Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,202
- 7,193
Jumanne, Agosti 22, 2023
Benki kuu ya Tanzania BoT imesema akiba ya fedha za Kigeni hadi jana ilikuwa Dola za Marekani bilioni 5.41 ambacho kinatosha kuagiza bidhaa za nje kwa miezi minne na siku 27.
Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema akiba ya fedha za Kigeni hadi jana ilikuwa Dola za Marekani bilioni 5.41; kiasi ambacho kinatosha kuagiza bidhaa za nje kwa miezi minne na siku 27.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 22, 2023; Mkurugenzi Utafiti na Sera wa benki hiyo, Suleiman Misango, amesema upungufu uliopo sasa wa fedha za kigeni ni himilivu kwakuwa akiba ipo ya kutosha.
Tangu vita vya Ukraine (Machi 2022 hadi Agosti 21, 2023), BoT imeuza Dola 5.18.5 milioni katika soko la fedha na kuanzia Julai Mosi hadi jana BoT ilikuwa imeuza zaidi ya Dola milioni 100 ikiwa ni ongezeko kubwa kuliko zaidi ya Dola milioni 62 zilizouzwa Julai hadi Septemba 2022.
Juni 8, 2023; Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba alinukuliwa akisema hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa zinaifanya Tanzania kuwa salama dhidi ya changamoto ya upungufu wa sarafu za kigeni ulioathiri nchi nyingi.
Miongoni mwa mataifa yaliyoathirika na upungufu wa dola ni Ghana, Misri, Zimbabwe, Nigeria na Kenya, ambayo baadhi yanafikiria kuweka kando matumizi ya dola katika biashara zake.
Hivi karibuni wakati wa mdahalo wa wadau wa sekta binafsi barani Afrika uliofanyika jijini Nairobi, Rais wa Kenya, William Ruto alitoa wito kwa mataifa ya Afrika kuwa na mfumo wao wa malipo na kuweka kando matumizi ya dola.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Tutuba alisema licha ya akiba ya fedha za kigeni kupungua nchini, hakuna changamoto hadi sasa.
Alisema Tanzania kila siku inauza hadi wastani wa dola milioni mbili, kiwango ambacho hakifikiwi na nchi yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Hadi Mei, mwaka huu, Tanzania ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni ya Dola bilioni 4.88 zinazotosha kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi minne na nusu, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita