Kitu ambacho kinafanya miji ya nchi zilizoendelea kuwa vivutio vikubwa ni kwa sababu wanaongeza thamani wa maeneo waliyonayo. Mfano Paris, ni inland city inapitiwa na mto seine, wakati wa winter hali ya hewa baridi unaweza hata ukakimbia. Lakini vitu kama eiffel tower, the Louvre museum, french cuisine na Notre dame cathedral vinavuta watu zaidi ya milioni 40 kwa mwaka kutembelea Paris na haijalishi hofu ya mashambulio ya kigaidi, watu wanazidi tu kwenda. Lakini jiji kama Dar, Location nzuri, white sand beaches, tropical climate nk, tuna watalii wachache sana. Tubadilike na kuleta thamani katika vitu tulivyonavyo tayari. Kwa mfano tena wa jiji lililokuwa na maendeleo sawa na Dar ni Dubai. Dubai ni jiji lililoko jangwani. Ni mafuta na beach tu ndo vilivyoisaidia Dubai. Wametengeneza vivutio vingi kiasi kwamba Dubai inaipita New York kwa idadi ya watalii kwa mwaka hivi leo wakati miaka kumi iliyopita Dubai ilikuwa hewa tu. We need to change. Sipendi notion ya kuziangalia eti nchi nyingine za kiafrika kuhusu maendeleo eti kisa wao wamefanya na sisi eti tufanye, hapana, tufanye vitu ambavyo waafrika wengine hawafanyi. Kama hakuna jiji Afrika lenye subway, tuwe wa kwanza kuwa na subway, wanasema "work hard till your enemies ask if you are hiring". I believe Tanzania inaelekea huko. We just need people full of great Ideas and Cash to transform this country.