Hilo la bichi kuwa na mchanga mweupe wabongo wengi tunalichukulia poa sana kwasababu tumekua wakiona bichi zina mchanga huo. Ila asikwambie mtu bichi zetu nzuri aisee, nchi nyingine beach zina mawe mawe, mchanga kama kokoto ndogondogo lakini jamaa wanakomaa hivyo hivyo kweye utalii, sisi mchanga mwembamba, laini, mweupe lakini tumezubaa zubaa tuu.
Nilikuwa nawashangaa jamaa zangu flani wanasifia Grand Canyon, nikasema hivi kuna nini hapo zaidi ya bonde na ukame lakini cha kushangaza watalii wanamiminika kila mwaka. Tatizo letu watanzania (kiujumla) tuna hulka za kutokujiamini, hatuthamini vya kwetu, hatujitangazi na kuweka mikakati kama nchi ya kutumia fursa.
Awamu hii imeanza na hilo la kujiamini, kwa kutuonesha wananchi kuwa uwezo wa kufanya mambo makubwa tunao tena kwa fedha zetu, uwezo wa kuwadindishia Barick na wachina kwenye mikataba yao ya kilaghai tunao. Hii wengi wa kizazi chetu tunaweza tusiione ila wale madogo wanaokua sasa watakuja kuwa watu wakujiamini sana na hii itaweza saidia katika kuchangamkia fursa za kiuchumi.
Tutafika tuu.