Benki Kuu Tanzania: Mlioficha Dola zirudisheni kwenye mzunguko

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1695642823361.png

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa, waziachie kwenye mzunguko wa Biashara, ili kuondoa uhaba wa Fedha hiyo Nchini.

Kauli ya BoT inakuja ikiwa ni wiki chache tangu Mkurugenzi Utafiti na Sera wa Benki hiyo, Suleiman Misango, aseme upungufu uliopo sasa wa Fedha za kigeni ni himilivu kwakuwa akiba ipo ya kutosha.

Hii kauli hii ya Benki Kuu inakupa tafsiri gani?
 
View attachment 2761849
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa, waziachie kwenye mzunguko wa Biashara, ili kuondoa uhaba wa Fedha hiyo Nchini.
...
Za serikali zikowapi ni aibu serikali kukosa akiba yakutosha kumpup soko mpaka listabilize
 
Hivi watu wa kitengo hawawezi kutoa taarifa nyeti kuhusu wahusika wakuu wenye kuhusika kuficha fedha za kigeni hasa dola za Kimarekani?

Yaani kweli BoT imefikia hatua ya kuishia kulalamika kuhusu upungufu uliopo katika mzunguko wa fedha za kigeni hapa nchini na kisha kuwapigia magoti wahujumu uchumi?

Taassi nyeti zinapaswa kuwachukulia hatua wahusika kwa kuwa wanafahamika, kama vile ambavyo alithubutu JPM kufanya. Ukiona serikali imeuchuna, huku taasisi yake nyeti ya fedha, BOT inalalamika, basi tambua inawagwaya wafanyabiashara na matajiri wakubwa, na hata inashindwa kuwachukulia hatua ijapokuwa inawatambua.

"Toothless bulldog"
 
Dhahabu sawa. Jee dhahabu si zinanunuliwa Kwa fedha? Jee hizo fedha za kununulia dhahabu za kuhifadhi tunazo??
Nchi yote hiyo Mkuu inashindwaje kununua dhahabu na kuweka reserve miaka yote hiyo
Ina maana nchi kama nchi pia haijui kujiwekea akiba kama kina sisi, haiwezekani mkuu hela zinapigwa kila siku za miradi na zingine zinatolewa

Angalia ziara ya PM kila mkoa kuna madudu na wizi wa kufa mtu

Siamini nchi haiwezi kuwa na akiba
Algeria nafikiri ndio wanaongoza kwa gold reserve Afrika pamoja na misukosuko yote lakini zimelala mahali
 
Back
Top Bottom