa ya hawa madaktari vijana mpaka mtu unajiuliza kama daktari kapita chuo kweli?na pia nimesikia malalamiko ya wengi tu kuwahusu.

Mfano wa kwanza, miezi kadhaa nilimsindikiza mzee wangu kupatiwa tiba ya tezidume,alikuwa na appointment na daktari,huyu Dokta kasoma Ulaya,mzee alishafanyiwa operation ya kwanza ile ya kukwangua(hawapasui)hospitali moja Dar mwaka Jana,ila akaanza kusumbuliwa tena,ikaonekana uvimbe umerudi tena,ndio akapata connection na huyu Daktari, Huyu Dokta anatumia njia tofauti,hafanyi operation ila anaingiza catheter mpaka kwenye tezi (trans urethral)halafu anaingiza dawa kuyeyusha na halirudi tena,kinachofuata ni kukojoa tu mikojo ya ule uchafu kutoka, huku ukitumia dose na kupumzika hospitali kwa siku kadhaa,hakuna maumivu wala vidonda.Sasa dokta anashangaa kwanini watu wanaendelea kupasuliwa wakati hizi procedure rahisi zipo kwenye vitabu?anasema huko kwenye hospitali nyingi anakozunguka kufanya hii procedure kwa wagonjwa wake anakutana na kesi ya akina mama wajawazito kupasuliwa hovyo bila sababu kabisa,anasema mtu kachelewa kidogo tu kujifungua dokta anasema aandaliwe kufanyiwa operation,anasema ameshaokoa kina mama wengi kufanyiwa operation bila sababu na wakajifungua salama kabisa,sasa unaweza ukaona jinsi hali ilivyo.

Mfano wa pili,niliwahi kumpeleka mtoto alikuwa anahoma,hana hamu ya kula na anatapika,sasa nikamkuta dokta kijana tu nikamweleza,wakati namweleza yeye anaitikia tu huku anajaza vitu kwenye PC,baada ya dakika chache akasema nenda maabara,kufika maabara mtoto akapimwa Choo, mkojo na damu,majibu yalipotoka hana ugonjwa,tukarudi kwa yule dokta akasema mtoto hana shida labda mabadiliko ya hali ya hewa tukapewa dawa za maumivu tukaondoka japo sikuridhika, kufika nyumbani mtoto bado anachemka,ikabidi kesho turudi tena palepale, safari hii nikamkuta mzee mmoja(Clinical officer),kwanza akampakata mtoto yeye mwenyewe,wakati namueleza yeye anamkagua mtoto, joto la mwili baadae akambembeleza afungue mdomo,ndio akajua kumbe mtoto ana matezi, sasa unaweza ukaona hata utofauti na namna huyu dokta na yule wa jana yake,yule hata kusikiliza tu Ilikuwa shida.

Mwisho,Nawapongeza sana madaktari vijana na wazee wanaofanya kazi kwa weledi mkubwa kuisaidia jamii katika hali zote vijijini na mijini ila wapo waoharibu hii tasnia hasa vijana na wanafanya madaktari vijana waonekane hawajitambui .

Nini maoni yako?

Tujitafakari katika hili.

N:B Picha sio ya mhusika.

Ahsante.

View attachment 2615354View attachment 2615355
Mimi kama Daktari nakubaliana na wewe, hata tasnia nzima ya afya inakubali kuwa fani imevamiwa Kwa sehemu kubwa kimaadili na kitaaluma.
 
Back
Top Bottom