Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
Imezitaja hatua hizo zinajumuisha uamuzi wa Marekani kulegeza masharti ya riba kwenye masoko yake ya fedha, kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na ya nchini na kuendelea kutoa bei elekezi na kufuatilia kwa karibu sekta ya fedha nchini.
Meneja Msaidizi Utafiti wa BoT, Dk. Lusajo Mwankemwa, amebainisha hayo alipotoa mada kuhusu majukumu ya taasisi hiyo benki hiyo wakati wa semina kwa waandishi wa habari, ambao walitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuimarisha upatikanaji dola nchini.
"BoT tunajua na tunaona dola zipo ila ni ngumu kukufuata kutaka tuchukue dola nyumbani kwako, mimi (BoT) nitasema dola moja ni kiasi hiki (bei elekezi).
"Siwezi kuja nyumbani kwako wewe uliyezihifadhi nikikwambie lazima kuuza kwa bei hii, BoT jukumu lake ni kutoa mwongozo wa kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikanaje," amesema.
Pia soma:
- BoT: Mnaoshikilia Dola mziweke sokoni kwenye mfumo rasmi