Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Tanzania kama Tanzania
Screenshot_20210317-183726.png
 
SITARAJII WAKENYA WAMPENDE RAIS MAGUFULI.

Na Thadei Ole Mushi.

Katika list ya Marais ambao waliwahi kuiongoza Tanzania, Rais Magufuli anaongoza kwa kuwa Rais anayeleta athari Hasi kwenye Uchumi wa Kenya. Ndio maana hizi chokochoko za kuchunguza JPM yupo wapi ana Hali gani vyombo vya habari vya Kenya navyo vinaimba na kufuatilia sana.

Twende sawa.....

1. UKUTA WA MERERANI

Kabla ya kujenga ukuta wa Mererani Kenya na India zilikuwa ndizo nchi zilizoongoza kwa kuuza madini ya Tanzanite. Mwaka 2013 kwa mfano India pekee iliuza madini ya Tanzanite yenye Thamani ya USD 300 Milioni Hadi Marekani ikawa inahoji Kama madini hayo yanachimbwa India au Tanzania.

Mwaka huo huo Kenya ilisafirisha na Kuuza nje Tanzanite yenye Thamani ya USD 100 Milioni. Wakati hayo yakifanyika Tanzania haikuweza hata kufikia mauzo ya USD 50 Milioni kwa mwaka 2013.

Toka ukuta huo ujengwa Kenya haijauza madini hata ya Buku ya Tanzanite nje ya nchi. Kenya inafahamu kuwa Kama Magufuli hatakuwepo Tanzania Basi huenda fursa hii ikafunguka Tena. Tumuombee Rais wetu... Fuata link ifuatayo kusoma athari za ukuta wa Mererani.

2. UJENZI WA RELI YA SGR.

Kuna watakaojiuliza Reli ya SGR inawahusu nini wakenya au ina athari gani kwa wakenya? Ni swali zuri Sana na kila anayejiuliza ni haki yake ajiulize.

Kama Kuna kitu kinawasumbua Kenya ni Mradi huu wa SGR. Tukumbuke kuwa issue hapa sio mataruma ya Reli Bali issue kubwa hapa ni bandari zetu Mombasa na Daresalam hili niliwahi kuwaambia na narudia Tena na Tena huenda hatuelewi Nini maana ya hii Vita tunayoizungumza.

Ipo hivi

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

"Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika....

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki Tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Daresalam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC - The East African - Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC

Hili Ni Gazeti la Kenya sio la Tanzania katika Hali Kama hii hawawezi kutufurahia sisi kupaa kiuchumi.

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.

3. MRADI WA STIGLERS GORGE.

Huu ni Mradi wa umeme ambao kufikia 2022 tunatarajia uwe umekamilia kabisa.

Mradi huu utatupatia megawatt 2,100 sawa na bwawa la Aswan la Misri ambalo nalo linatoa megawatt hizo 2,100.

Stiglers itakuwa bwawa Namba Moja Afrika yeye na Aswan kwa pamoja kwa kutoa megawatt nyingi na zinazolingana. Mabwawa Mengine yote yaliyobakia Afrika hayawezi kufikia kiwango hicho Cha Stiglers.

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga.

Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira....

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais wetu. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.

Linapokuja suala la kiuchumi kwa Dunia ya Sasa ni Vita. Na Kama hutoruhusu akili yako kufanya kazi Basi utajikuta ukiitikia chorus za nyimbo za mabeberu.

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?.....

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Sisi kujenga Stiglers tu imekuwa kelele kubwa. Nafikiri unaelewa Sasa na Kuna haja kubwa Sana ya kumuombea Rais wetu.

4. UJENZI WA VIWANDA NCHINI.

Sera ya Rais Magufuli toka ameingia madarakani Ni ujenzi wa Viwanda. Tafsiri ndogo tu Ni kwamba tunakwenda kuingia kwenye ushindani mkubwa Sana na Kenya kwenye kuuziana bidhaa. Maana yake Ni kuwa Kuna baadhi ya viwanda vya Kenya vitakufa kutokana na ujenzi wa viwanda nchini. Tukumbuke Soko kubwa la Kenya kwa bidhaa zake za viwandani Ni Kenya. Ingia supermarket kagua bidhaa nyingi zinatoka Kenya.

Kwa miaka ya karibuni Tanzania imeanza kuharibu dili hili la Kenya. Hata Panadol Sasa hatununui toka Kenya. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa Kenya ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda. Hii ni Vita.

Haya Ni mchache Kuna Mengine si ya kuyasema hapa. Na ndio maana huwa nasemaga Marais Kama JPM huwa hawapatikani Mara kwa Mara.

Ole Mushi
0712702602
 
Aisee good article.
 
Back
Top Bottom