Ndugu chukia wapinzani wako lakini ujue kuwa kama ulizaliwa mtanzania utabaki kuwa mtanzania tu, hata ukiidhalilisha nchi yako kwa uongo ujue unajiaibisha mwenyewe na wale unaowapambia hayo wanakuona mjinga vilevile na nakuahidi huna hata siku mbili utajutia huu uongo wako. Mimi ni mojawapo ninaependa mabadiliko ya uongozi Tanzania ila nakuhakikishia hata Tundu lisu hapo alipo kuna vitu tayari anajutia na hawezi kuendelea kuichafua Tanzania kwa mabeberu tena.
Iga mfano wa Wilbroad Silaa, alikua mpinzani na alikua mwakilishi wa Tanzania kwenye bunge la Ulaya kwa miaka tano ila hakuifitini nchi yake kwa wageni ingawa alikua bado chama pinzani. Jitathmini na utulize kichwa chako ufikirie utaifanyia nini Tanzania iweze kusonga mbele huku ukikumbuka kuwa LIFE IS NOT FAIR na life linapokupiga usimlaumu mtu hata kama yupo connected moja kwa moja na kuanguka kwako, mafanikio pekee ni kujifunza changamoto ulizopitia na kuendelea kusonga mbele kwa kujihami. "Chui ni mla nyama ila anapoenda kuwinda kama watoto wake hawajajificha ipasavyo anaweza kuja na nyama akute watoto wake walishakuwa kitoweo cha fisi lakini hamzuii kuendelea kuzaa" Jifunze kupambana na changamoto utashinda sio kulaumu wenzako